Wana wa Mungu aliye hai,thread hii imejaa upotoshaji,ni vigumu sana kuleta maswali ya kwenye mijadala ya dini then wewe uwe unajibu kwa kuandika.
Mleta mada ananikumbusha miaka ya 90,"Yahaya mpe miki",kuna mambo ameandika ni ya kweli kwa mfano paul kuwa farisayo na kuwa alikuwa akilitesa kanisa lakini kwa kuwa kuna uongo katika maelezo yake ,logically ni uongo.Nina majibu ya maswali yake lakini ni kupoteza muda kwani tutaandika magazeti hapa.Ushauri wangu tujifunze kunyamaza.
Yesu ni Mungu,ukubali ukatae.Wengi mmekalia vitabu vya dini wenzenu tunapata updates Mungu anasema na kanisa kila wakati.Tumeona mengi,nyie huko mliko mnajua wenyewe na mungu wenu.
Angalizo kwa Christians.Hizi ni siku za mwisho,elimu za upotofu ni nyingi,ningeuacha ukristo miaka ya 90 ,lakini nilichogundua jamaa wanasoma maandiko nusu kisha wanaweka yaliyo yao.
Mteule songa mbele,Mungu akusaidie ujue haya niyasemayo ni hakika na kweli,shetani ana muda mchache sana sasa siku hizi wengi tunapoteza muda na hawa wasio amini,je roho mtakatifu anakushuhudia uwaelimishe?Tujifunze kumwomba Mungu atuongoze.Kuna watu wapo hapa kukurudisha nyuma,na kuunajisi moyo wako.
Kuwa makini hata na maneno unayowajibu je yanapendeza mbele za Mungu.Biblia ilisha sema "mambo ya imani kwake yeye asiye amini ni kama upumbavu".
Nenda kahubiri injiri mtaani na si kwa hawa wanaotaka kubishana,utapoteza nguvu zako bure na utaishia kuunajisi moyo wako.Shetani kwa kuwa amegundua wakristo wengi hawasomi neno,amekuwa akilitumia neno hilo hilo la kwenye biblia kuwapata kwa kulipotosha.Mara ya mwisho umesoma biblia yako lini?Ndugu safari ya mbinguni siyo rahisi kama ambavyo wengi wanadhani,kuikana nafsi si kitu kidogo.
Je biblia haijasema mazungumzo mabaya uhalibu tabia njema?Tuwe makini kuna mambo madogo madogo yatatukosesha mbingu kama hatutakuwa makini.
Je huwa unachelewa kazini?je unadanganya kuhusu muda unao ingia kazini?Unamkosea Mungu,tuziangalie njia zetu,hizi thread zingine ni upepo tu.