Yetkin Gen Mehmen, Meneja wa Yapi Merkezi, kampuni inayojenga SGR ahukumiwa Kisutu

Yetkin Gen Mehmen, Meneja wa Yapi Merkezi, kampuni inayojenga SGR ahukumiwa Kisutu

Hii kesi mbona imetolewa maamuzi ndani ya muda mfupi hivi!!? Hakukuwa na mambo ya uchunguzi haujakamilika wala nini, kuna kitu hapo si bure.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kesi ikichukua muda mrefu mnalalamika kwamba kucheleweshwa kwa haki ni kumnyima mtu haki yake. Kesi ikiendeshwa haraka bado mnalalamika. Mtu ameshikwa na pesa kinachozidi kiwango kinachoruhusiwa.

Ushahidi kamili ni hizo fedha zenyewe. Sasa unataka kesi ichukue miezi mingapi na kwa sababu zipi kwa kuwa ushahidi upo hapo tayari kwamba fedha zilikuwa kiasi kadhaa ambacho kinazidi kiwango kinachoruhusiwa?

Kesi zote lazima ziendeshwe hivi na tulalamikie zile tunazoona zinazidi 'reasonable time' ya kufanya uchunguzi.
 
Pesa walizotaifisha zenyewe ni nyingi sana kuliko hizo wanazotaka alipe faini, naamini hakuna haki kabisa basi tu hizi zote ni hujuma, sas kama mtu ni manager wa kampuni inayojenga SGR pesa hizo kuwa nazo ni kitu gani kwani mbona fikra za kimaskini zinatutesa sana wabongoo ? hata kama ningekuwa mm wanikute na pesa ziwezi kuanza kutolea maelezo yeyote .
expand...Acha kuongea usichokijua! Tembea nchi yoyote kabla ya kuingia au kutoka uhamiaji katika viwanja vya ndege lazima utolee maelezo kiasi cha fedha ulichonacho vinginevyo zinataifishwa kama ni kikubwa kuliko kiwango kinachoruhusiwa
 
Acha kuongea usichokijua! Tembea nchi yoyote kabla ya kuingia au kutoka uhamiaji katika viwanja vya ndege lazima utolee maelezo kiasi cha fedha ulichonacho vinginevyo zinataifishwa kama ni kikubwa kuliko kiwango kinachoruhusiwa
Afrika ya Kusini nimeingia wanakuuliza kuthibitisha kama una pesa usijekuwa ni Mhamiaji haramu; kama huna pesa unakuwa deported back.
 
Bado haiingii akilini.. Mnafahamu kabisa ni manager wa kampuni kubwa mlioipa tenda ya SGR, sasa kuna ajabu gani kumkuta na hizo fedha? Na maelezo gani hasa mnayoyataka wakati mnafahamu fika ni manager wa kampuni wa kampuni kubwa na yenye tenda kubwa?

Huu ni udictator wa wazi kabisa..


Sent from my iPhone using JamiiForums


Mzee hii dunia inautaratibu pesa ikizid Dola 10k lazima useme kwann unatembea Nazi na usiweke bank hyo n kuzuia biashara haramu Kama drugs, human trafficking, na mengine pia unaeza kwenda tuseme South Africa unakila documents zinazokuruhusu kwenda huko Sasa lile lengo uliloliandika unaenda kulifanya ukiwa ushatua airport unaeza ulizwa maswali na migration officer pale airport ukishndwa kujibu kiusahihi mzee unarud kwenu.

Mfano umetua botwana karatasi ibaonyesha unaenda kula maisha unaulizwa umebeba kiasi gan unawaambia wanakwambia tuonyeshe Kama una mzigo mdogo kucompare na maisha yahuo mji hapohapo unaambiwa subiri flight inayofata ya kurud ulipotoka
 
Pesa walizotaifisha zenyewe ni nyingi sana kuliko hizo wanazotaka alipe faini, naamini hakuna haki kabisa basi tu hizi zote ni hujuma, sas kama mtu ni manager wa kampuni inayojenga SGR pesa hizo kuwa nazo ni kitu gani kwani mbona fikra za kimaskini zinatutesa sana wabongoo ? hata kama ningekuwa mm wanikute na pesa ziwezi kuanza kutolea maelezo yeyote .
sio roho za kimaskini ni sheria inasema hivyo
 
Kuna siku nilienda pale bureau de change ya mwanza hotel kubadilisha fedha... Ilikuwa jumapili... Akaja jamaa fulani mbabambaba hivi kubadilisha fedha....Mimi nikabadilisha zangu nikatulia kando kuzihesabu akaingia jamaa... Akauliza rate akaambiwa...Akachukua kikotoo chake akapiga hesabu zake haya...Akamwambia mtoa huduma anahitaji kubadi USD 70000!!!! Ikabidi nami nitulie nisome mchezo...mtoa huduma akasema dola ngapi??

Jamaa akarudia USD 70000....ikabidi tucheke aisee.... Jamaa katoa bahasha mbili.. Akatoa zile hela...Kweli aisee...Mtoa huduma akamwambia leo weekend hatuna,uje kesho jumatatu...jamaa akachukua pesa zake akasema poa.... Ila jamaa alikuwa wa kawaida sana kama wale wanaofanya kazi za nguvunguvu mjini... Nikaamini tembea uone.
 
Kuna sheria zingine zakipumbavu sanaaaa, mtu hela yake afu bdo mnambania

House girl(dada wa kazi) Ni binadamu aheshimiwe, apumzike, apewe Uhuru wa kuabudu pia
Wewe ndiyo mpumbavu sana hujui unatetea nini. Pesa yako utashindwa kuitolea maelezo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilienda pale bureau de change ya mwanza hotel kubadilisha fedha... Ilikuwa jumapili... Akaja jamaa fulani mbabambaba hivi kubadilisha fedha....Mimi nikabadilisha zangu nikatulia kando kuzihesabu akaingia jamaa... Akauliza rate akaambiwa...Akachukua kikotoo chake akapiga hesabu zake haya...Akamwambia mtoa huduma anahitaji kubadi USD 70000!!!! Ikabidi nami nitulie nisome mchezo...mtoa huduma akasema dola ngapi?? Jamaa akarudia USD 70000....ikabidi tucheke aisee.... Jamaa katoa bahasha mbili.. Akatoa zile hela...Kweli aisee...Mtoa huduma akamwambia leo weekend hatuna,uje kesho jumatatu...jamaa akachukua pesa zake akasema poa.... Ila jamaa alikuwa wa kawaida sana kama wale wanaofanya kazi za nguvunguvu mjini... Nikaamini tembea uone.
Mwenye akili timamu hawezi kubadilisha kiwango hicho cha fedha yaani million 163? Kwanza ukizibadili utazipeleka wapi kwani Benki mwisho wa siku utatakiwa uzitolee maelezo!
 
Serikali ina kazi kubwa sana kuelimisha Watanzania, hadi leo mtu hajui kupanda ndege na pesa zote hizo ni uhalifu, ulaya hata kutuma pesa za matumiz africa kuna limit sio unajitumia tu
 
Mambo mengine kama huna ufahamu bora unyamaze. Hizo hela ni sawa na million 200 za kitanzania. Unawezaje kuwa na cash kubwa hiyo mkononi kama sio kwa ajiri ya uhalifu? Kisheria za kibenki za Tanzania ukitaka kutoa (withdraw) kiasi cha million 10 lazima BoT ifahamishwe na lazima hiyo account iwe inayoeleweka vinginevyo utasubirishwa saana uku wakikuchunguza. Sasa RAIA wa kigeni kuwa na hela kubwa hiyo ya kigeni cash uwanja wa ndege ni uhalifu na unahatarisha usalama wa taifa. Nenda nchi yoyote duniani labla ya kuingia au kutoka lazima utolee maelezo kiasi cha fedha ulichonacho na uhalali vinginevyo zinataifishwa!

Alikuwa anaingia au anatoka nchini Tz?
 
Kwanza saiz na hiki kitambulisho Cha nida kilivyokuja Mambo yatakuwa magumu Sana hasa kwa wapigaji kwenye kufanya transaction au kusafiri Mana lazima ukitoe namba iandikwe Yan baada ya uchaguzi Mambo ya pesa za mpango wa kando zitakuwa ngumu Sana kuzifanya ziwe Safi japo tutazoea
 
Mwenye akili timamu hawezi kubadilisha kiwango hicho cha fedha yaani million 163? Kwanza ukizibadili utazipeleka wapi kwani Benki mwisho wa siku utatakiwa uzitolee maelezo!
Na ndiyo kilichonifanya nitulie nione picha litakuwaje kama atabadilishiwa au la....Hilo la kutunza benki sikulifikiria yawezekana alihitaji azitumie.
 
Bado haiingii akilini.. Mnafahamu kabisa ni manager wa kampuni kubwa mlioipa tenda ya SGR, sasa kuna ajabu gani kumkuta na hizo fedha? Na maelezo gani hasa mnayoyataka wakati mnafahamu fika ni manager wa kampuni wa kampuni kubwa na yenye tenda kubwa?

Huu ni udictator wa wazi kabisa..


Sent from my iPhone using JamiiForums
Ni kweli ameviolate sheria. Kwamba ukitaka kusafiri na $10k au zaidi lazima utoe taarifa.

Ila hiyo sheria ni ya kipumbavu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom