YES Tunahitaji Apartments Tanzania Lakini si kila Mkoa


Hivi kweli unaamini Europe ilii-underdevelop Africa? Mimi naona hicho kitabu cha bwana Rodney kimekaa kipropaganda zaidi kuliko kiuhalisia.

Africa ilikuwa underdeveloped hata kabla Europeans hawajaja.




Lakini mnachojadili hapa kiko tofauti na alichokisema mdau.

Yeye amesema Ulaya imeendelea kutokana na Afrika na sio kwamba Afrika haijaendelea kutokana na Ulaya.

Yaani mleta mada anaamini kuwa Afrika ndio iliyosababisha Ulaya iwe na maendeleo. Kwahiyo kama ni kitabu kingepaswa kuwa "How Africa Developed Europe"...
 
Last edited by a moderator:

Hii sheria inayomkataza mtu binafsi kuuza jengo lake kwa mtu binafsi mwingine iko kinyume na katiba ya nchi. Halafu huyo mmiliki akifa jengo hilo litaweza kurithiwa? Kama linaweza kurithiwa kwanini likatazwe kuuzwa?
 

Hata hiyo napinga! Ulaya imeendelea yenyewe kwa juhudi za watu wake. Hata mpaka kilichowafanya wazungu waanze kutembelea sehemu zingine za dunia ni maendeleo. Bila maendeleo wasingeweza kwenda sehemu zote hizo walizoenda kwa wakati ule.

Watu tokea 1215 wameandika Magna Carta unadhani mchezo....hayo ni maendeleo bana.
 
Kwani wewe kwako hilo neno linamaanisha nini?

Nadhani kabla ya hizo contacts, Afrika walikuwa na structures zao za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Nadhani Afrika ilikuwa na systems zake za kibiashara which were there for quite a long time kabla ya kuwa replaced na triangular trade.

Kama Europe imechangia basi mchango wake ni mdogo sana. Na kwanza sielewi hata imechangiaje wakati kulikuwa hakuna lolote la maana kabla wazungu hawajaja.

Kutokuwa na lolote kama nini kwa mfano?

Hicho kitabu kimeandikwa kutoka kwenye mtazamo wa Afrocentric, kwa maoni yangu.

Na mie kwa maoni tyangu, kulinganisha na vitabu vingine nilivyovisoma, at least hicho kitabu kimejaribu kuandika from historic point of view.


Again it all depend na maana yako ya maendeleo.
 
Hii sheria inayomkataza mtu binafsi kuuza jengo lake kwa mtu binafsi mwingine iko kinyume na katiba ya nchi. Halafu huyo mmiliki akifa jengo hilo litaweza kurithiwa? Kama linaweza kurithiwa kwanini likatazwe kuuzwa?

Inawezekanaje kuwa kinyume na katiba wakati katiba hiyo hiyo inaanza kwa kusema "Bila kuathiri sheria nyingine za nchi" blaa blaaa?

Hivyo basi, kama kuna sheria inayomkataza mtu binafsi kuuza jengo lake kwa mtu binafsi mwingine haiko kinyume kabisa na katiba kwa sababu katiba hiyo hiyo inasema wazi kuwa iko subject to other laws of the country.

Kuhusu jengo kurithiwa, you don't get more rights than the ones previously enjoyed by the deceased.
 
Nadhani kabla ya hizo contacts, Afrika walikuwa na structures zao za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Nadhani Afrika ilikuwa na systems zake za kibiashara which were there for quite a long time kabla ya kuwa replaced na triangular trade.

Kuna written records zozote ku-support hiyo supposition yako?

Kutokuwa na lolote kama nini kwa mfano?

Niliandika kutoka na lolote la 'maana'. Mfano higher learning institutions kama University of Bologna huko Italia au University of Salamanca huko Hispania - vyuo ambavyo mpaka leo vipo.

Jingine ni codified systems za utawala, sheria, dini, na kadhalika. Kama zilikuwepo Afrika kabla ya 1500 - 1600, kuna maandishi yoyote yanayoonyesha ushahidi wa existence yake?

Na mie kwa maoni tyangu, kulinganisha na vitabu vingine nilivyovisoma, at least hicho kitabu kimejaribu kuandika from historic point of view.

Okay, since ni maoni yako siwezi kubisha sana. Mimi naona kimeandikwa ki-Pan-Africanist zaidi.

Again it all depend na maana yako ya maendeleo.

Maendeleo tunayoyaongelea ni ule ubora na ukuaji wa jamii kutoka hatua ya chini/duni na kwenda kwenye hatua ya juu/na bora zaidi. Au wewe maana ya maendeleo kwako ni ipi?
 

Ndio maana nimemwambia dogo asilete hoja zinazoweza kuanzisha mjadala mwingine nmrefu...
 
Ndio maana nimemwambia dogo asilete hoja zinazoweza kuanzisha mjadala mwingine nmrefu...

Unajua hizo hoja za hao Pan Africanists zinapotosha sana wakati mwingine. Kwa mfano, wakati nasoma tulifundishwa kuwa eti Ghana ndo nchi ya kwanza kupata uhuru barani Afrika kumbe siyo kweli bana.

Ila watu wameaminishwa hivyo na kwa vile enzi hizo hata resources za kufanyia research tulikuwa hatuna basi kila uongo tunaolishwa tunaumeza tu mazima mazima bila hata uchunguzi.
 
EMT maelezo yako kuhusu Africa na underdevelopment yanakosa nguvu kwa sababu Afrika (kwa maana AFrika ya watu weusi) YOTE haijaendelea. North to South, East to West.

Hizo factors ziliweza vipi kuact effectvely kwa nchi zote across the continent?

Nchi za Ulaya zipo zilizoendelea na zile ambazo hazijaendelea zinajikongoja. Tena more interestingly wakati mwingine nchi iliyoendelea sana inapakana na nchi inayojikongoja!

Nchi za Afrika in general ni kubwa kuliko za Ulaya. Lakini nchi za Afrika originally ni ndogo zaidi ya nchi za Ulaya. Hizi kubwa ni "artificial" zilizozaliwa baada ya ukoloni. Inawezekana uwepo wa vinchi vidogovidogo (a.k.a makabila) kumechangia kiasi kikubwa vinchi hivi kuweza kuwa defeated na external invaders na hatimaye utamaduni na historia yake kuharibiwa kabisa. Lakini tukirudi nyuma tunaona kwamba viongozi wa mataifa (makabila) ya kiafrika walipaswa kujua kuwa kuna umuhimu wa kuwa na kingdoms/tawala kubwa zenye nguvu. Hawakufanikiwa kufanya hivyo either kwa kutokujua umuhimu wake au kushindwa kubuni mbinu ya kutekeleza.
Nyani Ngabu anakosea anaposema hakukuwa na mifumo. Mifumo ilikuwepo ila ilikuwa defeated na invaders na kuharibiwa kabisa. Kungekuwa hakuna mifumo, basi tusingeweza kuwa na tamaduni za makabila. Vitu kama ngoma pia vsingekuwepo.

Tukumbushane tu kuwa chuo kikuu maana yake ni sehemu ambayo watu wanakutana kujifunza. Unyago can be chuo kikuu. Kama utamaduni usingeharibiwa basi sehemu za mafunzo zingeendelezwa na kuwa bora zaidi kulingana na mahitaji. Sehemu zetu za mafunzo hazijahitaji majengo yenye kuta ngumu kwa sababu ya hali ya hewa ya tropiki. Wenzetu Ulaya wasingeweza kujifunza kwenye baridi hivyo wakabuni majengo magumu ambayo mpaka sasa yapo.

Pamoja na yote, hakuna sehemu moja ya dunia inayoweza kuinyeshea kidole nyingine kwamba ndio iliyosababisha kuendelea au kutokuendelea kwake.
 
Last edited by a moderator:
Nchi za Ulaya zipo zilizoendelea na zile ambazo hazijaendelea zinajikongoja. Tena more interestingly wakati mwingine nchi iliyoendelea sana inapakana na nchi inayojikongoja!

Hata hizo nchi za Ulaya ambazo zinaonekana kama hazijaendelea, nchi nyingi za Afrika zikifikia tu hata nusu ya maendeleo yake mbona zitajitapa sana. Hao Wakenya tu na Kinairobi chao wana ngebe utadhani sijui nini, sasa wakifikia hata nusu ya maendeleo ya Ureno mbona tutakoma.

anakosea anaposema hakukuwa na mifumo. Mifumo ilikuwepo ila ilikuwa defeated na invaders na kuharibiwa kabisa. Kungekuwa hakuna mifumo, basi tusingeweza kuwa na tamaduni za makabila. Vitu kama ngoma pia vsingekuwepo.

Kama ilikuwepo basi ilikuwa ipo ipo tu na ndiyo maana mpaka leo hatujitambui wala kujielewa. Uzungu tunautaka...Uafrika tunautaka....hatueleweki. Hata imani za kidini za asili ni kama hazipo tena. Watu wengi kama siyo Wakristo ni Waislamu.


Hii hoja ya hali ya hewa ni dhaifu kabisa kupata kutokea. Utadhani huko Ulaya ni baridi tu 24/7 365.
 
Kuna written records zozote ku-support hiyo supposition yako?

Zipo tuu nyingi mbona. Unataka nikaanze kupekua madesa yangu ya sekondari? Hunitakii mema wewe, chafya za vumbi saa hizi na jua lote hili? Halafu leo Friday najiandaa kwa kidate bana.

Niliandika kutoka na lolote la 'maana'. Mfano higher learning institutions kama University of Bologna huko Italia au University of Salamanca huko Hispania - vyuo ambavyo mpaka leo vipo.

Kama ni higher learning institutions basi Afrika ilikuwa na vyuo vikuu pia. Mfano, ni Sankore Madrasah aka the University of Madrasah, chuo kikuu cha Kiislamu kilichoanzishwa Timbuktu. Kilikuwa kinatoa mpaka degree za utafiti amabzo siku hizi tunaziita Ph.D.

Jingine ni codified systems za utawala, sheria, dini, na kadhalika. Kama zilikuwepo Afrika kabla ya 1500 - 1600, kuna maandishi yoyote yanayoonyesha ushahidi wa existence yake?

Mpaka sasa hivi, system ya utawala, sheria, n.k za Uingereza is largely uncodified. Unaweza kusema Uingereza is underdeveloped kwa sababu tuu haija-codify system yake?

Okay, since ni maoni yako siwezi kubisha sana. Mimi naona kimeandikwa ki-Pan-Africanist zaidi.
Let's put this to rest.

Maendeleo tunayoyaongelea ni ule ubora na ukuaji wa jamii kutoka hatua ya chini/duni na kwenda kwenye hatua ya juu/na bora zaidi. Au wewe maana ya maendeleo kwako ni ipi?

Right. Kwa mfano, enzi hizo walikuwa wanaishi on the basis that no individual rights, without duties to the society. Lakini siku hizi, kinacho matter zaidi ni individual rights. Unaweza kusema mabadiliko haya ni ukuaji wa jamii kutoka hatua ya chini ya kubalance rights and duties kwenda hatua ya juu zaidi ya ku-focus zaidi kwenye individual rights without duties?
 


Kwenye vita ukishindwa unapoteza kila kitu including utamaduni. Ndicho kilichotokea.

Hata wakati wa vita vya pili vya dunia, nchi ikivamiwa ilikuwa inabadilishwa mpaka offical language na vyuo vinafungwa. Kuna nchi mpaka sasa kila mwaka zinaadhimisha siku ya kuwachukia wajerumani kwa kuwafanyia unyama wa kudumaza elimu nchini mwao. Leo hii ukienda Uingereza na kufanya kichina kuwa ndio official language na lugha ya kufundishia chuo, automatically unakuwa umeshawaondolea uwezo waingereza wengi. Just one decision like that can destroy a nation.
Swala la hali ya hewa lina mantiki. Angalia hata picha za mavazi. Kama watu walitofautiana kwa mavazi, kwanini wasitofautiane kwenye nyumba? Ulaya miezi isiyokuwa na baridi ni minne tu. Ndio maana hata ukiangalia todays architecture ya Ulaya hawana utamaduni wa kuwa na balcony kubwa kama sisi. Nyumba zao hazina vibaraza kama sisi. Na maghorofa yao yana corridors ambazo ni indoor hata kama corridor hiyo iko pembeni kwa ukuta. Kwahiyo hali ya hewa ina nafasi yake muhimu sana kwenye utamaduni ambayo haipaswi kuwekwa pembeni.
 
Zipo tuu nyingi mbona. Unataka nikaanze kupekua madesa yangu ya sekondari? Hunitakii mema wewe, chafya za vumbi saa hizi na jua lote hili? Halafu leo Friday najiandaa kwa kidate bana.

Kidate na nani? Mwali?🙂


Hahahaaaa madrasa tena? Walikuwa wanatoa shahada katika fani zipi hao? Hicho chuo kipo hadi leo? Na nini cha maana kilichotokea hapo ambacho kilisaidia kuleta maendeleo ya mwanadamu?

Mpaka sasa hivi, system ya utawala, sheria, n.k za Uingereza is largely uncodified. Unaweza kusema Uingereza Uingereza is underdeveloped kwa sababu tuu haija-codify system yake?

Na kuna nchi ngapi hapa duniani ambazo zinafuata hiyo mifumo ya Uingereza?

Right. Kwa mfano, enzi hizo walikuwa wanaishi on the basis that no individual rights, without duties to the society.

What exactly is 'duties to the society'?

Lakini siku hizi, kinacho matter zaidi ni individual rights. Unaweza kusema mabadiliko haya ni ukuaji wa jamii kutoka hatua ya chini ya kubalance rights and duties kwenda hatua ya juu zaidi ya ku-focus zaidi kwenye individual rights without duties.?

Hapo kwenye duties inabidi upambanue zadi. Kwa sababu hata kulipa kodi nako ni duty to society vile vile...au siyo?
 
Last edited by a moderator:

Ninajua kuwa kuna sheria zinazokataza kubadili muonekano wa jengo.

Ila hiyo ya kuwa kuna sheria inayozuwia kuuza sijawahi kuiona

Unaweza kutuwekea kifungu cha sheria?

Manake isije ikawa kuna kosa la interpretation ya maana ya kisheria hapa
 
Swala la hali ya hewa lina mantiki.

Bado sioni mantiki yake kwenye uhusiano wake na maendeleo ya kiuchumi. If anything sisi wenye hali ya hewa nzuri zaidi tungekuwa na maendeleo sana kwa sababu hatuna mavimbunga makubwa wala ma snowstorms ambayo hurudisha nyuma maendeleo. Hivi kitu kama cha hurricane Sandy kingetua Dar hayo majanga yake yasingesemeka!


Hiyo hoja ya hali ya hewa ingekuwa ni kweli basi sisi ndo tungefaidika nayo sana maana kw kweli ukilinganisha na Ulaya, Afrika imekuwa favored sana. Hivyo mimi naikataa kata kata kuwa inahusiana na maendeleo ya Ulaya.
 

Hapa unaongelea nchi ipi?

Misri, Libya, Sudan, Afrika Kusini au all the way to Liberia?
 
EMT maelezo yako kuhusu Africa na underdevelopment yanakosa nguvu kwa sababu Afrika (kwa maana AFrika ya watu weusi) YOTE haijaendelea. North to South, East to West. Hizo factors ziliweza vipi kuact effectvely kwa nchi zote across the continent?

Kama nilivyosema mwanzo kuwa why Africa is underdeveloped is a complex issue involving many factors. Hata hivyo, Ulaya imechangia kwa kiasi fulani whether direct or indirect.

Kitu kingine ambacho nadhani kinatuadhiri ni kuwa tunatumia Ulaya kupima level ya maendeleo yetu. Kwa mfano, tumeona Ulaya walijenga hizi apartments za kuishi kama ni maendeleo na sisi ndiyo tuanaanza kuzijenga kwa kasi sasa. Hata hivyo, huko huko Ulaya wameaanza kubomoa hizo apartments kwa kigezo kuwa they are not fit for purpose.

Lakini kwetu ndiyo kwanza they are fit for purpose. Tunakopi na kupaste yanayofanyika Ulaya kwa sababu tunadhani kila kinachofanyika huko ni maendeleo. Hatuangalii kama hayo maendeleo yanafit in our local circumstances.

Nchi za Ulaya zipo zilizoendelea na zile ambazo hazijaendelea zinajikongoja. Tena more interestingly wakati mwingine nchi iliyoendelea sana inapakana na nchi inayojikongoja!

Na ukiangalia nchi nyingi za Ulaya zinazojikongoja hazikujihusisha moja kwa moja kwenye biashara ya utumwa na ukoloni. Does this imply anything?


Simply meaning kama kusingekuwa na ile partition ya Afrika, labda tungekuwa mbali zaidi kimaendeleo?


Indeed, hata tawala nyingi kwenye nchi za Afrika zimekopi na kupaste system ya utawala iliyokuwa inatumika na wakoloni. They're using exactly the same system. The masters are still the same, sema tuu wamebadilika rangi. Bado tunatumia indirect rule ambayo ilifanya wakoloni wa-survive dhidi ya indigenous system.

Nilisoma somewhere that so far kwenye bara la Afrika, Botswana ndiyo nchi pekee ambayo mfumo wake wa utawala umetengenezwa based on indigenous institutions.
 
Nauliza: Ya kwanza kupata uhuru barani Afrika kwako wewe ni ipi?

Ya kwanza kabisa sijui. Ila najua kwamba Ghana siyo ya kwanza kwa sababu, kwa mfano, Sudan ilipata uhuru wake mwaka 1956 na Ghana ilipata uhuru wake mwaka 1957. Hivyo, Ghana haiwezi kuwa nchi ya kwanza Afrika kupata uhuru.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…