Yes!! English never loved us, not to this extent

Yes!! English never loved us, not to this extent

Nisaidie tafsiri yake mkuu!
Alipost yeye,lakini alikuwa anamaanisha wanasubiri kuku apikwe....sasa kuku akichinjwa haitwi hen tena,na jamaa alishindwa kupangilia vizuri sentensi yake. Ingia jukwaa la jokes kuna uzi wa vituko mtandaoni
 
Alipost yeye,lakini alikuwa anamaanisha wanasubiri kuku apikwe....sasa kuku akichinjwa haitwi hen tena,na jamaa alishindwa kupangilia vizuri sentensi yake. Ingia jukwaa la jokes kuna uzi wa vituko mtandaoni
Kwa hiyo unataka nikacheke tena😄
 
Hizo kazi anapewa msanii aandike hilo bango, bahati mbaya huenda alikosea ila ndo ivo labda na huyo mkandarasi hakua na time ya kuliangalia tena.

Wachoraji ambao ndo hasa hupewa hizo tenda za kuandika mara nyingi tu huwa wanakosea kuandika.
 
Mnahangaika sana
Hichi kiingereza kitaleta chakula mezani
Kitawajengea nyumba
Mbona hao wakenya wenyewe mnaosema wanajua kila siku ni njaa kwao kingewafanya wawe wa dunia ya kwanza. Lkn ndio wenyemaisha magumu wengi.

Huko marekani wanaoongea kiingereza bado kuna watu wanaishi kama wapo jehanam
Mtu kama akiamua kutumia lugha yoyote hata kama siyo kiingereza ni vyema kuwa makini na ufasaha wa kutumia hiyo lugha,hapo unaona kilichofanyika kwenye hilo bango ni uzembe,hata kama wangeamua kutumia kamusi za kwenye simu wangeweza kuandika kwa usahihi,kinacholaimiwa hapo ni kukosa ubunifu wa kupeleleza mambo.
 
Grammer imemgonga na degree yake. Wakati wa sherehe jamaa aliombwa aanzishe sala kwa lugha ya malkia, ni kicheko. Lord, come, look at our food before eating. Asante Yesu, Amen.
 
Okay imeelezea kasayansi kidogo ,, mimi siyo mwalimu wa kiingereza lakini ntajaribu kukuelekeza kwa kadri navyoelewa hii lugha

Katika lugha ya kiingereza kuna

Direct speech
Hapa mtendaji mkuu ( subject au actor) anakuwa mwanzo afu mtendewa (object au receiver) anakuwa mwishinoni ..

Mfano ,,, john kicks a ball

John ni mtendaji (subject au actor)
A ball ni mtendewa (receiver au object)

Popote ukiona sentensi ipo hivi basi ni direct speech ..

Indirect speech ..
Hapa mtendewa ( receiver au object anakuwa mwanzo na mtendaji( actor au object )
Mfano
The ball is kicked by john

The ball ni mtendewa (object au receiver )

John ni mtendaji ( subject au actor)

Sasa katika hii lugha ya kiingereza
Mfumo huu wa pili (indirect speech ) mara nyingi hutumika pindi unapokuwa hutaki kutaja jina la mtendaji au pindi unapokuwa humjui mtendaji aliyefanya jambo au tukio..

Mfano unaweza kuandika
The ball is kicked
Hapo nimeamua kutomtaja mpigaji au simjui aliyepiga mpira .. japo mto anaweza kukuuliza by who ??

Sasa tuje kwenye mada yetu

H.i.v is killed
Hii ni inderect sentence
Ikiwa na maana H.i.v imeuwawa au imetokomezwa ,,, kweli sentensi hii ipo sahihi lakin haina maana kwanini kwasababu
H.i.v bado ipo , na ni ugonjwa hatari hivyo ni wazi aliendika hapa hakuelewa alichokiandika..

Sijui kama nipo sahihi wengine wanaweza kuja kujazia pale nilipokosea
Upo sahihi mkuu. Kiuhalisia haikutakiwa kuandikwa vile
 
Kujua kiingereza kunakuwezesha kuelewa mambo mengi kwa upana, kwasababu mambo mengi yanaelezewa kwa kiingereza(iwe ni ya kitaaluma, kibiashara nk)

Sio kwamba kitakulipa, hapana.
Unamaanisha kuzungumza kiingereza au kujua kiingereza!

Ni kweli watanzania wengi hatujui kuzungumza kiingereza kwa ufasaha ila kiingereza kinaeleweka kwa wengi.

Suala la kuchangamkuia fursa kunasababu nyingi zaidi ya hiyo unayoisemea ya lugha ikiwa ni pamoja kushikana mkono au konekisheni! Ujasiri ukitazama watanzania wengi hatupeani konekishenj haijalishi ni ndani au nje ya nchi.

Angalia mifumo yetu ilivyo leo hii wangapi wanapaspot za kusafria ? Fatilia uone mzunguko wake na sababu kibao ...

Lugha ni tatizo lakni sidhani kama mtu akipata fursa na unaujuzi wako utashindwa kujifunza lugha ya mawasiliano ya kila siku.
 
Mtu kama akiamua kutumia lugha yoyote hata kama siyo kiingereza ni vyema kuwa makini na ufasaha wa kutumia hiyo lugha,hapo unaona kilichofanyika kwenye hilo bango ni uzembe,hata kama wangeamua kutumia kamusi za kwenye simu wangeweza kuandika kwa usahihi,kinacholaimiwa hapo ni kukosa ubunifu wa kupeleleza mambo.
Hayo makosa ya maandishi na maana ndio kazi yenyewe?

Kujua kiingereza vizuri sio ufanisi wa kazi mkuu.

Leo wachina wanajenga barabara wengi wao kiingereza ni shida au wengine hawajui kabisa! Mbona wanafanya kazi na zinaonekana.

Watanzania tunapenda sana kukosoa lakni utendaji kazi ni wazembe sana ndicho kinapelekea kutoaminika! Tunaunafiki sana tukipewa kazi sababu zinakuwa nyingi sana
 
waafrica ni washmba sana, yani tunahisi kuzungumza kiengereza ndio ujanja. acha tuendelee kuwa mafukara tu
 
Back
Top Bottom