Mkuu Kimweri nimependa maelezo yako, lakini challenge kubwa kwa haya mashirika ya umma ni construction costs na mfumo mzima ulivyo jinsi vinayoathiri ku-set competitive price, be it rental or sale price!
Sheria inawahitaji kutumia Public Procurement Act, na mara nyingine unakuta mradi ni affordable homes au low cost housing (How low is Low and how affordable is affordable is questionable) lakini anapewa Consultant Class One, na unajua bei za Class I na Class 5 au 7 ni tofauti!
Wakati huo kuna private developers wao wanatumia vibao tu (refer majengo yanayoanguka jijini Dar) utakuta Architect, Main Contractor, Sub Contractor, Electrical Engineer, Mechanical Engineer, Poject Manager, Quantity Surveyor etc lakini in reality kuna fundi ujenzi mzoefu alimradi anaweza ku-interpret michoro, na hao wengine ni geresha tu! Kwa mashirika ya umma, hao wote lazima wawe procured na kulipwa professional fees!
Hivyo ukiangalia mashirika ya umma, gharama ni kubwa na hivyo kuathiri sale/rental price maana kama investment lazima uangalie rate of return pia