Yesu hakupigiliwa misumari kwenye viganja vya mikono!

Yesu hakupigiliwa misumari kwenye viganja vya mikono!

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Wachoraji wa picha za Yesu akiwa msalabani mnatakiwa kuelewa historia ya ile adhabu ya kifo enzi zile. Misumari ilikuwa inapigwa hapo mahali unapovaa saa ya mkononi siyo katikatiya kiganja kama picha nyingi zinavyoonyesha.

Sababu ni kwamba wangepiga misumari katikati ya kiganja na kumning'iniza mtuhumiwa msalabani basi misuli ya viganja haingeweza kuhimili uzito wa mwili na viganja vingechanika na msulibiwa kuanguka chini.

Upo ushahidi wa kutosha wa sayansi ya manbo ya kale uliogundua mifupa ya waliosulibiwa ikonyesha mahali misumari ilipopigiliwa.

Ndugu zetu Mashahidi wa Yehova huwa wanachora kwa usahihi japo kuna ubishi kama msalaba ulikuwa ni nguzo moja au mbili. Wachoraji wetu rekebisheni hilo tafadhali.
 
Biblia waongo ila wewe uliyezaliwa juzi ndio mkweli?

Biblia haihitaji hata siku.moja tafsiri kutoka mavitabu mengine ya kuokoteza barabarani

Ikiandika msalaba ina maana ya msalaba sio gogo lililosimama wima
Amka kijana.
Hivyo vitabu vya dini, ni story za kutunga tu.
Ni uongo na vitisho tu.
 
Back
Top Bottom