Ok sawa, sijui tatumia lugha gani ili uweze nielewa acha nijaribu.
Lengo la mungu ilikuwa kuishi na mwanadamu kwa ukaribu Kama ilivyokuwa edeni kwenda kuwatembelea wakati wa jua kupunga. Lkn pia mawazo ya mwanadamu wakati huo ilikuwa Ni kuwaza mema tu hapakuwa na mawazo mabaya. Kumfikiria Mungu kumpenda na kumsifu kwa kazi yake.
Dhambi ilipoingia tulibadilika kabisa kutoka utukufu na kuwa chini ya dhambi yaani watumwa wa dhambi, akili na mawazo yote yalitawaliwa na dhambi hivyo kila tuwazalo na tufanyalo inakuwa kwa ajili yakumkosea Mungu kwakuwa ndivyo dhambi inavyohitaji tufanyalo.
Kwa hiyo Sasa Mungu akawa amebaki kuduwaa na kutushangaa namna tulivyo mtenga badala yakupata sifa kutoka kwetu badala yake anapata machukizo. Dhambi ikabadili kabisa mfumo wa maisha ambao Mungu alikuwa ameupanga na kwakuwa tayari alikuwa ameshaweka adhabu yakifo aliacha tuendelee kufa Hadi pale alipoandaa mpango wa wokovu.
Tukirudi kwako kuwa baada ya mpango wa wokovu dhambi zilipungua?
Dunia baada ya dhambi ililaaniwa Sasa Mungu hawezi kuilaani alafu Tena awake maisha ya milele kwenye eneo lenye laana hapana. Anasema hajipingi. Kama alivyombariki adamu hakuweza kumlaani Tena baada ya anguko la dhambi badala yake aliilaani ardhi. Hivyo Basi aliandaa eneo la maisha mengine mapya ya utakatifu kwa wateule watakaoshinda baada yakuishi kwa kumcha Mungu kwenye dunia iliyo chini ya utumwa wa dhambi.
Sasa baada ya yesu kuondoa kiambaza kilichotutenga, ndipo Sasa tunakufa karibu na Mungu kwa kuongea nae, na kuwa karibu nae. Hapa Ni kwa wale waliookoka ndio wanaelewa vizuri, kwa mtu ambaye bado anaishi dhambini hawezi kunielewa.
Dhambi zinapungua kwa watu wanaoishi utakatifu. Wewe huwezi kujua sababu bado hujaanza kuishi utakatifu.
Katika majira zote saba zilizopita hakuna mtakatifu aliwahi kuvuka na kumfikia Muumba hata mmoja.Ikabidi aje yeye mwenywe kuishi nasi.Rejea
Luka 16:19-26
Hata lazaro alipokufa alifikia kifuani mwa Ibrahim kufarijiwa na sio kwa Muumba wake.
Daniel 7:21
Nikatazama, na pembe iyo hiyo ilifanya vita na watakatifu, ikawashinda;
Ufunuo 11:7
Hata watakapoumaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika kuzimu atafanya vita nao, naye atawashinda na kuwaua.
Muumba alilazimika kuja kuishi nasi na kututoa kwenye utumwa baada ya waliotumwa wote kushindwa hata baada ya kumtuma Yesu maana kusudi lake halikuwa sisi kufa bali kuishi umilele naye.Rejea
Ufunuo 21:3
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
Isaya 57:15
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na moyo uliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Hosea 13:14
Nitawakomboa na nguvu za kaburi; nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu.
1Korintho 15:51
Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala(kufa) sote, lakini sote tutabadilika,
Mhubiri 3:11
Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo
milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.
Yesu mwenywe alisema Muumba(aliyemtuma) asipofupisha siku hakuna mtu angepona hata ile damu yake iliyomwagika kuna fumbo dunia ilificha ya walivyoiba alivyokuja navyo katika efeso 1:21-23 ndo maana akasema katika
Mathayo 26:29
Lakini nawaambieni, Sitakunywa kabisa tangu sasa uzao huu wa mzabibu, hata siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.
Alisema hayo akijua Muumba atakuja na damu yake mwenywe kutukomboa maana yake waliiba na kuchukua kila alichokuja nacho. (lilikuwa fumbo la imani)