Yaya Toure amshutumu Pep Guadiola kuwa anawabagua wachezaji kutoka Afrika

Rotation yake yeye na Silva? uyo kocha kaugua ? wabongo bana Pana chakulalamika hapo ?

Kama ni hivyo basi angemruhusu kusajiliwa na timu zingine zilizokuwa zikimhitaji wakti ule (msimu wa 15/16/ na 16/17 au 17/18) badala ya kumzuia au na hii waionaje?
 
Kubali au ukatae, Yaya Toure ndiye alikuwa mchezaji influential sana Manchester City wakati wa Roberto Mancini na Emmanuel Pellegrino.

Au umesahau hiyo?

Yaya Toure hajawah kuwa Zaidi ya Silva hata siku moja.
Nahuo wakati wa Mancini unaozungumzia weye ndiomana timu ilikua very average kutokana na wachezaji kama yeye, Na saivii timu ni tishio kabisa kutokana na kuleta wachezaji wenye ubora.
 
Yaya Toure hajawah kuwa Zaidi ya Silva hata siku moja.
Nahuo wakati wa Mancini unaozungumzia weye ndiomana timu ilikua very average kutokana na wachezaji kama yeye, Na saivii timu ni tishio kabisa kutokana na kuleta wachezaji wenye ubora.

Mkuu, uko serious kweli unaita ile timu ilikuwa average?

Lakini Silva si amecheza na Yaya Toure timu moja pamoja na Mario Balotelli?

Mbona unasahau ukweli kwamba Manchester imetwaa ubingwa wa Ligi kuu ya England Toure akiwa na huyo Silva?
 
Mkuu, uko serious kweli unaita ile timu ilikuwa average?

Lakini Silva si amecheza na Yaya Toure timu moja pamoja na Mario Balotelli?

Mbona unasahau ukweli kwamba Manchester imetwaa ubingwa wa Ligi kuu ya England Toure akiwa na huyo Silva?

Ilikua average, City ya mwaka huu haijawahi kutokea, nafikiri record zote za nyuma wamevunja. Wameiguza ligi kuwa one horse race, hiyo unayoizungumza weye haikuahi kufanya hivo.
 
Ilikua average, City ya mwaka huu haijawahi kutokea, nafikiri record zote za nyuma wamevunja. Wameiguza ligi kuwa one horse race, hiyo unayoizungumza weye haikuahi kufanya hivo.

Hiyo haina ubishi ingawa hawakuweka rekodi ya kutofungwa msimu mzima.

Ila tukirudi kwenye mada ni kwamba Guadiola anashutumiwa kwa ubaguzi dhidi ya wachezaji wa kutoka Afrika.

Hiyo ni shutuma nzito na Machester City bado wanaitafuna na wamekataa kujibu mapigo.

Ila kuna maoni mengine kutoka sehemu mbalimbali kumhusu Guadiola.

Hata mimi naweka mashaka kidogo kutokana na suala la aina ya mtindo ambao Guadiola anataka wachezaji wacheze wawapo uwanjani.

Inawezekana wachezaji wengi kutoka Afrika huwa hawafuati maelekezo vile inavyotakiwa na kuamua kujichezea "chandimu" kwamba liwalo na liwe.

Lakini hii itakuwa ni kujidhalilisha kukubali kwamba pamoja na unyota wao nao wachezaji hawa bado wana mapungufu katika suala la kufuata maelekezo ya meneja anataka nini.

Ndiyo maana Fernandinho ametumika sana labda kutokana na utaalam wa wachezaji kutoka Brazil

Sasa Fernandinho na Yaya Toure nani alikuwa analipwa zaidi pale Manchester City?

Yaya Toure alikuwa akilipwa pauni 200,000 kwa wiki zaidi ya Fernandinho na Silva!

Je, alikuwa alilipwa fedha hizo kutokana na jina tu ama uchezaji wake awapo uwanjani?
 
Lile likipara Nilibaguzi lakupindukia ndo macatalonia yalivo ni mabaguzi yakiwango cha juu
 

Mazingira mkuu, Yaya alisainiwa kwa mkataba mnono kutokana na mazingira aliosainiwa ya kugombeana na timu nyengine, isitisho nafikiri kama jamaa humfahamu jinsi alivokua anatikisa kibiriti kilasika kwa lengo awe anaengezewa mshahara mara kwa mara, je uliwahi ona Silva kaleta drama ili aengezewe mshahara?

Kuhusu suala la ubaguzi ni uzushi tu, waafrika tuna matatizo sana tunapokosa kitu tu tunafukuzia kwenye kubaguliwa.
Katika mchezaji aliekua anachukiza kwa washbiki wa Barcelona basi ni keita, na alikua anapendwa sana na Pep. unamkuta yupo katikati ya kina Messi, Xavi na Iniesta. kuachwa kwa Yaya ilitafsiriwa ni ubaguzi lakini keita na Abidal kuendelea kucheza kwenye timu watu hawakuliona.

Kuihalisi yaya yupo too slow kuweza kufit kwenye standard ya Pep, na uwezo wake huwezi ufananisha na wa Silva au De bruyn. Na hata kwa position Dm Fernandinho anacheza vizuri zaidi kuliko yaya.
 

Nimekupata hapo.

Seydou Keita aikuwa ni DM na Eric Abidal alikuwa ni beki mshahara wa kushoto au beki wa kati.

Hawa wawili hawakuwa na mbadala kwani pale Barca hata Maxwell alipoletwa na Pep Guadiola hakuweza kumtoa Abidal kwenye hiyo nafasi.

Keita unafahamu release clause yake kutoka Sevilla kwenda Barca ilikuwa ni kiasi gani? Euro milioni 90.

Ila Pep angeweza hata kumchezesha Yaya Toure mechi ambazo si more competitive badala ya kumuacha kabisa nje akasugua bench.

Hali hii huleta sintofahamu kubwa.

Au labda tuseme pia kwamba kwa kuwa Yaya Toure alikuwa ni attacking midfielder basi hakuwa na uwezo wa kushawishi mechi zipi acheze.

Au asiyo?
 
Yaya alikuwa DM. Ndio maana aliwekwa benchi ili mtoto wa nyumbani Sergio Busquet apate nafasi.
 
Jamaa dume zima lina mambo ya ajabu kabisa. sijui anajihisi kama anakiwango kama cha iniesta au modric nahisi.

Kuna kipindi alinuna kisa timu haijamfanyia birthday !!!!!!!!!
Nikiweka kando kinachojadiliwa kuhusu ubaguzi wa pep dhidi ya waafrika,Yaya anatabia za ajabu sana za kilialia.

Kama unakumbuka kipindi fulani BBC walitoa tuzo ya mwanasoka bora wa Africa, walimpa Auba,Yaya alilaani utafikiri yeye pekee ndio anafaa kuwa mwanasoka bora.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…