secret file
JF-Expert Member
- Sep 10, 2019
- 5,843
- 8,637
Umekariri wenye hela ni wavaa suti....Kuna siku nilienda pale bureau de change ya mwanza hotel kubadilisha fedha... Ilikuwa jumapili... Akaja jamaa fulani mbabambaba hivi kubadilisha fedha....Mimi nikabadilisha zangu nikatulia kando kuzihesabu akaingia jamaa... Akauliza rate akaambiwa...Akachukua kikotoo chake akapiga hesabu zake haya...Akamwambia mtoa huduma anahitaji kubadi USD 70000!!!! Ikabidi nami nitulie nisome mchezo...mtoa huduma akasema dola ngapi?? Jamaa akarudia USD 70000....ikabidi tucheke aisee.... Jamaa katoa bahasha mbili.. Akatoa zile hela...Kweli aisee...Mtoa huduma akamwambia leo weekend hatuna,uje kesho jumatatu...jamaa akachukua pesa zake akasema poa.... Ila jamaa alikuwa wa kawaida sana kama wale wanaofanya kazi za nguvunguvu mjini... Nikaamini tembea uone.
njoo kilingeni kwetu tunavaa kobasi na kaptura..
lkn watu wana hela za kununulia dreemliner...