Tulimlea sana Manara akitukana watu kwa kigezo cha utani na kuwakera utopolo,sasa huyo katugeuka! Tunaenda kufanya kosa jingine la kumchekea Mo,kila kinachosemwa juu yake jibu linakuwa rahisi tu "shida yetu makombe" ashawahi kusema anajitoa siku flan hivi alisusa watu walichanganyikiwa,akabembelezwa yakaisha,Kwasasa ipo kama anatafuta sababu hivi,tuwe wa kweli hivi alichofanya ni sawa? Kulipa ada ya usajili ndio nini kwa mfano,mbona hajanipa mimi hiyo pesa kampa chama? Si kwavile anatumikia na anastahili? Kwenye hili Mo kachemka sio la kumtetea,na hii ni mbaya sana kama huu mtifuano wao watauweka hadi kwa wachezaji! Hivi chama kajisikiaje baada ya jibu la bosi? Viongozi wa simba wajipange sana huwa uwekezaji ukamilike watu wanunue hisa,simba isimame yenyewe bila hivyo ipo siku Mo atakuja kusepa ghafla tu na timu itayumba