Wewe na wenye mawazo kwamba Yesu alilaaniwa, tunawaombea dhambi hiyo ifutike kwa kuwa mnawaza kibinadamu. Na haipendezi kuleta ubishi wa kidini, kwa kuwa nguzo kuu ni IMANI.
Yesu kuzaliwa kwake, maisha yake na kifo chake kilitabiriwa mapema, kama baadhi yetu humu walivyonukuu vifungu vya Biblia. Kosa lao kubwa ni kutafsiri hayo maandiko kibinadamu.
Pamoja na upendo wa Mungu kuwatuma manabii, ikiwamo Muhammad, binadamu aliendelea kuwa mdhambi na ndipo akamtuma Yesu mwanae (nabii mkuu wa mwisho) kuwakomboa binadamu kwenye minyororo ya dhambi (shetani).
Kifo cha Yesu ndivyo Mungu alipenda iwe, kuwakumbusha binadamu kwamba ukifanya dhambi utaadhibiwa. Na adhabu kubwa, inayotisha binadamu, ni mauti.