Yericko Nyerere: Mwanasiasa bora wa upinzani

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Habari wapendwa.

Leo tena nimeamua nitumie haki yangu ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni bila kuvunja sheria. Ingawa bado hakuna chama mbadala wa CCM hadi sasa lakini tukiri kuna baadhi ya wapinzani wana siasa nzuri zinazofaa kimaendeleo. Mfano mzuri ni mwanasiasa Yericko Nyerere ambaye pia ni jasusi huko ufipani.

Yeriko ni kijana tegemeo kwa chama chake hasa nyakati hizi. Kwangu mimi Yeriko ana vitu tofauti sana na wanasiasa wengine wa upinzani hasa upande wa vijana. Vijana wengi wa upinzani wameonyesha udhaifu mkubwa sana kisiasa hadi wanatia aibu. Kwanini nasema Yeriko ni bora?

Kwanza jamaa ni msomi. Elimu yake haina mashaka. Kwa mujibu wa maandishi yake mwenyewe amejitambulisha kama mhandisi wa umeme ingawa hakutaja kasomea wapi na lini. Taarifa zisizo rasmi zinasema kasomea VETA Mufindi. Pia elimu yake ujasusi aliyosomea Uingereza inamweka kwenye viwango vya juu. Pili kaonyesha kuwa siasa ni sehemu tu ya maisha yake lakini ana shughuli zake za halali za kujiingizia kipato. Ni mwandishi mahiri wa vitabu. Pia ni mmiliki wa ranch ya mbuzi katoliki. Kimsingi jamaa kajipanga na ni mchapakazi.

Baada ya wasifu wake huo mdogo kwa mujibu wa taarifa zake, turudi kwenye shuguli zake za kisiasa ambazo zinamfanya awe mwanasiasa bora. Yeriko kaonyesha nidhamu kubwa sana kwa uongozi wa chama chake kwa maana ya mwenyekiti Mbowe. Katika misukosuko yote kaonekana akiwa upande wa mwenyekiti. Kisiasa ni muhimu sana kijana kuwa mtiifu kwa wakubwa hasa ule upande wenye maamuzi. Pamoja na utiifu pia wakati mwingine Yeriko hujitahidi kutoa mawazo yake binafsi kwenye mambo ya chama chake. Wakati Nasari kavuliwa uanachama kwa sababu za kutohudhuria bungeni, Yeriko alikosoa kitendo cha Nasari kutohudhuria bungeni na kushauri wabunge wengine wa chama chake kutofanya mambo ya kitoto yanayoweza kuepukika. Jambo lingine linamtofautisha Yeriko na vijana wa Bavicha ni uvumilivu. Hapa mtandaoni wanasiasa wengi vijana wa CHADEMA hupandwa na hasira haraka sana ukitofautiana nao hoja. Hutukana na ku-block. Ndugu Malisa ni kinara wa kublock akifuatiwa na Maria tsehai. Yeriko katika hilo kaonyesha ukomavu. Pia Yeriko ni mbobezi wa mahakama ya Kisutu kwahiyo angalau anafahamu ladha ya kuwa mwanasiasa upinzani.

Kasoro ya Yeriko ni ile kuwaita vijana wa CCM kwa jina la vibaka wa Lumumba. Hakika hii ni kauli ya kukera sana. Kwa kumalizia nimpongeze Yeriko kwa siasa anazozifanya. Ikimpendeza afanye kuwasiliana na Mh Polepole apewe kadi ya CCM.
 
Hongera zake jasusi mbona alivyomshauri rais kuhamia Dodoma na akatoa sababu za kiusalama hukusema humu wakati rais alitekeleza mawazo yake
 
Unasema elimu yake haina mashaka alafu wakati huo huo unasema hujui kasomea wapi chuo? Hakika upunguani ni tatizo kwenye hii nchi
Nimeandika kwa mujibu wa taarifa alizoandika yeye mwenyewe. Ulitaka niseme kitu nisichokijua?
 
Wapi umeandika kwa mujibu wa alivyosema yeye?
Uzi unaeleza kana kwamba wewe ndiye unamuelezea, sio yeye anajielezea, sasa iweje useme kwa mujibu wake?
 
Soma vizuri usikurupuke.
Soma vizuri usikurupuke.

Nimesoma vizuri na ndio maana nimekuambia kuwa huwezi sema elimu ya mtu haina shaka wakati huo huo huna taarifa ya vyuo alivyosomea? Labda uwe punguani.

Wewe umechukua taarifa zake, ukamuelezea kwa akili yako kuwa elimu yake haina shaka, muda huo huo unasema hujui kasomea chuo gani, muda huo huo unasema kuwa kasomea "uingereza" hapa ndio ukazidi kuvurunda, je ni chuo kiitwacho uingereza au kasomea nchini Uingereza?
Ulipaswa useme kasomea Chuo fulani nchini uingereza tena ungetaja na mwaka kabisa kama ushahidi kusapoti statement yako kuwa "elimu yake haina shaka"

Lako huko kote holaa!

Ngoja nikuache maana hujui hata nazungumzia nini
 
Unasema elimu yake haina mashaka alafu wakati huo huo unasema hujui kasomea wapi chuo? Hakika upunguani ni tatizo kwenye hii nchi
Mimi hata simwelewi kaandika nini. Hukuhandisi halafu kasomea veta pia mbonezi ktk uandishi lkn hajui hiyo gani kaipata wapi Sasa ndo nn?
 
Umekuja kujisifia.

Ila we jamaa huwa unaforce ukubalike Ila kiukweli haukubaliki hata kwa wanachadema wenzio.
 
Nimesoma vizuri na ndio maana nimekuambia kuwa huwezi sema elimu ya mtu haina shaka wakati huo huo huna taarifa ya vyuo alivyosomea? Labda uwe punguani.

Wewe umechukua taarifa zake, ukamuelezea kwa akili yako kuwa elimu yake haina shaka, muda huo huo unasema hujui kasomea chuo gani, muda huo huo unasema kuwa kasomea "uingereza" hapa ndio ukazidi kuvurunda, je ni chuo kiitwacho uingereza au kasomea nchini Uingereza?
Ulipaswa useme kasomea Chuo fulani nchini uingereza tena ungetaja na mwaka kabisa kama ushahidi kusapoti statement yako kuwa "elimu yake haina shaka"

Lako huko kote holaa!

Ngoja nikuache maana hujui hata nazungumzia nini
Usilazimishe niandike unavyotaka wewe.
Mimi hata simwelewi kaandika nini. Hukuhandisi halafu kasomea veta pia mbonezi ktk uandishi lkn hajui hiyo gani kaipata wapi Sasa ndo nn?
Sijaandika ili wewe uelewe.
 
Ujasusi wa Yericko Nyerere ndani ya Chadema ni sawa na ujasusi wa jamaa anaitwa Bollen Ngetti ndani ya CCM ila kwa sasa yuko jela. Hawa vijana ni hatari sana kwa muatakabali siasa za nchi hii. Kama huyo Bollen anadaiwa kufungwa lakini gereza aliko halijulikani. Kitengo hatari sana.
 
Umekuja kujisifia.

Ila we jamaa huwa unaforce ukubalike Ila kiukweli haukubaliki hata kwa wanachadema wenzio.
Mpuuzi sana huyu jamaa.
Ana ID fake kibao. Anajianzishia uzi
Wa kujisifu ili akubalike.

Anatumia nguvu kubwa aonekane mwanasiasa bora na Mwandishi (Mzee wa Ku copy)
 
Kwanza jamaa ni msomi. Elimu yake haina mashaka. Kwa mujibu wa maandishi yake mwenyewe amejitambulisha kama mhandisi wa umeme ingawa hakutaja kasomea wapi na lini. Taarifa zisizo rasmi zinasema kasomea VETA Mufindi
Hakyanani wewe unaweza kuua mtu kwa kicheko. Kwamba jamaa ni msomi ... elimu yake haina mashaka ..... kasomea VETA Mufindi
Mbavu zangu mie 😂😂🤣🤣
 
Habari wapendwa.

Leo tena nimeamua nitumie haki yangu ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni bila kuvunja sheria. Ingawa bado hakuna chama mbadala wa CCM hadi sasa lakini tukiri kuna baadhi ya wapinzani wana siasa nzuri zinazofaa kimaendeleo. Mfano mzuri ni mwanasiasa Yericko Nyerere ambaye pia ni jasusi huko ufipani.

Yeriko ni kijana tegemeo kwa chama chake hasa nyakati hizi. Kwangu mimi Yeriko ana vitu tofauti sana na wanasiasa wengine wa upinzani hasa upande wa vijana. Vijana wengi wa upinzani wameonyesha udhaifu mkubwa sana kisiasa hadi wanatia aibu. Kwanini nasema Yeriko ni bora?

Kwanza jamaa ni msomi. Elimu yake haina mashaka. Kwa mujibu wa maandishi yake mwenyewe amejitambulisha kama mhandisi wa umeme ingawa hakutaja kasomea wapi na lini. Taarifa zisizo rasmi zinasema kasomea VETA Mufindi. Pia elimu yake ujasusi aliyosomea Uingereza inamweka kwenye viwango vya juu. Pili kaonyesha kuwa siasa ni sehemu tu ya maisha yake lakini ana shughuli zake za halali za kujiingizia kipato. Ni mwandishi mahiri wa vitabu. Pia ni mmiliki wa ranch ya mbuzi katoliki. Kimsingi jamaa kajipanga na ni mchapakazi.

Baada ya wasifu wake huo mdogo kwa mujibu wa taarifa zake, turudi kwenye shuguli zake za kisiasa ambazo zinamfanya awe mwanasiasa bora. Yeriko kaonyesha nidhamu kubwa sana kwa uongozi wa chama chake kwa maana ya mwenyekiti Mbowe. Katika misukosuko yote kaonekana akiwa upande wa mwenyekiti. Kisiasa ni muhimu sana kijana kuwa mtiifu kwa wakubwa hasa ule upande wenye maamuzi. Pamoja na utiifu pia wakati mwingine Yeriko hujitahidi kutoa mawazo yake binafsi kwenye mambo ya chama chake. Wakati Nasari kavuliwa uanachama kwa sababu za kutohudhuria bungeni, Yeriko alikosoa kitendo cha Nasari kutohudhuria bungeni na kushauri wabunge wengine wa chama chake kutofanya mambo ya kitoto yanayoweza kuepukika. Jambo lingine linamtofautisha Yeriko na vijana wa Bavicha ni uvumilivu. Hapa mtandaoni wanasiasa wengi vijana wa CHADEMA hupandwa na hasira haraka sana ukitofautiana nao hoja. Hutukana na ku-block. Ndugu Malisa ni kinara wa kublock akifuatiwa na Maria tsehai. Yeriko katika hilo kaonyesha ukomavu. Pia Yeriko ni mbobezi wa mahakama ya Kisutu kwahiyo angalau anafahamu ladha ya kuwa mwanasiasa upinzani.

Kasoro ya Yeriko ni ile kuwaita vijana wa CCM kwa jina la vibaka wa Lumumba. Hakika hii ni kauli ya kukera sana. Kwa kumalizia nimpongeze Yeriko kwa siasa anazozifanya. Ikimpendeza afanye kuwasiliana na Mh Polepole apewe kadi ya CCM.
Yerko ni CCM kindakindaki
 
Back
Top Bottom