Yemen: Tutageuza Bahari Nyekundu kuwa kaburi la muungano unaoongozwa na Marekani iwapo wutaamua kuchukua hatua yoyote dhidi ya Yemen

Yemen: Tutageuza Bahari Nyekundu kuwa kaburi la muungano unaoongozwa na Marekani iwapo wutaamua kuchukua hatua yoyote dhidi ya Yemen

Kama kuna Taifa limewahi pigana na USA na Israel likafanikiwa basi bado halijazaliwa, wanapoteza mda.
🤣 🤣 🤣 israhell ipi hii ambayo wanamgambo wake wa idf wanaoana vitani
Au israhell ile inayopelekewa moto na wanamapambano wa hamas
 
Njaa ya chakula tu inaendelea kuua wengi huko, vita wataiweza?
Ujinga ni mzigo
Hata Afghanistan njaa iliwatesa sana ila United shit of Americant na shosti zake walikimbizwa
Kuna muda hio hio njaa ndio inawafanya watu washinde
Mido ist inataka kuji restart ishaona ujinga wa united shit of Americant
Leo muungano unaoundwa na United shit of Americant mpaka saudia anaugomea bado tu hujaelewa
Houthi kundi teule
 
Yemen si ya kutishiwa na Mtu Saud Arabia alijifanya Superpower kujiona ana ndege sijui F15 na Europe fighter Typhoon na silaha za kila aina aliwakusanya UAE, US, Israel, Baharain, Morocco ,Egypt, Jordan wakapeleka F16 na Kuwait F18, na Qatar Mirage pamoja na Sudan na Pakistan walipeleka majeshi yao walikimbia mmoja mmoja wakabaki Saud Arabia na UAE badaye UAE akakimbia ikabaki anawasapoti wa pinzani kule South Yemen, ilibidi Saud Arabia akaombe poa nao kwa njia ya Oman .

America na Israel hawamuwezi hata wajikusanye vipi
Bahrain peke yake ndie kakubali kuburuzwa kuingia katika huo muungano wa kijanja.Qattar wamemtolea ukali lord Austin na kumwambia hawaingii kwenye muungano huo.
Nakubaliana na wewe hayo mataifa yote hayatamuweza maskini Yemen.Si kwamba Yemen ana silaha kuwashinda wao lakini nia yao ndio nguvu kubwa itakayowapa ushindi.Kwa upande wa pili kitakachowashinda hayo mataifa ni hofu ya kufungua uwanja mwengine wa vita unaoweza kuleta maambukizi ya vita vibaya .
Mwishowe ili kuepuka kipigo cha Houth wataachia Gaza mikononi mwa Hamas na wapalestina wenyewe na itakuwa ndio mwisho wa vita na itakuwa ushindi kwa Hamas chini ya tufani la Alaqsa.
Ingelikuwa kila nchi ndugu na wapalestina inatumia nafasi yake kama Yemen basi vita vingeisha mapema kwa aibu kubwa ya Israel na Marekani.Na sasa ushindi unakuja kwa kuchelewa la kuficha aibu za walioshindwa.
 
Wanaukumbi.

Waziri wa Ulinzi wa Yemen Meja Jenerali Mohammad al-Atifi:
Amesema kuwa Vikosi vya Wanajeshi wa Yemen vitageuza Bahari Nyekundu kuwa kaburi la muungano unaoongozwa na Marekani iwapo muungano huo utaamua kuchukua hatua yoyote dhidi ya Yemen.

======

🇾🇪🇺🇸 Yemeni Defense Minister Major General Mohammad al-Atifi:

The Yemeni Armed Forces will turn the Red Sea into a graveyard of the US-led coalition if the alliance decides to take any action against Yemen.

======

Mpaka sasa makumpuni makubwa ya meli Dunia yamesimamisha meli zao kupita Bahari Nyekundu.

Moja ya kampuni kubwa zaidi za usafirishaji wa meli duniani, Maersk, ilisema Iilikuwa inasimamisha meli zake kupitia njia kuu ya Bahari Nyekundu kufuatia mashambulizi ya waasi wa Houthi wa Yemen.
Maersk, ambayo inamiliki kundi la meli 300, katika tangazo la Jumamosi. Ikizingatiwa kuwa takriban 12-14% ya biashara ya kimataifa hupitia Mfereji wa Suez, hili ni tukio muhimu ambalo linaweza kuathiri njia za biashara za kimataifa na bei za bidhaa nchini Israel.

Kampuni ya usafirishaji ya Ujerumani ya Hapag-Lloyd ilitangaza pia kuwa inasimamisha usafirishaji wa meli za Bahari baada ya moja ya meli zake kushambuliwa na Houthis.

Kampuni ya meli ya Hong Kong ya OOCL (Orient Overseas Container Line) ilitangaza kwamba "kutokana na matatizo ya uendeshaji," itaacha mara moja kusafirisha mizigo kwenda na kutoka Israel
Yahya Saree, msemaji wa Jeshi la Yemen:


View: https://x.com/me_observer_/status/1737102785848512969?s=46&t=mTROWpaJUT8H393JMgWOvw

Yemen?
Hana ubavu huo.

Mgambo wetu wa kikosi kimoja tu wanatosha kabisa kuiteka Yemen nzima.
 
Yemen failed state anatishia viranja wa dunia🤣😅😂
Huyo kiranja wa dunia si ndo alipigwa nchini Somalia akakimbia na kuwatelekeza wanajeshi wake wakazungushwa mitaani wakiwa uchi?
Huyo kiranja si juzi tu kaikimbia Talban baada ya kupambana nao zaidi ya miaka 20?
Huyo kiranja si ndo alipakatwa mchana kweupe nchini Vietnam akakimbia na chupi mikononi?

Punguza mihemko vita sio lelemama.
 
Yemen?
Hana ubavu huo.

Mgambo wetu wa kikosi kimoja tu wanatosha kabisa kuiteka Yemen nzima.
Marekani anajua wazi peke yake hawezi ndiyo maana anataka muungano, huo unaoongozwa na Marekani, unajumuisha Uingereza, Canada, Ufaransa, Italia, Uholanzi, Norway, Seychelles, Uhispania, na haswa, Bahrain-taifa pekee la Kiarabu linaloshiriki katika muungano huo nchi zingine zinasema zitashiriki lakini zinaomba zisitajwe unajua sababu gani wanaogopa.
Weww ufahamu chochote kuhusu Yemen jiulize kwa nini wamejikusanya wote kupambana na Yeme😂
 
Operesheni za majini za Yemen zinalenga kuwaunga mkono wananchi wa Palestina katika kukabiliana na uvamizi na mzingiro wa Gaza, na sio onyesho la nguvu wala changamoto kwa mtu yeyote. Yeyote anayetaka kupanua mzozo lazima abebe matokeo ya matendo yake. Muungano ulioundwa na Marekani ni wa kuilinda Israel na kuilinda bahari bila uhalali wowote, na hautaizuia Yemen kuendelea na operesheni zake halali za kuunga mkono Gaza, kama vile Amerika ilivyojiruhusu kuiunga mkono Israel kwa kuunda muungano na bila ya muungano, wananchi wa eneo hili wana uhalali kamili wa kuwaunga mkono wananchi wa Palestina, na Yemen imejitwika jukumu la kutetea haki ya Palestina na dhulma kubwa ya Ghaza….
Jamani hii ngoma ya Red sea inaenda kuiharibu nchi ya Yemen ambayo ilikuwa inaanza kutulia kidogo, huyo Yemen anataka kuua rais wake, vita itaanza askari wa Yemen wataenda kujificha kwa raia na miskitini, kitakachotokea ni maafa makubwa, miaka ya nyuma kipindi cha mzozo wa USA na Iraq watu wengi mkiongozwa na kauli za hasan chemical mlisema wanajeshi wa USA watachujwa wote zitarudi maiti na Iraq itashinda vita, Ghadaf hivyo hivi,
Hamas hivo lakini tumeshuhudia maafa makubwa sana kwa upande wa nchi za kiarabu,
 
Uzuri wa Marekani huwa hana shughuli ndogo. Unakumbuka enzi zile za maharamia wa kisomali walivyokua wanateka meli kwenye pembe ya Africa,??
Mkuu kwa sasa Mmarekani anaweza akapata shida sana kuwashughulikia hao Wayemen. Hii ni kwa sababu Marekani ameshavunja uhusiano na Russia kwa kuwasaidia Ukraine. Kabla ya hapo haikuwa rahisi kwa Russia kuisaidia waziwazi nchi kama Iran, North Korea na nchi nyingine za kaliba hiyo. Kwa kipindi hiki Russia, China. North Korea na Iran wanaweza kumsaidia Yemen ili kumharibia Mmarekani. Vilevile, usidhani Yemen anajitutumua tu bila kuwa na backup, kuna nchi zinazomchochea kufanya hayo ayafanyayo.
 
ngoja waje wapakatwe tuanze free yemen
Unajuwa tujifunze na history, kuna nchi hajizajawahi kuwa matajiri na wakasimama imara, ziko nchi sio kwamba wana dhana za kisasa za vita ila wanawapiganaji, kuna watu wanajuwa kupigana vita kuwa na ushujaa, Afghanstan wameshapigana mpaka na NATO lakini ni majeuri sana, Hawa Yemen wameshambuliwa mwaka sijui wa gapi huu na matajiri wa Gulf lakini wameomba poo wenyewe vita haishi. Siku hizi haya ma drones ni hatari vinarushwa na kupiga. Ziko nchi kuzikalia huwezi hata hapo Somali tumeyaona.
 
Kwa mujibu wa waziri mkuu wa UK ni kwamba hao wa Yemeni nyuma yake kuna mrusi na muirani ambao wanataka kupandisha bei ya mafuta na bidhaa ili uchumi wa nchi za magharibi uvurugike.
Putin anataka auze wese kwa Bei mbaya..sasa mkong'oto ukianza nani atawasaidia hao iran na urusi hawataonekana.
 
Kwa kipindi hiki Russia, China. North Korea na Iran wanaweza kumsaidia Yemen ili kumharibia Mmarekani. Vilevile, usidhani Yemen anajitutumua tu bila kuwa na backup, kuna nchi zinazomchochea kufanya hayo ayafanyayo.
Iran ndo anaweza kufanya hivyo.
China hathubutu, anaogopa yale yaliyomkuta Mrusi kwa mali zake kupigwa pini. Wachina wanajali sana uchumi wao.
Hata Russia akifanya ni kwa kificho sana, na saivi pumzi hana.
 
Hili Jukwaa lina maajabu. Kumbe mpaka Yemen ni anaweza ipiga US? Du kumbe saiv mataifa yote ya Kiarabu wanaweza mkunguta super power? Kweli US kajichokea
Nadhani unapotosha kidogo, USA ni super power wala hakuna mtu kasema Yemen atampiga US ila sasa kama USA wanamalengo ya wazi katika hili ni kuhakikisha meli zinapita salama na kuzuia hawa jamaa kuzuia njia, sasa ikitokea USA wako wana patrol lakini meli hazipiti kuogopa ikiwa imezuiwa au bado hazijisii usalama hapo ndio ushindi wa Yemen ila wakiweza kurudisha amani ya njia hapo US wameshinda.
 
Hili Jukwaa lina maajabu. Kumbe mpaka Yemen ni anaweza ipiga US? Du kumbe saiv mataifa yote ya Kiarabu wanaweza mkunguta super power? Kweli US kajichokea
Hahaha..
Mkuu, hizo ni propaganda za wafia dini ya mudi
 
Huyo kiranja wa dunia si ndo alipigwa nchini Somalia akakimbia na kuwatelekeza wanajeshi wake wakazungushwa mitaani wakiwa uchi?
Huyo kiranja si juzi tu kaikimbia Talban baada ya kupambana nao zaidi ya miaka 20?
Huyo kiranja si ndo alipakatwa mchana kweupe nchini Vietnam akakimbia na chupi mikononi?

Punguza mihemko vita sio lelemama.
Afgan kakaa miaka 20 kaachia koloni ulitaka akae kuna nini pale. Yaani somalia pqlqkavu vile kiranjaa aangaike napo yeye anaenda sehem ananyosha magaidi na kuondoka
 
BREAKING:

⚡ 🇮🇱🇲🇾Vikwazo dhidi ya uagizaji-uagizaji wa meli wa Israel vinazidi kuwa kimataifa polepole. Malaysia yapiga marufuku kampuni ya usafirishaji ya ZIM yenye makao yake nchini Israel kuingia katika bandari za nchi hiyo, uamuzi huo utaanza kutekelezwa baada ya wiki 4.

Marufuku hiyo pia inahusu meli nyingine yoyote inayosafiri chini ya bendera ya Israel au wale wote wanaokuja au wanaopanga kuhamia Israel.

Vita vinapigananwa kwa njia nyingi.
 
Back
Top Bottom