Yesu Kristo aliuawa kwa sababu za kisiasa zaidi kuliko za kidini

Nime-highlight sehemu hiyo hapo juu kwa sababu ya maneno: Kifo cha Yesu Kristo. Hivyo basi, ninataka kujua msingi wa madai yako kwamba, "Yesu Kristo aliuawa kwa sababu za kisiasa zaidi kuliko za kidini".

Vitabu vyote ulivyofanya rejea, vimeandika kuwa, kazi ya Yesu, aliyofanya katika kipindi cha miaka mitatu, na ambayo ndio ilipelekea kifo chake, ilikuwa: "Kufundisha na Kuhubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu". Kwa maana nyepesi, Yesu alishughulikia mambo ya dini tu.

Ni wazi Yesu hakuwa na tatizo na Wayahudi au watu wengine wowote wa wakati wake, wala utawala wa Warumi. Ugomvi wa Yesu ulikuwa kati Yake na Mafarisayo, na Waandishi, ambao hawa walikuwa watalaamu wa dini ya kiyahudi, na Yesu alitofautiana nao kwamba mengi, ambayo yanaweza kuhitimishwa kwa neno: Unafiki.

Sasa, kwa kuzingatia kazi ya Yesu, ambayo imeelezwa wazi kwetu sisi wote, ni kwa namna gani Kifo Chake kiwe cha kisiasa na sio kidini?
 

YESU HAKUSULUBIWA WALA HAKUUAWA ; ALIYESULUBIWA NI SIMON Sikiliza mpaka mwisho upate jibu, tumia KJV



View: https://www.youtube.com/watch?v=x6pF9WG3HaA&t=367s&pp=ygUoc2hlaWtoIGFiZHVsbGFoaSBhbmQgY2hyaXN0aWFucyBpbiBrZW55YQ%3D%3D
 
Ilitabiriwa kuwa atauawa na waliotimiza utabiri huo ni Wanasiasa, ila sababu za kifo chake si za kisiasa kwa sbabu hich kifo tayari kilikuwa kimeshatabiriwa
Wao walidhani kuwa anataka kuwanyang'anya maslahi yao.
Aliuawa na wanasiasa lakini sababu za kifo chake ni ili utabiri utimie
Kwa hiyo tunaweza kusemani kuwa ni sababu za kisiiasa zilizottimiza utabiri wa kifo cha Yesu na si kwamba Yesu aliuawa kwa sababu za kisisasa
 
Swali hili si lazima kujibu kama hujalielewa au huwezi kulijibu KABLA HIZI DINI KUJA AFRICA ILIKUA KUNA TAMADUNI ZA MATAMBIKO KATIKA KILA KABILA NA MIUNGU YAO PIA. JE, HIKI KIZAZI CHOTE CHA KABLA YA HIZI TUNAZOZIITA DINI ZENYE VITABU VITAKATIFU NA SHARIA ZAKE WOTE WAMETUMBUKIA MOTONI KAMA MWANADAMU WA SASA AMBAYE ASIYE NA HOFU JUU YA MUNGU NA ASIYE NA MUDA WA KUMUABUDU.............!?
 
Hayo uliyoyasema yote yalitakiwa yatimie ili litimie neno alilosema nabii isaya 53:1-12
 
Somo zuri asante kwakuniongezea maharifa Leo kichwani mwangu
Ila majibu ya yesu kwann yalikuwa sio ya Moja kwa Moja?
Yaani ukimuuliza swali anakujibu kwa swali!!!!
Mfano kwenye kutoa ushuru,
Hayo maswali walikuwa wanamuuliza ili kumtega wapate namna ya kumshitaki kwa sheria zao za kidini au kumchonganisha na Watawala,kwa sababu yeye alijua mawazo yao nayeye alikuwa anawauliza ili wakijibu wajitege wao kwa majibu yao wenyewe.
 
Mwanasiasa Pilato alinawa mikono na kusema mtu huyu hana hatia. Hajuna siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…