Yes!! English never loved us, not to this extent

Nisaidie tafsiri yake mkuu!
Alipost yeye,lakini alikuwa anamaanisha wanasubiri kuku apikwe....sasa kuku akichinjwa haitwi hen tena,na jamaa alishindwa kupangilia vizuri sentensi yake. Ingia jukwaa la jokes kuna uzi wa vituko mtandaoni
 
Alipost yeye,lakini alikuwa anamaanisha wanasubiri kuku apikwe....sasa kuku akichinjwa haitwi hen tena,na jamaa alishindwa kupangilia vizuri sentensi yake. Ingia jukwaa la jokes kuna uzi wa vituko mtandaoni
Kwa hiyo unataka nikacheke tena😄
 
Hizo kazi anapewa msanii aandike hilo bango, bahati mbaya huenda alikosea ila ndo ivo labda na huyo mkandarasi hakua na time ya kuliangalia tena.

Wachoraji ambao ndo hasa hupewa hizo tenda za kuandika mara nyingi tu huwa wanakosea kuandika.
 
Mtu kama akiamua kutumia lugha yoyote hata kama siyo kiingereza ni vyema kuwa makini na ufasaha wa kutumia hiyo lugha,hapo unaona kilichofanyika kwenye hilo bango ni uzembe,hata kama wangeamua kutumia kamusi za kwenye simu wangeweza kuandika kwa usahihi,kinacholaimiwa hapo ni kukosa ubunifu wa kupeleleza mambo.
 
Grammer imemgonga na degree yake. Wakati wa sherehe jamaa aliombwa aanzishe sala kwa lugha ya malkia, ni kicheko. Lord, come, look at our food before eating. Asante Yesu, Amen.
 
Upo sahihi mkuu. Kiuhalisia haikutakiwa kuandikwa vile
 
Kujua kiingereza kunakuwezesha kuelewa mambo mengi kwa upana, kwasababu mambo mengi yanaelezewa kwa kiingereza(iwe ni ya kitaaluma, kibiashara nk)

Sio kwamba kitakulipa, hapana.
Unamaanisha kuzungumza kiingereza au kujua kiingereza!

Ni kweli watanzania wengi hatujui kuzungumza kiingereza kwa ufasaha ila kiingereza kinaeleweka kwa wengi.

Suala la kuchangamkuia fursa kunasababu nyingi zaidi ya hiyo unayoisemea ya lugha ikiwa ni pamoja kushikana mkono au konekisheni! Ujasiri ukitazama watanzania wengi hatupeani konekishenj haijalishi ni ndani au nje ya nchi.

Angalia mifumo yetu ilivyo leo hii wangapi wanapaspot za kusafria ? Fatilia uone mzunguko wake na sababu kibao ...

Lugha ni tatizo lakni sidhani kama mtu akipata fursa na unaujuzi wako utashindwa kujifunza lugha ya mawasiliano ya kila siku.
 
Hayo makosa ya maandishi na maana ndio kazi yenyewe?

Kujua kiingereza vizuri sio ufanisi wa kazi mkuu.

Leo wachina wanajenga barabara wengi wao kiingereza ni shida au wengine hawajui kabisa! Mbona wanafanya kazi na zinaonekana.

Watanzania tunapenda sana kukosoa lakni utendaji kazi ni wazembe sana ndicho kinapelekea kutoaminika! Tunaunafiki sana tukipewa kazi sababu zinakuwa nyingi sana
 
waafrica ni washmba sana, yani tunahisi kuzungumza kiengereza ndio ujanja. acha tuendelee kuwa mafukara tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…