Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Status
Not open for further replies.
Yesu Kristo anajulikana katika Quran kama Neno la Mungu.roho ya Mungu kuna maana gani hapo.Mungu aliumba kila kitu kutumia neno.je neno ni nani
Maandiko yako wazi tatizo ni uelewa wako na walimu wako wa imani nadhani ni vyema unajifunza zaidi kuhusu imani yako ujue ni kama allah ni Mungu kwanini anaapa kwa aliyeumba mbingu na ardhi.?
 
Amekamatwa??
Yuko mahabusu??
Kesi lini kwani??
Mfuate huyo Paulo mkamalizane huko huko maana sisi unaotuambia hatuna mamlaka yoyote juu yake.... na ujue hapa sio mahakamani ebooooh [emoji35] [emoji35] [emoji41] [emoji41]
 
Kumbuka we huwezi kumfanya Yesu awe Mungu au asiwe Mungu. Kama kuangamia naona ni wewe utaangamia kwa kapinga ukweli Yesu ni kweli na uzima.
 
Maandiko yako wazi tatizo ni uelewa wako na walimu wako wa imani nadhani ni vyema unajifunza zaidi kuhusu imani yako ujue ni kama allah ni Mungu kwanini anaapa kwa aliyeumba mbingu na ardhi.?
Acha ushamba wa maandiko......hapo anaambiwa mtume wetu kuapa na siyo Mungu ndiye anayeapa wewe. Mmejitahidi sana kupotosha maandiko ili kuupakazia uislamu lakini mmekwama. Poleni sana bandugu....
 
soma hii ufunguke!; omary ibn khatab alimuuliza mtume sababu ya kushuka baqara 223!; akasema imeshuka kwa ajili ya kuwaingilia wanawake tupu zao za nyuma..
Addrul manthur j.uk 473
Fat'hul baary j.8 uk.38-39
Kasome ufunguke!; Allah amewafaridhia ndogo kwa nini mnatakaabar? kula tu..hhhhhhhhhh...
Uongo mkubwa huo. Hiyo baqara 223 imekataza kuwaingilia wanawake nyuma iweje hiyohiyo iruhusu kuwangilia nyuma? Huo ni ujinga na upu.mbafu wa makaratasi yakuokota waliyotunga walokole. Pole sana!!!!
 
Akili yako imeishia hapo. Hazikutoshi, ipo siku utaju kuwa Yesu Kristu ni kweli na uzima. Mohamed mwenyewe kapinga sana ukirsto mwisho kafa yeye ukirsto upo utakuwa wewe?
Pole sana. Huwa mnaishia kutukana na kusisitiza ipo siku tutajua Yesu sijui ndo kristo mara sijui ni Mungu mara ni Mwana.....eeeeh haieleweki tushike lipi. Toa maandiko na wewe acha kutukana ewe unayejifanya pasta.
 
Matayo 28:19 ```Basi,enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu""""""

Mstari huu unakuonyesha mambo kadhaa Dotto,,,,
1.Yesu sio mtume(ktk Qur'an Yesu sio issa ila Yahsua ibn masihi) issa anaweza kuwa mtume ila YESU Hana hadhi ya chini kiasi hicho..YESU Anaongelea utatu mtakatifu hapo na hadhi yake ni MUNGU.

2.Yesu ni mwana wa MUNGU na kama ilivyo mwana wa binadamu ni binadamu basi pia kama ilivyo YESU ni mwana wa MUNGU basi yeye ni MUNGU.Yeye alizaliwa kabla ya kuumbwa kiumbe chochote ""Wakolosai 1:15-17"""pitia hapa kuna maneno ya kweli na kila unachotaka kuelewa kuhusu YESU.

3.Usiwe unamuongelea Paulo kulingana na viongozi wako wa dini wanaomdharau na kumchukia(nimesikia wengine wakijitoa ufahamu na kumwita Shoga)) Jiulize kwamba Yeye alie katika Ukristo amezuia nini katika dini Yenu ya Uislam,,,amehatarisha maslahi ya nani???
Kwa nini mnashindwa kuongea mambo mnayoyaona sahihi kwa kumhofia???

Je!! Wewe muislamu utaweza kumbainishia mkristo ubaya wa Paulo kulingana na uelewa wako mdogo na mtazamo wako finyu wa biblia??

Je!? Huwezi kumwongelea Yesu pekee pasi na kumchanganya na Paulo mtume wa mataifa??

YESU KRISTO HAKUTUMWA KWA WATU WOTE

Yesu Kristo anasema; "Msidhani ya kuwa nilikuja kuitangua Torati au Manabii, la, sikuja kutangua, bali kuitimiliza. Kwa maana nawaambieni, mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka yodi moja na nukta moja ya Torati haitaondoka mpaka yote yatimie (Mathayo 5:18-18)"

Ni dhahiri kuwa Nabii Musa na manabii wengine waliotangulia walikuja kuwafundisha na kuwaongoza Waisraeli tu. Yesu Kristo amekwisha kubali katika maneno ya juu ya kuwa amekuja kulitimiza kusudi lile ile ya Musa na Manabii wengine waliotangulia.

Lakini tunaona mapadri wamekwisha fika katika kila sehemu ya dunia hata Afrika ijapokuwa Yesu Kristo mwenyewe hakuwa na nia na kusudi ya namna hii kabisa.

Sasa swali hasa linalotakiwa kufikiriwa, si Wakristo wanafanya nini, bali ni, "Je, Yesu Kristo alikuwa na nia na azimio gani?"

Mwenyezi Mungu alikuwa na kusudi gani alipomtuma Yesu Kristo?

Jambo hili haliwezekani kuelezwa kwa njia nzuri na yeyote isipokuwa lielezwe na Yesu Kristo mwenyewe.

Na Yesu amekwisha sema wazi "Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya lsraeli (Matt. 15:24).

Tena akasema, "Mwana wa Adamu alikuja kukiokoka kilichopotea (Matt. 18:11)."

Kwa hiyo mafundisho ya Yesu Kristo ni kwa ajili ya Waisraeli tu si kwa watu wengine kabisa.

Inasemekana kwanba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine kabisa,

Inasemekana kwamba Yesu Kristo aliwaagiza wanafunzi wake waende kwa watu wengine pia.

"Basi endeni kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi mkiwabatiza kwa jina la baba na-roho mtakatifu. (Matt. 28:19)"

Lakini kushika dalili katika maneno haya kuwa Yesu Kristo aliwaamuru wafuasi wake kupeleka ujumbe wake kwa watu wengine wote wasio Waisraeli, pia si sawa.

Maana Yesu Kristo amesema wazi kabisa:

"Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata katika zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara. Mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli (Matt. 28:19).

‘Tena, "Sikupelekwa ila kwa kondoo zilizopotea za nyumba ya Israeli (Matt. l5:24).

"Tena, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa (Matt. 15:26)

"Sio haya tu bali pia tunasoma,

"Hawa thenashara Yesu aliwatuma akawaagiza, akinena, katika njia ya mataifa msiende wala miji mwa Wasamaria msiingie; Afadhali shikeni njia kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli (Matt. 105-6)""

Kutoka kwa mafungu ya maneno haya ni kuwa wafuasi wake wameamrishwa naye kupeleka ujumbe wake kwa mataifa yote ya Israeli si mataifa yote ya ulimwenguni. Mtu asidhani ya kwamba mawazo ya maneno yajuuni kuwa waende kwanza miji ya Waisraeli na baadaye kwenye miji mingine. La, maana kwenda kwa kondoo waliopotea wa Israeli si maana yake kuvitazama vijiji tu, bali ni kuwaingiza katika dini ya Ukristo. Basi kwa hakika maana hasa ya maneno haya ni kuwa Waisraeli wote waingie katika Ukristo, Mkristo na padri ye yote asijielekeze kabisa kwenye mataifa mengine. Yesu Kristo amehakikisha wazi wazi ya kuwa kazi ya kuwahubiria dini Waisraeli na kuwaingiza katika njia yake haitamalizika mpaka kufika kwake mara ya pili, kama ilivyosema:

"Watakapowaudhi katika mji huu, kimbilieni mwingine kwa maana ni kweli nawaambieni, Hamtaimaliza mji yote ya Israeli hata ajapo mwana wa Adamu (Matt.10:23).

"Katika maneno haya inajulikana wazi ya kuwa yaliyosemwa katika Mathayo (28:19) makusudio yake ni kwamba wahubiri Wakristo wasimamishe Ukristo katika miji ya Israeli na waingize kabila la Israeli katika dini yao si kuvitembelea tu na kuvitazama vijiji vya Waisraeli. Na pia ni wazi ya kuwa kazi hii ya kuhubiri na kuwaingizia haitamalizika mpaka Yesu Kristo aje mara ya pili. Kwa hiyo kuwahubiri watu wengine wasio katika mataifa ya Israeli ni kinyume kabisa na mafundisho na maagizo ya Yesu Kristo. Hata mitume wa Yesu pia walifahamu kuwa ni kosa kuwahubiri watu wengine wasio Waisraeli. Tunasoma:

Mimi nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata katika zamani za kuzaliwa upya atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu.

"Basi wale waliotawanyika kwa sababu ya ile shida iliyotokea kwa habari ya Stefano wakasafiri hata Foiniki na Kupro na Antiokia. Wasilihubiri lile neno ila kwa Wayahudi peke yao!! (matendo11:19)."

Hivyo, mitume wa Yesu waliposikia ya kuwa Petro aliwahubiri watu wasio Israeli pahali fulani, wakakasirikia nawakashindana naye:

"Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemi, wale walio wa Tohara wakishindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao" (Matendo 11:2-3)",
 
Hawa mataifa umewaelewaje?? Ukiacha Paulo ambaye kazi alioifanya haina kifani alihubiri ugiriki,,Macedonia,Syria,Italy nk.Mtume wa YESU Yohana alieandika kitabu cha Ufunuo aliandika kitabu hiki akiwa amewekwa kizuizini katika nchi ya Uturuki.Maana yake na yeye alikuwa akiwahubiria mataifa.""Yohana3:16 Kwa maana jinsi hii, MUNGU aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanae wa pekee ili KILA amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele.
 
soma hii ufunguke!; omary ibn khatab alimuuliza mtume sababu ya kushuka baqara 223!; akasema imeshuka kwa ajili ya kuwaingilia wanawake tupu zao za nyuma..
Addrul manthur j.uk 473
Fat'hul baary j.8 uk.38-39
Kasome ufunguke!; Allah amewafaridhia ndogo kwa nini mnatakaabar? kula tu..hhhhhhhhhh...

Adrul manthur na Fat hul barry ni vitabu vya kanisa katoliki ?

During the Last Supper the Gospel of John describes how the “beloved” disciple laid himself on Jesus’ inner tunic — his undergarment – John 13:25 and 21:20

“In the Book of John a word is used eight times that means ‘is in love with’ with the implication of sexual intimacy.

Five times it is used with reference to Jesus’ relationship with John.

Once it is used to define Jesus’ relationship with Lazarus.

And it is also used to describe his relationship with Mary and with her sister Martha.

In John 19:26-28, Jesus is described as seeing an unidentified man: “the disciple standing by, whom he loved.

Again this particular disciple is identified as “the” disciple who Jesus loved. Again, not the common love he had for all of his disciples but a VERY special love

Robert Goss, assistant professor of comparative religion at Webster University, stated that Jesus and the beloved disciple: “… eat together, side by side. What’s being portrayed here is a pederastic relationship between an older man and a younger man. A Greek reader would understand.” Anyone that has studied Greek History would also understand.
 
Paulo anaweza kua sawa tu,kwa MUNGU yote yawezekana kama alivyoweza kumtengeneza popo.wengine wanamuita ndege na wengine humwita mnyama.yamkini YESU alikua BINADAMU na MUNGU pia
VIPI HAPA NDO MWISHO WAKO WA KUFIKIRI AUU....
 
Hawa mataifa umewaelewaje?? Ukiacha Paulo ambaye kazi alioifanya haina kifani alihubiri ugiriki,,Macedonia,Syria,Italy nk.Mtume wa YESU Yohana alieandika kitabu cha Ufunuo aliandika kitabu hiki akiwa amewekwa kizuizini katika nchi ya Uturuki.Maana yake na yeye alikuwa akiwahubiria mataifa.""Yohana3:16 Kwa maana jinsi hii, MUNGU aliupenda ulimwengu,hata akamtoa mwanae wa pekee ili KILA amwaminie asipotee bali awe na uzima wa milele.

The Interpreter's Bible, sahifa 441 jalada VII ambamo imeandikwa hivi:

"Yaonekana wazi kuwa Yesu hakika aliamini kuwa ujumbe wake kwanza na khasa ni kwa watu wake mwenyewe." Ndio maana alisema:

Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua
. Mathayo 7.6

Mbwa
na nguruwe ni watu wa mataifa yasiyokuwa wana wa Israili.

Ukristo haufai kufundishwa watu wo wote isipokuwa Mayahudi.

Hayo ndiyo mawazo ya Yesu, au ya hao walioandika Injili na wakatia maneno hayo kinywani mwa Yesu.

Tukiendelea na isemavyo Biblia juu ya ujumbe wa Yesu tunapata ushahidi zaidi kutokana na Injili ya Mathayo:

Hao Thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Mathayo 10.5-6

Hao Thenashara ni wanafunzi wake kumi na mbili aliowateua mwenyewe Yesu kutangaza mafunzo yake.

Hapo anawapa amri zilizo wazi kuwa wasiwaendee watu wa Mataifa, yaani wasiokuwa Waisraili.

Hao wanafunzi kumi na mbili ndio wanaoitwa katika Biblia "mitume" kwa kuwa walitumwa na Yesu.

Na wao kama yeye mwenyewe hawakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa Israel" kwani "si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa." Na wanawakirisha kabila 12 za israil.

Yesu alionya, lakini Paulo hakusikia:

"Katika njia ya Mataifa msiende, wala katika mji wo wote wa Wasamaria msiingie. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na wakawararua."

Akazidi kuwaasa: "Mwanafunzi hampiti mwalimu wake bali yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake" Mathayo 10:24

Lakini tunaona paulo amempita hata mwalimu wa walimu, na hii inadhihirisha kuwa Paulo hakuwa mwanafunzi wa Yesu.

Yesu anasema; Jitieni nira yangu mjifunze kwangu" (Mat 11:29-30) Sasa ndugu yangu wewe unajifunza kwa nani mpaka useme Yesu ni Mwokozi wa Ulimwengu?
 
Matendo ya mitume10&11 kuna majibu yako yote.Ukiwa na mda pitia.
 
Kwa nini Yesu alisema maneno kama haya ya kukataa na kukataza kuwafunza dini ila Waisraili tu?

Kwa nini alitumia mifano mibaya kama hivyo "mbwa" na "nguruwe" kwa kuwakusudia hao watu wengine wasio Mayahudi, yaani ndio mimi na wewe mwenzangu?

Wataalamu wa Kikristo na wasio Wakristo wamestaajabishwa na maneno hayo.

Ni maneno machache katika aliyoyasema Yesu ambayo yamewatatiza wasomaji Wakristo kuliko maneno haya.

Wapo wanaoona kuwa Yesu alitumia matusi yale kuwaita wote wasio Mayahudi kufuata mwenendo wa Kiyahudi, yaani ndio hivyo Mayahudi wawaonavyo binaadamu wote wasio kuwa wao.

Na wapo wasemao kuwa Yesu akipenda kufunza kwa mifano, na hivyo anafananisha kama kwamba yeye anaamini hiyo imani mbovu ya Kiyahudi ya kudharau watu wasiokuwa kabila yao.

Na wapo wengine ambao wanaona maneno yale ni ya Mathayo, na yeye Mathayo (au ye yote yule aliyeandika Injili hiyo) kamuambatisha nayo Yesu maneno hayo, kwa kuwa yeye mwandishi alikuwa Mkristo wa kabila la Kiyahudi na anacho kiburi cha Kiyahudi.

Ama kusema kuwa hakutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa Israeli inaonekana kama kilivyosema kitabu cha The Interpreter's Bible kuwa Yesu hakika kwanza aliamini kuwa alitumwa kwa Waisraili tu.

Ni jambo la kustaajabisha kuwa Mungu au Mwana wa Mungu aje duniani atumwe na kwanza asiujue utumwa wake ila aamini tu kuwa katumwa kwa watu wake wa Kiyahudi basi.

Na kama yeye ni Mungu au Mwana wa Mungu, katumwa na nani?

Kama katumwa na Mungu, basi yeye si Mungu.

Si hilo tu, bali hata akiwa ni Nabii na Mtume wa Mungu tunamtaraji aujue tangu mwanzo huo ujumbe wake aliokuja nao, asiwe kutapatapa, kupapasa, na kuhangaika katika jambo la msingi.

Hapana haja ya kuyatafutia tafsiri hii na maana hii, hayo maneno yaliyo wazi ya Yesu Kristo.

Yesu hakika hakutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

Yesu hakika kawakataza "mitume" wake wasende kuwahubiria mataifa mengine.

Yesu ni kweli kaonya kuwa kuwafundisha mafunzo yake hayo mataifa mengine ni sawa sawa na kuwapa mbwa kilicho kitakatifu, na kuwatupia lulu nguruwe. Kwa nini ikawa hivi?

Ikiwa Yesu kweli katumwa na Mungu, kwa nini ujumbe wake uwekewe mipaka kwa jamaa zake tu wa Kiisraili, na yeye asikiuke mipaka ile?

Naam, zipo sababu zenye nguvu kwa hayo.

Kwa hakika hayo hayakuwa mageni, wala Yesu hakuwa Mtume wa mwanzo kutumwa hivyo na Mwenyezi Mungu. Mitume wote waliokwisha kuja kabla yake walikuwa ni Mitume wa vikundi vyao tu, na zama zao tu, na walikuja na mafunzo yao maalumu machache.

Musa alikuwa hivyo, na Yesu hali kadhaalika. Hali yake hali ya wenziwe, ila yeye alikuwa ndiye Mtume wa mwisho katika Mitume waliotumwa kwa kabila maalumu. Kwa nini Mwenyezi Mungu akafanya hivyo?

Kwa nini Yesu alikatazwa, mathalan, asiwahubirie yeye wala wafwasi wake, Waafrika, au Wazungu, au Wahindi, au Machina, au Waarabu?

Amekatazwa kwa sababu kabila zote hizo zilikuwa hata hazijachukua khatua ya mwanzo ya kuamini Mungu Mmoja. Kabila hizo na mataifa hayo yalikuwa makafiri ama wa kuabudu masanamu, au kuabudu mapango au miti au viumbe vyengine au kuabudu wanaadamu wenzao. Na ujumbe wake Yesu ni kutengeneza mwenendo, tabia ya watu ambao tangu hapo wanayo imani ya Mungu mmoja. Yeye hakuwa na uwezo wala muda wa kujenga tangu chini.

Yeye kazaliwa katika umma wenye kuamini Mungu Mmoja, umma wenye sharia ya Mwenyezi Mungu.

Kazi yake kwa muda mchache alioishi na kuhubiri ni kiasi ya kuwapiga msasa tu Mayahudi ambao walikwisha tahiriwa, wanajua cha halali na haramu, na muhimu kabisa wanamjua Mwenyezi Mungu Mmoja, asiyezaa wala kuzaliwa. Ila yao Mayahudi ni kutokuwa na huruma, na kuifanya dini sharia tu isiyo na roho na imani.

Mayahudi waliishika sharia ya Musa kwa dhaahiri yake, lakini waliutupilia mbali uchamngu wa Ibrahimu, wakashika ya kuonekana na watu, na wakatupa ya ndani anayoyaona Mwenyezi Mungu na dhamiri zao.

Walipoacha "mitume" wa Yesu amri hiyo ya Mungu ya kutowendea makafiri wasiomjua Mungu wala msingi wa sharia, ndipo mafunzo ya Yesu yalipochafuka.

Kwani hao makafiri walipoingia katika Ukristo walijigeuza jina tu, lakini waliingiza karibu yao yote ya kikafiri katika dini ya Yesu, ikaitwa Ukristo, na hali sio Ukristo kabisa aliyoufundisha Yesu.

Mahekalu yao ya kipagani yakageuzwa makanisa, na mizimu na mapango yao yakawa ndio monastari za Kikristo.

Lau kuwa Wana wa Israili wangeli mwitikia Yesu, basi Ukristo usingelichafuka kama ulivyo chafuka.
 
Katika hio mistari niliokupa utaona petro mtume akiambiwa asimdharau yoyote bali awe Karibu hata na watu walioonekana wachafu,,pili hata mwanamke alieambiwa chakula cha watoto hawapewi mbwa baada ya kujinyenyekesha alipokea baraka yake na mwanae akaponywa.

YESU sio mtume labda unionyeshe popote pale kwenye biblia.
Wala sio nabiii kamwe,,

YESU ni mwana wa MUNGU.Na njia sahihi ya kufika mbinguni.
 
  • Thanks
Reactions: J C

Yeye mwenyewe Yesu amesema kuwa yeye ni Mtume, yeye ni Mtumishi, yeye ni Nabii.

Je, nini mawazo ya wale wafuasi wake waliomuamini na wakamwona na wakaishi naye?

Injili zinatwambia:

Basi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni. ------Yohana 6.14

Nao walipotafuta kumkamata, waliwaogopa makutano, kwa maana wao walimwona kuwa nabii.
Mathayo 21.46

Hata alipoingia Yerusalemu, mji wote ukataharuki, watu wakisema, Ni nani huyu? Makutano wakasema, Huyu ni yule nabii, Yesu, wa Nazareti ya Galilaya.------Mathayo 21.10-11

Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Akawaambia, ni Maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda mbele za Mungu na watu wote.--------------Luka 24.13-19

Injili kwa umoja wao zinathibitisha kuwa watu wake Yesu waliokuwa naye na kumuamini na wakaona miujiza yake tangu kuzaliwa kwake mpaka mwisho wake walimjua kuwa ni Nabii wa haki, naye ni mtu, mwanaadamu.

"Hakika huyu ni nabii", anasema Yohana.

"waliwona kuwa nabii", anasema Mathayo.

"Huyu ni yule nabii, Yesu", anasema tena Mathayo.

"Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii", anasema Luka.

Jinsi ya hadhari zake asisingiziwe kuwa anazo au anadai sifa za uungu, Yesu alikataa hata kuitwa "Mwalimu mwema".

Sikiliza masimulizi ya Injili ya Marko:

Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akmwuuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? Yesu akamwambia, Kwa nini kuniita mwema? hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu.-------Marko 10.17-18

Tafsiri kubwa kabisa ya Biblia iitwayo The Interpreter's Bible inasema kuwa kauli hiyo ya Yesu, yaani: "Kwa nini kuniiita mwema? hakuna aliye mwema ila mmoja, ndiye Mungu", imewatatiza wataalamu wa thiolojia (ilimu ya Ungu) ya Kikristo wa baadaye.

Wameona taabu kuambatisha maneno haya yalio wazi na imani yao kuwa Yesu ni mungu, na hali hapo dhaahiri yake ni kuwa anakataa uungu. Kwa hivyo basi kujitoa kimasomaso ikaandikwa katika Injili ya Mathayo (ambayo iliandikwa baada ya Marko) kwa njia nyengine.

Ilivyoandikwa katika Mathayo ni hivi:

Na tazama, mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu, nitende jambo gani jema, ili nipate uzima wa milele? Akamwambia, Kwani kuniuliza habari ya wema? Aliye mwema ni mmoja.----Mathayo 19.16-17

Kila imani ilipozidi kugeuka maandiko mapya yaliandikwa na kunasibishiwa Yesu.

Kitabu hicho The Interpreter's Bible kinaikataa tafsiri ya kusema kuwa makusudio ya Yesu yalikuwa ni kusema: Kama unanita mwema, basi unakusudia kuwa mimi ni Mungu. Hayo siyo. Aliyokusudia Yesu kusema ni kuwa :Sifai kupewa sifa za Mungu.

Mtaalamu wa Biblia wa Kitaliana, Marcello Craveri, ameandika katika kitabu chake The Life of Jesus (Maisha ya Yesu):

"Yesu kwa mara moja alimpa somo zuri kabisa la unyenyekevu, ambalo juu ya mengineyo, ni ushahidi ulio wazi ya kwamba hakupata kabisa kujiona mwenyewe ni sawa na Mungu: Kwa nini kuniita mwema? Hakuna mwema ila mmoja, ndiye Mungu."

Muhtasari wa yote , ni kuwa tumepata uthibitisho wa kutosha kutokana na Biblia kuwa Yesu wa Nazareti ni mwanaadamu, Nabii wa Mungu, na Mtume wake.
 
Katika hio mistari niliokupa utaona petro mtume akiambiwa asimdharau yoyote bali awe Karibu hata na watu walioonekana wachafu,,pili hata mwanamke alieambiwa chakula cha watoto hawapewi mbwa baada ya kujinyenyekesha alipokea baraka yake na mwanae akaponywa.

YESU sio mtume labda unionyeshe popote pale kwenye biblia.
Wala sio nabiii kamwe,,

YESU ni mwana wa MUNGU.Na njia sahihi ya kufika mbinguni.

Ukristo tuuonao na ulioenea ulimwenguni sio Ukristo aliofundisha Yesu.

Wa Yesu ulitoweka na mwenyewe na wafuasi wake wa mwanzo wa kabila la Kiyahudi.

Paulo kaufuja Ukristo.

Kauli zinazonukuliwa kwa kudai kuwa ni ushahidi kuwa Yesu mwenyewe alitaka mafunzo yake yakafundishwe kwa ulimwengu wote yamo katika Injili ya Mathayo 28.19-20, Injili ya Luka 24.46-49 na Marko 16.15.

Mathayo inasema: Basi, enendeni, mkwafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.----Mathayo 28.19-20

Luka anatwambia:

(Yesu) akwaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Na tazama, naweletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kueni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.----Luka 24.46-49

Na Injili ya Marko inasema:

(Yesu) akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.--Marko 16.15

Je, imekuwaje?

Yesu ni kigeugeu?

Mbona huku anawakataza wanafunzi wake wasende kuwahubiria ila kabila kumi na mbili za Israili, na huku anawaambia nendeni kuwahubiria Injili ulimwengu mzima.

La, Yesu si mbabaishi, wala si kigeugeu.

Hebu natuziangalie vilivyo hizo amri mbili, moja ya kuwa mafunzo yake wasifunzwe ila wana wa Israili tu, na ya pili ni hii ya kuwa watu wote wafunzwe dini.

Vipande vyote vitatu tulivyonukulu mwishoni havitaji mambo ya Yesu alipokuwa na maisha yake ya uhai wa kidunia, lakini vyaeleza mambo yaliyotukia baada ya "kufufuka kutoka wafu" kama inavyosimuliwa na Injili zote tatu.

Yajuulikana kuwa Injili ya mwanzo kuandikwa ni Injili ya Marko.

Hizo nyingine ziliandikwa baadae, na labda ujuzi wao ulitegemea hiyo hiyo Injili ya Marko.

Yajuulikana vile vile kuwa maneno yote yaliyohusu kufufuka Yesu kutokana na wafu, pamoja na hayo maamrisho ya kwenda kuihubiri Injili "kwa kila kiumbe", kinyume na maamrisho yake yote ya kuwa asihubiriwe ila Muisraeli tu - maneno hayo yote hayakuwamo katik Marko ya asili, bali yaliongezwa baadae.

Encyclopaedia Brittanica, nakla ya 11, jalada 17, sahifa 730, yasema ya kuwa kipande chote hicho kiliongezwa baadae, yamkini mwanzo mwanzo wa karne ya pili, kuchukua maneno yaliyopotea, au yaliyoonekana kuwa ni mapungufu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom