Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 9,397
- 12,415
JINA LA YESU LITUKUZWE WATOTO WA MUNGU!
Watu wa Mungu walio okoka na ambao bado hawajaokoka! Leo ngoja tuzungumze juu ya Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai! Leo natangaza habari za wokovu! Leo natangaza jina lipitalo majina yote jina la YESU KRISTO!
JINA LA YESU LINA NGUVU!
Maana maandiko yasema katika Matendo 4:12:
“Wala hakuna wokovu kwa mwingine awaye yote; kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo kuokolewa kwalo, ila jina la Yesu!”
YESU ni jina la uzima. YESU ni jina la uponyaji. YESU ni jina la rehema. YESU ni jina la ushindi juu ya dhambi, juu ya giza, juu ya kifo!
Yesu Alikuja kwa Ajili Yako!
Yohana 3:16 yasema:
"Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwana wake wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."
Yesu hakutumwa kwa matajiri tu, wala kwa watakatifu tu, wala kwa viongozi wa dini tu, alikuja kwa ajili ya mkulima, mfanya biashara, kijana wa mtaani, kahaba, mlevi, mchawi, na kila mtu! Hii ndiyo neema ya Mungu!
Yesu Alikufa Lakini Akafufuka!
Wengine walikufa wakabaki kaburini. Yesu peke yake alifufuka! Maandiko yanasema katika Luka 24:5-6:
"Mbona mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu? Hayupo hapa, amefufuka!"
Yesu yu hai! Yesu si historia, YESU ni HALISI! Yuko leo kuokoa, kuponya, na kuweka huru!
Rudi kwa Yesu Leo Kabla Haijachelewa!
Ndugu yangu, dunia hii inapita. Anasa, pesa, cheo, uzinzi, bangi, pombe vyote vitakoma. Lakini roho yako ni ya thamani. Usiiuze kwa dhambi. Usicheze na wokovu. Yesu anasema katika Ufunuo 3:20:
"Tazama, nasimama mlangoni nabisha; mtu akisikia sauti yangu na kuufungua mlango, nitaingia kwake."
Leo ni siku ya wokovu. Leo ni siku ya kumfungulia Yesu mlango wa moyo wako.
Tubu na Mkabidhi Maisha Yako Leo!
Piga magoti kama unavyojisikia. Funga macho. Sema:
“Ee Bwana Yesu, najua nimekosa. Najua nimekataa sauti yako mara nyingi. Lakini leo, nimerudi. Nisamehe dhambi zangu. Nioshe kwa damu yako. Ingia moyoni mwangu. Andika jina langu katika Kitabu cha Uzima. Na kuanzia leo, nitakutumikia. Wewe ni Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Amina!”