Yericko Nyerere na historia ya African Association

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Kumekuwa na shinikizo kubwa sana kwangu kutoka kwa ndugu na jamaa kuwa nijibu maneno ya Yericko Nyerere kuhusu historia ya African Association (AA).

Wengi waliomsikiliza Yericko katika kipindi cha TV ya Star Times hawakupendezewa na jinsi Yericko Nyerere alivyoeleza historia hiyo na kuiita AA chama cha ‘’walevi.’’

Yericko anawataja viongozi wa AA President Cecil Matola yeye anamwita ‘’Cecilia’’ ambalo ni jina la kike.

Anaendelea kusema kuwa Secretary Kleist Sykes ametolewa Uzulu wakati wa Vita Vya Kwanza na Vya Pili Vya Dunia.

Kleist Sykes kazaliwa Pangani mwaka wa 1894 na ni mtoto Sykes Mbuwane na mama yake jina lake Kwemah kabila yake Mnyaturu.

Sykes Mbuwane ametoka Imhambane, Mozambique.

Waasisi wa AA ni Cecil Matola, Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamis, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Rawson Watts na Raikes Kusi.

Yericko kazungumza mambo asiyoyajua anachanganya miaka na taarifa kwa hakika ni vichekesho vitupu.

Jengo la African Association limejengwa na wanachama wenyewe kwa kujitolea kuanzia mwaka wa 1929 hadi 1933.

Jengo ambalo lilijengwa New Street kona na Kariakoo lilifunguliwa na Gavana Donald Cameron ambae Yericko anamwita Edward Cameron.

Jengo lililojengwa Stanley Street ni jengo la Al Jamiatul Ismaiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) chama kilichoanzishwa na wanachama Waislam waliokuwa pia ni wanachama wa AA.

Hayo mengine sioni sababu ya kuyasemea.

Historia yote ya AA iliandikwa na Kleist Sykes kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Mswada huu ulikuja kuchapwa mwaka wa 1973 kama sura katika kitabu alichohariri John Iliffe, "Modern Tanzanians," Daisy Sykes Buruku, "The Townsman: Kleist Sykes UK. 95 - 114.

1670820809467.png

1670820863154.png
1670820900801.png
 
Mzee Saidi unapotea sana mtandaoni siku hizi.
Nashukuru kwa ilmu uliyotoa ingawa kwa muhtasari.

Hakika tunahitaji kuifahamu historia ya Tanganyika iliyokuja kujiunga na Zanzibar kuunda Tanzania
 
Msanii,
Nipo sana hapa nastaajabu wewe kusema nimepotea.
Nakukaribisha katika Group yangu: ''Historia Yetu Miaka 100.''

Kumekuwa na shinikizo kubwa sana kwangu kutoka kwa ndugu na jamaa kuwa nijibu maneno ya Yericko Nyerere kuhusu historia ya African Association (AA).

Wengi waliomsikiliza Yericko katika kipindi cha TV ya Star Times hawakupendezewa na jinsi Yericko Nyerere alivyoeleza historia hiyo na kuiita AA chama cha ‘’walevi.’’

Yericko anawataja viongozi wa AA President Cecil Matola yeye anamwita ‘’Cecilia’’ ambalo ni jina la kike.

Anaendelea kusema kuwa Secretary Kleist Sykes ametolewa Uzulu wakati wa Vita Vya Kwanza na Vya Pili Vya Dunia.

Kleist Sykes kazaliwa Pangani mwaka wa 1894 na ni mtoto Sykes Mbuwane na mama yake jina lake Kwemah kabila yake Mnyaturu.

Sykes Mbuwane ametoka Imhambane, Mozambique.

Waasisi wa AA ni Cecil Matola, Kleist Sykes, Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamis, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Rawson Watts na Raikes Kusi.

Yericko kazungumza mambo asiyoyajua anachanganya miaka na taarifa kwa hakika ni vichekesho vitupu.

Jengo la African Association limejengwa na wanachama wenyewe kwa kujitolea kuanzia mwaka wa 1929 hadi 1933.

Jengo ambalo lilijengwa New Street kona na Kariakoo lilifunguliwa na Gavana Donald Cameron ambae Yericko anamwita Edward Cameron.

Jengo lililojengwa Stanley Street ni jengo la Al Jamiatul Ismaiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) chama kilichoanzishwa na wanachama Waislam waliokuwa pia ni wanachama wa AA.

Hayo mengine sioni sababu ya kuyasemea.

Historia yote ya AA iliandikwa na Kleist Sykes kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Mswada huu ulikuja kuchapwa mwaka wa 1973 kama sura katika kitabu alichohariri John Iliffe, "Modern Tanzanians," Daisy Sykes Buruku, "The Townsman: Kleist Sykes UK. 95 - 114.
Kwa mujibu wa Yerico, chama cha AA kilikuw akikundi cha wanywa gongo tu
 
Dogo kaja mjini miaka ya 2000 historia ya AA ataijulia wapi.

Hata kumjibu ni kumpa ujiko.
Mzee Mohamed Said ameiishi historia ya uhuru wa Tanganyika.
Histiria sio lazima uwe ulikuwepo wakati wa matukio. Haya unayapata kupitia masimulizi na kujisomea
 
Hahahahahahahahaha Yericko hana tofauti na hawa vijana wanaojiita wachambuzi wa mpira
Mtoto wa miaka ya 90 anakusimulia tukio lililotokea miaka ya 80 huko tena wewe Ulilishuhudia
Ila yy akisimulia sukari nyingi mnooo, mbwembwe na uongo mwingi aonekane anajua
 
Back
Top Bottom