Yeriko Nyerere: CIA waliamini Mtu aliyepaswa kukabidhiwa Nchi ya Tanganyika baada ya Wakoloni Waingereza kuondoka ni Mangi Thomas Mariale!

Hupaswi kumuamini muongo/lijongo hata akisema ukweli-Fareed Kubanda.
 
HILO NI LIJINGA
 

..Mangi Marealle ni mmoja kati ya Watanganyika waliokwenda UN kudai Uhuru wa Tanganyika.

..Ushahidi wa maelezo ya Mangi Marealle akiwa UN upo hapa Jamii Forum, hakuna mahali alisema uhuru ucheleweshwe.

..Tanu ilisaidiwa na vyama vya kikabila pamoja na Machifu wakati wa kudai Uhuru ndio maana hakukuwa na masuala ya ukabila hata baada ya kupatikana uhuru wa Tanganyika.
 
Halona Ubishi hili.
 
Wakati wa harakati za Uhuru kuanzia 1954 Nyerere alikuwa ameanzisha TANU na katika harakati zake za mwanzo alikumbana na kizingiti cha mkono wa dola ambapo katika baadhi ya sehemu hakuwa anapewa ushirikiano na Machifu ambao walikuwa upande wa Serikali ya Kikoloni. Mwaka 1956 aliteuliwa kuingia katika LEGCO lakini alijiuzuru mwaka mmoja baadae kutokana na kutotambuliwa kwa mchango wake wowote.

Baada ya Mkutano wa Tabora na Uchaguzi wa 1958 wa kura tatu na TANU kuibuka na ushindi mkubwa dhidi ya UTP na TANC basi ilionekana kuwa Machifu wasingeweza kuikwepa TANU. Hata hivyo walikuwa wamechelewa. Na katika kikao chao cha Februali 1959 Saidi Maswenya wa TANU kutoka Maswa na kwa niaba ya Chama Aliwaambia Machifu kuwa ni vyema wakadandia gari wakati muda ukiwa upande wao, vinginevyo wangeachwa. Katika kikao chao kingine mwaka huo Machifu waliamua kutumia ushawishi wao kubagain na TANU iwapo wanaiunga mkono ni maslahi gani wangelipata.

Mwalimu Nyerere aliamua kukata mizizi wa fitna kwa kuitisha kamati yao ya watu 12 ambapo kulikuwa na Chifu Amri Dodo wa Babati, John Maruma wa Rondo, Petro Marealle wa Vunjo, Abdiel Shangali wa Hai, Abdala Fundikira wa Unyanyembe, Haruna Lugusha wa Itetemia, Patrick Kunambi wa Morogoro, Michael Lukumbuzya wa Ukerewe, Kimweri Magogo wa Usambara, Mwami Theresa Ntare wa Kasulu, Adam Sapi wa Kalenga na Humbi Ziota wa Nzega...na akawaambia kuwa katika Utawala mpya hawakuwa na nafasi labda waiunge mkono TANU na pia wagombee ili kuendelea kuwepo katika Halmashauri. Na kuwa hadi kufikia Julai 1962 ingelibidi wawe wamekabidhi ofisi.

Na kweli ilipofika Julai 1962 hawakupata tena mishahara na kazi zao zikafungwa rasmi. Baadhi yao waliendelea kupewa heshima na jamii zao lakini wengi wao walibaki maskini.

Hata hivyo kuna baadhi ya Machifu waliopatana na Mwalimu kama Adam Sapi ambaye aliteuliwa kuwa Mbunge na Spika, Chifu Haruna Lugusha aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Agricultural Society na Michael Lukumbuzya aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanganyika huko India. (Soma. Aspects of Colonial Tanzania cha Prof. Lawrence Mbogoni)
 
Tatizo ni credibility ya mwandishi.
 

..Muandishi Mohamed Said anasema Machief walianza kushawishiwa kuhusu Uhuru wakati mipango ya kuanzisha Tanu inafanyika.

..Pia safari ya Mwalimu Nyerere, na Mangi Marealle kwenda UN nadhani ilikuwa mwaka 1955, kwa hiyo inaelekea baadhi ya Machifu hawakuchelewa kuunga mkono harakati za uhuru.
 

Kuna watu bafo wanamwamini Yericko?

Huyu jamaa hata hivyo vitabu kumbe kawaibia watu na kujifanya kaviandika yeye. Kuna Wakili moja wa Kihaya aliyoa hiyo siri kwa vile na yeye ni muathitika.Alitaka kumfungulia kesi Yerick aksomba msamaha. Mazungumzo ya huyo Wakili yaliyatoa kwenye sauti ts Watanzania early this month.
 
🤣 🤣 🤣
 
Yericko mweupe na hivyo vijalida vyake kama vya shigongo. Yeye anaviita vitabu
 
Mkoloni mwingereza na beberu mkuu marekani walitaka kukabidhi nchi yetu kwa machifu. Ujue machifu ni kama wafalme maana uongozi ni kurithishana kiokoo. Nchi isingekua na demokrasia ya kweli ila vibaraka wanaotumikia maslahi ya mabeberu kwa moyo wao wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…