Code:
ukihoji kwa nini Esau hayupo kwenye baraka za Israel basi itakubidi pia uhoji kwa nini Ishmael asiwe na baraka ya Isaka.
Ishmael tayari alishabarikiwa na Mungu kwa namana tofauti na Isaka,Lakini Esau ni katika baraka za Isaka.
Code:
Lakini Isaka akasema, “Ndugu yako alikuja kwa hila, naye amechukua baraka yako.”
Hapa tukubaliane kwamba Esau alifanyiwa faulo mbaya ndani ya 18 na refa akapeta!.
Code:
Utaishi kwa upanga wako, na utamtumikia ndugu yako; lakini utakapoasi utaivunja kongwa yake shingoni mwako.”
Nini maana ya "utakapoasi utaivunja kongwa yake shingoni mwako.”?
Mkuu!Mjadala wetu hasa unahusiana na kuliangalia eneo la Canaan linalogombewa na wana wa Israel na hao wengine wanaoitwa waparestina.
Code:
Ikiwa,Esau na kizazi chake siyo wana wa Israel na siyo waisrael.Je,Esau na kizazi chake wanaitwaje?,nchi yao ni ipi?Race yao ni ipi hapo mashariki ya kati?
Katika maswali hayo umejibu hivi "Baadhi wanasema ni mataifa ya kiarabu na ulaya. Ukifatilia historia yao utaelewa zaidi.".
Sasa mkuu tukitumia maandiko inaoneka Esau alioa pia katika kizazi za Ishmael:
Mwanzo 28
5 Basi Isaka akampeleka Yakobo, naye akaenda Padan-aramu, kwa Labani, mwana wa Bethueli, Mshami, ndugu wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau.
6 Esau akaona ya kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padan-aramu, ili ajitwalie mke huko, na katika kumbariki akamwagiza, akasema, Usitwae mke wa binti za Kanaani,
7 na ya kuwa Yakobo amewatii babaye na mamaye, akaenda Padan-aramu.
8 Esau akaona ya kuwa binti za Kanaani hawakumpendeza Isaka, baba yake.
9 Basi Esau akaenda kwa Ishmaeli akamtwaa Mahalathi, binti Ishmaeli mwana wa Ibrahimu, ndugu wa Nebayothi, kuwa mkewe pamoja na wakeze aliokuwa nao.
Hapa sasa ndiyo connection ya kiarabu inatokea.[emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu!Yakobo(Israel) aliondoka katika nchi aliyozaliwa na kwenda kukaa katika nchi ya Harani (Uturuki)ya leo kwa kumkimbia kaka yake Esau.Miaka 7 na miaka 7 mingine alimtumikia mjomba wake Labani kwa ujira wa kupewa wake,na aliendelea kukaa huko mpaka alipokamilisha kuzaa kizazi chake chote cha wana 12(wanaisrael).Kifupi Israel alikaa Uturuki kwa zaidi ya miaka 20 kabla ya kurudi aliko zaliwa.Na kwa kipindi chote hicho kaka yake Esau,aliekuwa akiendeleza kizazi katika nchi waliyozaliwa.
Mwanzo 31:13,17-18
13 Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.
17 Ndipo Yakobo akaondoka, akapandisha wanawe na wakeze juu ya ngamia.
18 Akachukua wanyama wake wote, na mali yake yote aliyokuwa ameyapata, na wanyama aliowapata katika Padan-aramu, ili afike kwa Isaka babaye katika nchi ya Kanaani.
Baada ya miaka ishirini ndiyo Israel anarudi katika nchi aliyozaliwa na kwa kaka yake Esau:
Mwanzo 32
3 Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu.
4 Akawaagiza akisema, Mwambieni hivi bwana wangu, Esau, Hivi ndivyo asemavyo mtumwa wako, Yakobo; Nimekaa ugenini kwa Labani, na kukawia huko hata sasa,
Swali,kizazi cha Esau ambaye alioa pia kwa waishmael kipo wapi hii leo ikiwa watu wanadai kuwa hilo eneo la Canaan nila Israel(Yakobo) peke yake?.
Tuendelee ,
Kwa mujibu wa maandiko,Esau alihamia katika milima ya Seiri (Syria)ya sasa.
Mwanzo 36
6 Esau akawatwaa wakeze, na wanawe, na binti zake, na watu wote wa nyumbani mwake, na ng'ombe zake, na wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyoyapata katika nchi ya Kanaani; akaenda mpaka nchi iliyo mbali na Yakobo nduguye.
7 Maana mali yao yalikuwa mengi wasiweze kukaa pamoja, wala haikuweza nchi ya kusafiri kwao kuwachukua, kwa sababu ya wanyama wao.
8 Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu.
Esau akiwa katika makazi mapya,alijenga na kuendesha ufalme huko.
Mwanzo 36
31 Na hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla ya kumiliki mfalme ye yote juu ya wana wa Israeli.
32 Bela wa Beori alimiliki katika Edomu, na jina la mji wake ni Dinhaba.
33 Akafa Bela, akamiliki Yobabu mwana wa Zera, wa Bosra, badala yake.
34 Akafa Yobabu, akamiliki Hushamu, wa nchi ya Watemani, badala yake.
35 Akafa Hushamu, akamiliki Hadadi wa Bedadi badala yake, naye ndiye aliyepiga Midiani katika nyika ya Moabu, na jina la mji wake ni Avithi.
36 Akafa Hadadi, akamiliki Samla wa Masreka badala yake.
37 Akafa Samla, na Shauli wa Rehobothi, ulio karibu na mto, akamiliki badala yake.
38 Akafa Shauli, akamiliki Baal-hanani, mwana wa Akbori, badala yake.
39 Akafa Baal-hanani, mwana wa Akbori, akamiliki Hadadi badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu.
40 Na hayo ndiyo majina ya majumbe waliotoka kwa Esau, kufuata jamaa zao, na mahali pao, kwa majina yao. Jumbe Timna, jumbe Alva, jumbe Yethethi,
41 jumbe Oholibama, jumbe Ela, jumbe Pinoni,
42 jumbe Kenazi, jumbe Temani, jumbe Mibsari,
43 jumbe Magdieli, jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu, kufuata makao yao, katika nchi ya mamlaka yao. Naye huyo ndiye Esau, baba ya Edomu.
Lakini baadaye wana wa Israel waliingia kwa Edomu na waliimiliki tawala ya Esau pamoja na kwamba Esau aliwahama kwa wema.
Ilikuwaje kizazi cha Israel kuimilimi nchi ya Esau?.
Kwanza kabisa ugomvi kati ya Esau na Yakobo,sikwamba ulianzia pale Yakobo alipozipora baraka za Esau kwa hila ya mama yao.Bali uadui kati yao ulianzia tangu tumboni.
Mwanzo 25,
21 Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.
22 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana.
23 Bwana akamwambia,Mataifa mawili yamo tumboni mwako,Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako.Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili,Na mkubwa atamtumikia mdogo.
Angalia hapo mstari 23 jinsi ulivyosema.Kifupi Esau alitengwa na muamuzi wa kati kwa kuamua kumeza filimbi kwa faulo zote alizochezewa Esau na Yakobo.
Kukua kwa ugomvi kati ya Esau na Yakobo,
Hesabu 20,
14 Kisha Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi wamwendee mfalme wa Edomu, na kusema, Ndugu yako Israeli asema, Wewe wazijua taabu zote zilizotupata;
15 jinsi baba zetu walivyotelemkia Misri, nasi tulikaa Misri muda mwingi, nao Wamisri walitutenda vibaya sana, na baba zetu pia;
16 tena tulipomlilia Bwana, akatusikiza sauti yetu, akamtuma malaika, na kututoa tutoke Misri; nasi tupo hapa Kadeshi, mji wa mpakani mwako mwa mwisho;
17 tafadhali utupe ruhusa tupite katika nchi yako; hatutapita katika mashamba, wala katika mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visimani; tutaifuata njia kuu ya mfalme, tusigeuke kwenda upande wa kuume, wala upande wa kushoto, hata tutakapopita mpaka wako.
18 Edomu akamwambia, Hutapita katika nchi yangu, nisije nikakutokea kupigana nawe kwa upanga.
19 Wana wa Israeli wakamwambia, Tutakwea kwa njia kuu; tena kama tukinywa maji yako, mimi na wanyama wangu wa mifugo, ndipo nitakulipa thamani yake; nipe ruhusa nipite kwa miguu yangu wala sitaki neno lingine lo lote.
20 Akamwambia, Hutapita katika nchi yangu. Kisha Edomu akamtokea ili kupigana naye, na watu wengi, na kwa mkono wa nguvu.
21 Basi hivyo Edomu akakataa kumpa Israeli ruhusa kupita katika mipaka yake; kwa hivyo Israeli akageuka na kumwacha.
Baada ya matukio hayo,Israel aliamuriwa kupigana na Esau(Edomu).
Obadia 1
1Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu; Tumepata habari kwa Bwana, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema,Haya,inukeni ninyi;Na tuinuke tupigane naye.
2 Tazama, nimekufanya mdogo kati ya mataifa; Umedharauliwa sana.
3 Kiburi cha moyo wako kimekudanganya, Wewe ukaaye katika pango za majabali, Mwenye makao yako juu sana; Asemaye moyoni, Ni nani atakayenishusha mimi?
4 Ujapopanda juu kama tai, Ijapokuwa kioto chako kimewekwa kati ya nyota, Nitakushusha kutoka huko; asema Bwana.
5 Kama wevi wangekujilia, kama wanyang'anyi wangekujilia usiku, (jinsi ulivyokatiliwa mbali!) Je! Wasingeiba kiasi cha kuwatosha? Kama wachumao zabibu wangekujilia, je! Wasingeacha baadhi ya zabibu, ziokotwe?
6 Jinsi watu wa Esau wanavyotafutwa-tafutwa! Jinsi hazina zake zilizofichwa zinavyoulizwa-ulizwa!
7 Watu wote wa mapatano yako Wamekufukuza, hata mipakani; Wale waliofanya amani nawe Wamekudanganya, na kukushinda; Walao mkate wako wameweka mtego chini yako; Wala hana ufahamu wa hayo ndani yake.
8 Siku hiyo, je! Sitawaangamiza watu wenye akili katika Edomu, na wenye ufahamu katika kilima cha Esau? Asema Bwana.
9 Na mashujaa wako, Ee Temani, watafadhaika, hata iwe kila mtu akatiliwe mbali kwa kuuawa katika kilima cha Esau.
10 Kwa sababu ya udhalimu aliotendwa ndugu yako Yakobo, aibu itakufunika, nawe utakatiliwa mbali hata milele.
11 Siku ile uliposimama upande, siku ile wageni walipochukua mali zake, na watu wa kabila nyingine walipoingia katika malango yake, na kumpa kura juu ya Yerusalemu, wewe nawe ulikuwa kama mmoja wao.
12 Lakini usiitazame siku ya ndugu yako, siku ya mashaka yake, wala usisimange juu ya wana wa Yuda siku ya kuangamizwa kwao; wala usinene maneno ya kiburi katika siku ya shida yao.
13 Usiingie katika lango la watu wangu, siku ya msiba wao; naam, usiyatazame mateso yao, siku ya msiba wao; wala usitie mikono yako juu ya mali zao, siku ya msiba wao.
14 Wala usisimame penye njia panda, ili kuwakatilia mbali watu wake wakimbiao; wala usiwatoe watu wake waliosalia, katika siku ya dhiki.
15 Kwa maana hiyo siku ya Bwana i karibu juu ya mataifa yote; kama ulivyotenda, ndivyo utakavyotendwa; malipo yako yatakurudia juu ya kichwa chako mwenyewe.
16 Kwa maana kama vile mlivyokunywa juu ya mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote watakavyokunywa daima; naam, watakunywa na kubabaika, nao watakuwa kana kwamba hawakuwa kamwe.
17 Bali katika mlima Sayuni watakuwako wenye kuokoka, nao utakuwa mtakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki milki zao.
18 Na nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu itakuwa mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaka kati yao, na kuwateketeza; wala hatasalia mtu awaye yote katika nyumba ya Esau; kwa kuwa Bwana amesema hayo.
19 Na watu wa Negebu wataumiliki mlima wa Esau; na watu wa Shefela watawamiliki Wafilisti; nao watalimiliki konde la Efraimu, na konde la Samaria, na Benyamini atamiliki Gileadi.
20 Na watu wa jeshi hili la wana wa Israeli waliotekwa, walio kati ya Wakanaani, watamiliki mpaka Sarepta; na hao watu wa Yerusalemu waliotekwa, waliomo Sefaradi, wataimiliki miji ya Negebu.
21 Tena waokozi watakwea juu ya mlima Sayuni ili kuuhukumu mlima wa Esau; na huo ufalme utakuwa ni mali ya Bwana.
Angalia,pamoja na Mungu kuahidi kumsambalatisha Esau (Edomu),lakini kutimia kwa hilo ni labda mpaka mwisho wa dunia kwa maana Edomu ataendelea kupajenga tena na tena hata milelele.
Malaki 1
Ufunuo wa neno la Bwana kwa Israeli kwa mkono wa Malaki
2 Nimewapenda ninyi, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Umetupendaje? Je! Esau siye ndugu yake Yakobo? Asema Bwana; ila nimempenda Yakobo;
3 bali Esau nimemchukia na kuifanya milima yake kuwa ukiwa, na urithi wake nimewapa mbweha wa nyikani.
4 Ijapokuwa Edomu asema, Tumepondwa-pondwa, lakini tutarudi na kupajenga mahali palipoachwa hali ya ukiwa; Bwana wa majeshi asema hivi, Wao watajenga, bali mimi nitaangusha; na watu watawaita, Mpaka wa uovu, na, Watu ambao Bwana anawaghadhabikia milele.
Mpaka hapa,tunamuona adui wa Israel (Yakobo) ni Esau(Edomu).Kifupi hapo mashariki ya kati,wanaopigana ni MAPACHA Esau na Edomu.
Naomba nisimame hapa tena kwa sasa.