Yesu aliumba Mbingu na Nchi

Mkuu, unataka kutuaminisha kwamba Mungu yupo lkn sio huyu wa uislam na ukristo. Sasa huyo unaemjua wewe tupe habari zake tumjue.
 
Mkuu, unataka kutuaminisha kwamba Mungu yupo lkn sio huyu wa uislam na ukristo. Sasa huyo unaemjua wewe tupe habari zake tumjue.
Je wajua Nyoka(dragon au dagon) nae alikuwa Mungu na kuna baadhi ya mataifa wanamuabudu mfn China,

Mungu mke nae alikuwa Mungu na aliabudiwa na ulimwengu wote kwa kujua ama kutojua.

Matendo 19:27
Si kwamba kazi hii yetu ina hatari ya kudharauliwa tu; bali na hekalu la mungu mke aliye mkuu, Artemi, kuhesabiwa si kitu, na kuondolewa utukufu wake, ambaye Asia yote pia na walimwengu wote humwabudu.

Muumba ni mmoja nae ndio the real Source hana mwanzo wala mwisho Kama wengi walivyofundishwa.

Sio mkristo wala muislam o bhudda yeye ni wa wote.
 
Hujajibu , muumba ni mmoja lkn yupi? Tupe habari zake.
Kibiblia inatanabaisha habari za miungu kuwa ipo mingi baada ya kutupwa duniani walijenga himaya zao na kuabudiwa. Kuna ashera, dagon nk. Yote Ni miungu, hata Yale mapigo kumi misri ilikuwa Ni miungu kumi ya misri iliyopigwa na Mungu muumba.

Hatutishwi na uwingi wa miungu, tunatishwa na sifa za Mungu mwenye uweza mbabe anayeweza kutamka na miungu yote ikafyata mkia. Hao ma artemi hushika baadhi ya maeneo madogo lkn hawana uwezo wa kumudu dunia yote Wala kujitangaza Kama afanyavyo Mungu wetu.
 
Imani logic yake ni imani.
Hapa ndo unapoanza kuhalalisha kisicho sawa, hata wewe mwenyewe unaona wazi kuwa hicho unachokiamini ni illogical.

Imani sio kuamini tu kibubusa! ... otherwise wewe unaamini vp kama kuabudu ng'ombe ni imani potofu? .... ukiona unashindwa ku-justify imani yako basi we jua huna tofauti na yule anayeamini ng'ombe kuwa ndo mungu na mwokozi wake.
 
Ambaye hataangamia ni yule tu atakaye mwamini Yesu Kristo kwamba alichukua dhambi zake na kufa msalabani kwaajili yake.
Una maanisha mtu aamini tu kibubusa? how do u reconcile the correctness ya upande mmoja ikiwa kuna dini nyengine na yenyewe inasema wokovu ni kupitia imani hiyo tu? tufanye "ana ana doo" ama?

Hata Musa alipotaka kuthibitisha kuwa imani yake ni superior kwa wale makuhani wa kichawi alidondosha fimbo yake chini na ikageuka nyoka mkubwa na kuwameza wale nyoka wa kichawi ... hakuna blaa blaa katika imani.
 
Amen, Yesu Kristo ni Mungu mkuu
 
Yani ajabu yenu nyinyi ni kuwa mnaziacha verses zilizo clear na kujichanganya na zile zilizo ambiguous. Mfano mzuri ni hiyo verse hapo chini

John 17:3 "Now this is eternal life: that they know you, the only true God, and Jesus Christ, whom you have sent."
 
Ubarikiwe sana
 
Unatumia mistari ya Biblia kuthibitisha Imani ya Biblia hiyo hiyo, huo sio usomi.
Sawa na kusema wewe Mungu kisha ila uthibitisho wako no kitabu ulicho andika mwenyewe
Stupidity
 
Unatumia mistari ya Biblia kuthibitisha Imani ya Biblia hiyo hiyo, huo sio usomi.
Sawa na kusema wewe Mungu kisha ila uthibitisho wako no kitabu ulicho andika mwenyewe
Stupidity
Majibu yote yapo ndani ya biblia. Biblia ndio funga kazi.
 
Chukua aya nzima ya 17
 
Yesu si mungu na hajawahi kuwa mungu
Hata ROHO MTAKATIFU ni mungu tumia akili kutambua uwezo wa utendaji wa mungu ...musa aliona mti unawaka moto ule mti na moto vilikuwa ni mungu.

Mungu anaweza kujigeuza kitu chochote ila hakuna aliye wahi kuiona nafsi ya mungu ...maana hata sisi binadamu hatujawai kuziona nafsi zetu....tatizo lenu waislamu na wakristo mmeshindwa kujua MUNGU NA YESU NA ROHO MTAKATIFU NI NINI..!?🤔🤔
ndiyo maana wakristo wapumbavu wanapotosha kuwa mungu ana nafsi tatu ....Kusema mungu ana nafsi tatu ni upumbavu....
💥Sasa nitaeleza Mungu na Yesu na Roho mtakatifu ni nini ? hadi vyote hivyo viwe ni 👉 Mungu mmoja Nafsi moja.

1) MUNGU NI NAFSI YA MUNGU MWENYEZI
2) YESU NI NAFSI YA MUNGU NDANI YA MWILI WA MWANADAMU USIO NA NAFSI YA MWANADAMU
3)ROHO MTAKATIFU NI NAFSI YA MUNGU NDANI MWILI WA MWANADAMU WENYE NAFSI YA MWANADAMU ( yaani nafsi mbili ndani ya mwili mmoja) ....

Kitu kingine ni kutambua Yesu anapo sema "MWANA" umaanisha mwili wake...na anapo sema "BABA" umaanisha Nafsi yake ambayo ndiyo Mungu Mwenyezi.
Sasa baada ya fafanuzi hii nakushaurini kasome Injili yote upya kwa kutumia fafanuzi hii kisha mtajua nini ni nini.... kisha tumieni fafanuzi hii kujibu maswali yote ya mashehe wanayo hoji kuhusu yesu utapata majibu kamili ...

Mfano waislamu wanasema 👉Hakuna aliye muona mungu duniani na biblia inasema hivyo hivyo je kama Yesu nini Mungu mbona kaonekana? Jibu ni kuwa 👉Yesu ni Nafsi ya mungu ndani ya mwili wa mwanadamu hivyo bado hakuna aliye muona mungu ....

Swali lingine la waislamu ni hili 👉je Mungu anakufa hata sekunde moja ? Jibu ni👉 hapana Mungu awezi kufa hata sekunde moja ...waislamu watakuuliza sasa mbona Mungu yesu kafa na kufufuka siku ya 3 je huyo ni Mungu gani anaye kufa ? ...hapa kwa kutumia fafanuzi za yesu ni nani na ukienda msalabani tunamsikia Yesu akimwaidi yule mtu waliye sulibiwa naye kuwa 👉leo hii utakuwa pamoja nami pema peponi ...hapa waislamu watakuambia biblia inajichanganya 🤕 kwa sababu wakristo mmesema yesu alikufa msalabani na kufufuka siku ya 3 sasa hapa mbona inasema yesu alikuwa pema peponi siku ile ile...jibu 👉 kilicho kufa na kufufuka siku ya tatu ni MWILI WA YESU SIYO NAFSI YA YESU KWA SABABU NAFSI YA YESU NDIYO NAFSI YA MUNGU MWENYEZI...ndiyo maana msalabani anamwambia yule mtu leo utakuwa pamoja nami pema peponi ...hivyo Mungu akufa msalabani bali alitoka ndani ya mwili na kufanya mwili kuwa mfu kwa sababu mwili ulibaki bila ya nafsi ...huko ndiyo kufa kwa yesu....sasa utajua kuwa nikweli mungu hawezi kufa hata sekunde moja ...
Kisha siku ya tatu Nafsi ya mungu ikarejea ndani ya mwili wa Yesu kaburini na mwili ukafufuka.

Bwana Rabbon Bwana Utam FaizaFoxy adriz ...njoeni mjifunze injili ya kweli mumjue kwanini kristo anaitwa mfalme
 
Mungu ni MMOJA NAFSI Moja.

Awapo KITI Cha enzi ni Mungu BABA.

Akija katika mwili wa mwanadamu kuokoa ni Mungu Mwana.

Aishipo ndani ya Mtu Ili kumsaidia kujitakasa aitwa Mungu Roho mtakatifu.

Na Jina la Mungu huyo mmoja tulilopewa WANADAMU liwezalo kuokoa ni Yesu Kristo/YESHUA HAMASHIACH.

Ubarikiwe 🙏
 
Yani hakuna mtu aliyewahi kusikia concept ya utatu mpaka ukirsto ulivoenda Roma!
 
Nashusha injili ya kweli tofauti naya makanisani ndiyo maana wakina FaizaFoxy wamepoa baada ya kuwashushia nondo sahihi wanabaki kushangaa tu...mimi sikukubali mafundisho ya injili kuwa ni yakweli kwa kufuata mkumbo in short wazazi wangu walikuwa waislamu hivyo ninapo sema kuhusu dini siongei kishabiki ndiyo maana injili ninayo ijua mimi ni tofauti na injili ya makanisani iliyo potoshwa.
 
Sasa badili hiyo avatar ya zombie.

Umeijua Nuru, kuwa Nuru uangaze.
 
Ikikupendeza,

Uje utupe ushuhuda wa mapito Yako kiimani Hadi kuijua Kweli Toka huko kwenye dini Ile.
 
Yani hakuna mtu aliyewahi kusikia concept ya utatu mpaka ukirsto ulivoenda Roma!
Tapeli alipo kosa jibu la ukweli utumia uongo ...sasa siku jibu la ukweli likija yule tapeli ubaki anashangaa maana jibu huwa limenyoka kiasi awezi kulikanusha ndiyo hii habari ya nafsi tatu ....hapa wakristo wanaodai nafsi tatu na mitume yao feki kina mwamposa uwezi kuwaona wanakuja kutetea hoja zao mbele yangu... ninaijua injili yote ya kweli kwa asilimia 100 ni tofauti kabisa na hiyo ya makanisani kwenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…