Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Yesu si Mungu, Paulo ana kesi ya kujibu

Status
Not open for further replies.
Unajua mkuu Biblia na maneno aliyoyasema Yesu ukienda kichwa kichwa utachanganyikiwa sana kwani kulisoma neno tu haitoshi inapaswa uchanganyanye na imani ndani yake na Mungu akujaalie jicho la kiroho kuyatam bua maandiko maana jinsi unavyojaribu kuyapangua maandiko kwa lugha ya kisheria utakwama na mwisho hatakuwa na mshindi bali wote mtaishia kuchanganyikiwa na Neno la Mungu litabaki kuwa imara na la kuaminiwa. Yaani hoja ya kumpambanisha Yesu na Baba kuwa nani mkuu ili kudhibitisha uungu wa Yesu au kuubatilisha ni upagani na kufuru kubwa.
Toa ufafanuzi wewe maana umeongea bila kutetea hoja wakati mimi nimekupa andiko. Yohana 14:28 linasema baba ni mkuu kuliko yesu
 
Kwahiyo kulikuwa na yesu wawili. Mwingine alikuwa mbinguni kama mungu na mwingine alikuwa duniani kama binadamu. Maana yesu alivyokuwa duniani bado alikuwa tegemezi kwa mwingine mfano kwenye

Mathayo 27:45-47

Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa, nchi yote ikawa katika giza. 46 Mnamo saa tisa Yesu akalia kwa sauti kubwa, "Eli, Eli, lema sabakthani?" Maana yake, "Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?"
Maneno aliyoyasema Yesu ni maneno yalisemwa na Daudi katika zaburi alikuwa akiimba zaburi. BIBLIA inasema Mungu alikuwa ndani ya Yesu akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake. Rejea ataitwa Emmanuel yaani Mungu pamojq nasi.
 
Kwani andiko linasema alisikilizwa kitu gani? Na pia linasema kwanini alisikilizwa?
Andiko linasema "yeye katika siku hizo za mwili alimtolea yule awezaye kumuokoa na kumtoa katika mauti,maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi,akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu.

Inamaana alimtolea Mungu vitu hivyo hapo juu, machozi,dua.

Akasikilizwa tu, sababu ni mcha Mungu.
 
Toa ufafanuzi wewe maana umeongea bila kutetea hoja wakati mimi nimekupa andiko. Yohana 14:28 linasema baba ni mkuu kuliko yesu
Na pale anaposema mimi na Baba tu umoja?. Pia Tomaso alipomwambia tuoneshe Baba yatutosha Yesu alijibu nini?. Umemwona na anayesema naye ndiye Tomaso akasujudu akasema Bwana wangu na Mungu wangu.

Ninasema Biblia ukiiisoma ili idhibitishe mawazo yako itafanya hiyo kazi na utaishia kuwa mkavu kwa mambo ya kimungu.
 
Hili kweli hili zigo watu wamebebeshwa yaani Yesu ni Mungu !!! Daah jamani hivi hata gwajima ndivyo anavyoamini hivyo daah hawa jamii wamepotea
Kwani mkuu kuna tatizo????

Huu mzigo ni mwepesi sana kwetu, kuliko ule wa mtu kuja kutoka pangoni na kutwambia amepewa kitabu na malaika[emoji22] [emoji22] [emoji22] [emoji22] .

Hii mimi siikubari hata iweje.
 
Jina lako ni Rangimoto, rangi ikipata moto mara nyingi ulipuka au inaongeza kasi ya moto kwa kasi kubwa sana. Pili moto ni kitu cha hatari, hakipaswi kusogerewa hasa moto ulio waka kutokana na rangi.

Dotto short yake Doo, Doo maana yake mlango. Mlango ni sehemu ya kupitia. Dotto Rangimoto maana yake ni MLANGO WA KUINGIA KWENYE MOTO.

Tafakarini sana maana hakuna mtu ambae yupo sahihi. Na ukifatana na mtu ambae hayupo sahihi, tegemea kesho wewe kutokuwa sahihi.
 
Na pale anaposema mimi na Baba tu umoja?. Pia Tomaso alipomwambia tuoneshe Baba yatutosha Yesu alijibu nini?. Umemwona na anayesema naye ndiye Tomaso akasujudu akasema Bwana wangu na Mungu wangu. Ninasema Biblia ukiiisoma ili idhibitishe mawazo yako itafanya hiyo kazi na utaishia kuwa mkavu kwa mambo ya kimungu.
Mkuu usitumie ujuzi wajuu sana kuwaelewesha hawa watawehuka, nenda nao taratibu.
 
Maneno aliyoyasema Yesu ni maneno yalisemwa na Daudi katika zaburi alikuwa akiimba zaburi. BIBLIA inasema Mungu alikuwa ndani ya Yesu akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake. Rejea ataitwa Emmanuel yaani Mungu pamojq nasi.
kwanini usiseme tu kuwa waandishi walikopi hiyo sentensi kutoka kitabu cha zaburi?.

Pia yesu hakupatwa kuitwa Emanuel,kwahiyo hayo maneno ya isaya hayahusiani na yesu japo walijaribu kufanya spinning ili ionekane isaya alitabiri kuja kwa yesu
 
Naona unaanza kuandika tu chochote, baada ya kuona hutaweza kuelewa.
 
Aisee mnachekesha sana mara spinning mara ooh ilitungwa na watu mara Yesu sio Mungu . shauri yenu uvumilivu wa Mungu ni wote muifikie toba muepuke moto wa jehanum aliowekewa shetani na watu wake kuzimu.

Ndugu usiwe mmoja wao. Kuwa mmoja wa kondoo.
 
Maneno aliyoyasema Yesu ni maneno yalisemwa na Daudi katika zaburi alikuwa akiimba zaburi. BIBLIA inasema Mungu alikuwa ndani ya Yesu akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake. Rejea ataitwa Emmanuel yaani Mungu pamojq nasi.
Umeona sasa? Mungu alikuwa ndani ya yesu na sio kwamba Mungu alikuwa ni yesu na sio kwamba yesu alikuwa ni Mungu. Mungu kuwa ndani ya yesu inamaanisha kuwa yesu alikuwa anafanya vitu kutoka kwa muongozo wa Mungu na sio kwa uwezo wake.

Yohana 5:30-33

Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
31 Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.
32 Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli.
33 Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akaishuhudia kweli.
 
Naona unaanza kuandika tu chochote, baada ya kuona hutaweza kuelewa.
nina ushahidi mkuu,hayo maneno ,"eloh eloh lamasabaktan "yamechukuliwa toka zaburi na inatia wasiwasi kama kweli yesu aliyatamka,kwani waandishi wanapishana,
mmoja anadai kabla yesu hajakata roho alitamka ," eloh eloh.....,kisha akakata roho.

Mwandishi mwingine anasema,yesu alitamka ,"IMEKWISHA",kisha akakata roho,

mwandishi wa tatu anadai yesu alisema,"baba yangu roho yangu naikabidhi kwako",kisha akakata roho,

so nani yuko sahihi hapo,

pia uelewe copy za aina hiyo toka agano la kale kuja jipya zipo
 
Umeona sasa? Mungu alikuwa ndani ya yesu na sio kwamba Mungu alikuwa ni yesu na sio kwamba yesu alikuwa ni Mungu. Mungu kuwa ndani ya yesu inamaanisha kuwa yesu alikuwa anafanya vitu kutoka kwa muongozo wa Mungu na sio kwa uwezo wake.

Unakataa nini unakubali nini mkuu????

Sasa kwa mantiki hiyo hapo juu, nikuulize swali fikirishi-"yesu alizaliwa akiwa na UMungu ndani yake au au alizaliwa UMungu akaukuta?????

Yohana 5:30-33

Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
31 Mimi nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.
32 Yuko mwingine anayenishuhudia; nami najua ya kuwa ushuhuda wake anaonishuhudia ni kweli.
33 Ninyi mlituma watu kwa Yohana, naye akaishuhudia kweli.
 
nina ushahidi mkuu,hayo maneno ,"eloh eloh lamasabaktan "yamechukuliwa toka zaburi na inatia wasiwasi kama kweli yesu aliyatamka,kwani waandishi wanapishana,
mmoja anadai kabla yesu hajakata roho alitamka ," eloh eloh.....,kisha akakata roho.

Mwandishi mwingine anasema,yesu alitamka ,"IMEKWISHA",kisha akakata roho,

mwandishi wa tatu anadai yesu alisema,"baba yangu roho yangu naikabidhi kwako",kisha akakata roho,

so nani yuko sahihi hapo,

pia uelewe copy za aina hiyo toka agano la kale kuja jipya zipo
Embu fanya ulete hapa.
 
Paulo anaweza kua sawa tu,kwa MUNGU yote yawezekana kama alivyoweza kumtengeneza popo.wengine wanamuita ndege na wengine humwita mnyama.yamkini YESU alikua BINADAMU na MUNGU pia
NIAMBIE WW KAMA YESU AWEZA KUWA BINAADAMU NA MUNGU PIA;JE MUNGU AKIFA NANI ATAIENDESHA DUNIA.........? MAANA TUNAAMINI KTK IMANI YA UISLAMU , MUNGU NI UWEZO UNAOWEZA USIWEZWA........!, HAKUZAA, WALA HAKUZALIWA, HALI WALA HANYWI, YESU ALIKUWA AKILA AKILALA USINGIZI NA MENGINEYO KAMA BINAADAMU, kimaumbile ukila ukinywa lazima utaenda choo, je unaamini kweli mungu anaenda chooni.......?
 
Vitabu vya dini vinachanganya sana..nadhan biblia imesema katika kitabu cha mwanzo "natumuumbe mtu kwa mfano wetu" kwa uelewa wangu mdogo sentesi hii inamaanisha Mungu ni Mtu na ndo mana akaumba kiumbe MTU kwa mfano wake..! Lakini kwenye biblia hiyo hiyo kuna maelezo kuwa Mungu hashikiki, haonekani, hanusiki na yupo kila mahala..! Kwa maelezo haya Mungu anakosa sifa za MTU wa kawaida..!
 
NIAMBIE WW KAMA YESU AWEZA KUWA BINAADAMU NA MUNGU PIA;JE MUNGU AKIFA NANI ATAIENDESHA DUNIA.........? MAANA TUNAAMINI KTK IMANI YA UISLAMU , MUNGU NI UWEZO UNAOWEZA USIWEZWA........!, HAKUZAA, WALA HAKUZALIWA, HALI WALA HANYWI, YESU ALIKUWA AKILA AKILALA USINGIZI NA MENGINEYO KAMA BINAADAMU, kimaumbile ukila ukinywa lazima utaenda choo, je unaamini kweli mungu anaenda chooni.......?

Uislamu wako na ukristo ni dini tofauti, ukitafuta reference za bible kwenye uislamu lazima utachanganyikiwa.
 
Vitabu vya dini vinachanganya sana..nadhan biblia imesema katika kitabu cha mwanzo "natumuumbe mtu kwa mfano wetu" kwa uelewa wangu mdogo sentesi hii inamaanisha Mungu ni Mtu na ndo mana akaumba kiumbe MTU kwa mfano wake..! Lakini kwenye biblia hiyo hiyo kuna maelezo kuwa Mungu hashikiki,haonekani,hanusiki na yupo kila mahala..! Kwa maelezo haya Mungu anakosa sifa za MTU wa kawaida..!
Natumuumbe mtu kwa mfano wetu hakukumaanisha kuwa Mungu ana umba mtu kwa jinsi alivyo yeye bali Mungu ana umba mtu kwa namna maalumu aitakayo yeye mwenyewe. ni lugha ya mafumbo
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom