ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Hebu tupe brief ya hiyo historia uliyosoma, au at least list ya vitabu nikapige shule ya histori.
Kwenye historia upande wa Afrika, mie nilisoma "How Europe Underdeveloped Africa" by Walter Rodney.
Mwandishi aliandika kitabu hiki miaka 1960s mara tuu baada ya nchi za Kiafrika kujipatia uhuru wao.
Hivi kweli unaamini Europe ilii-underdevelop Africa? Mimi naona hicho kitabu cha bwana Rodney kimekaa kipropaganda zaidi kuliko kiuhalisia.
Africa ilikuwa underdeveloped hata kabla Europeans hawajaja.
Zipo sheria zinazoweza kuzuia siyo tuu kuuza nyumba bali hata kufanya marekebisho yanayobadilisha mwonekano wa hiyo nyumba.
Sheria za aina hiyo zinatumika sana kwenye listed buildings or heritage/historical buildings kama njia mojawapo ya kulinda majengo muhimu.
A listed buildings (hasa majengo ya Grade 1) hayawezi kubomolewa, kupanunuliwa, kufanyiwa marekebisho au hata kuuzwa bila idhini maalumu kutoka planning authority.
Inategemea una maana gani by the term "underdevelopment".
Kilichosabisha African underdevelopment ni complex issue, but Europe imechangia pia.
Whether or not hicho kitabu ni propaganda, inategemea na approach yako kwenye suala zima la uhusiano kati ya Europe na Afrika.
Basically, zipo three major views, Eurocentric approach, Afrocentric approach and historical approach.
Inadaiwa hiki kitabu ni baadhi ya vitabu vichache ambavyo at least vimejaribu kuangalia suala from the historical point of view.
Having said that Waafrika nao wamechangia na bado wanaendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa tuu to their own underdevelopment. Maana tokea uhuru, we are still underdeveloping
Kwani wewe kwako hilo neno linamaanisha nini?
Kama Europe imechangia basi mchango wake ni mdogo sana. Na kwanza sielewi hata imechangiaje wakati kulikuwa hakuna lolote la maana kabla wazungu hawajaja.
Hicho kitabu kimeandikwa kutoka kwenye mtazamo wa Afrocentric, kwa maoni yangu.
Hmm...nani anadai hivyo? Maana mimi naona ni kana kwamba kinataka kuaminisha watu kwamba Afrika ilikuwa sawa na Ulaya kwa kiwango cha maendeleo wakati watu wa hayo mabara mawili walipokutana. Mimi hiyo dhana sikubaliani nayo kabisa. Kama tulikuwa sawa kimaendeleo iweje wazungu waje watu bamboozle kiasi hicho?
Siyo tokea uhuru tu. Hata kabla ya uhuru hakukuwa na lolote la maana hadi wazungu walipokuja na kuanza kusomesha watu wetu maana sisi wenyewe hatukuwa hata na shule za maana.
Lakini mnachojadili hapa kiko tofauti na alichokisema mdau.
Yeye amesema Ulaya imeendelea kutokana na Afrika na sio kwamba Afrika haijaendelea kutokana na Ulaya.
Yaani mleta mada anaamini kuwa Afrika ndio iliyosababisha Ulaya iwe na maendeleo. Kwahiyo kama ni kitabu kingepaswa kuwa "How Africa Developed Europe"...
Last edited by a moderator: