Huduma ya Yesu ilihudumiwa na voluntary giving za watu walioona ukweli wa huduma yake (siyo haya mazingaombwe na motivational speeches za hawa wahubiri uchwara wa leo). Wala mitume wa Yesu wala hakuna popote kwenye maandiko ya kikristo (Agano Jipya) kumesema utoe fungu la kumi. Mtume Paulo aliyeandika sehemu kubwa ya Agano Jipya aliagiza tu kuchanga chochote ili kuwasaidia maskini waliokuwa wakiishi Yerusalemu. Matapeli wamekuja na fundisho la Wayahudi la fungu la kumi na kwa sababu wajinga hawaishi wametoboa hasa. Kama wewe unasema fungu la kumi bado ni lazima basi unasema pia sadaka za kuchinja wanyama ni lazima. Ukisema hilo Yesu alilimaliza msalabani unakimbia kivuli chako mwenywe. Mengine yote ya biblia ya Wayahudi huyataki ati wewe ni mkristo ila fungu la kumi ndio unalikumbatia. Huo ni uongo na wizi uliojificha kwenye mafundisho yasiyokuwepo kwenye hilo Agano jipya unalolihubiri. Utapeli mtupu na wizi wa mchana kweupe.