Yondo Kusala Denise (Yondo Sister), JamiiForums tunakupa heshima zako na tunauthamini mchango wako, hatuna tuzo, ila tuna uzi wako

Mkuu heshima yako
 
Naaam muziki wake ulituburudisha haswa.
Indeed Mungu amjalie Afya Njema
 
Lutu Mabangu ametajwa na Extra musica kwenye albamu ya Etat Major, ule wimbo wa "La pluie" ulotungwa na Roga roga[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91], nlijua tu Lutu Mabangu atakua mtu mzito.
 
Asante sana Buji... Hawa ndio wanamuziki wa ujana wetu.. Huyu mwanadada alitusababishia sana ndoto nyevu na wimbo wake wa Mbuta mutu

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].......nilikuwa napiga hesabu amenizidi miongo miwili na ushee, lakini hata mimi miaka hiyo ya 90 nilikuwa naweweseka sana juu yake [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Ule muuno wake ulikuwa siyo wa Dunia hii
 
Wacongoman wako juu sana kwenye muziki. Enzi za miaka ya 1990's, muziki wa Kikongo ulikuwa ndiyo moto wa kuotea mbali.

Enzi hizo kuna akina Pepe Kale, Bozi Boziana, Yondo Sister, Aulus Mabere, Allain Koukou, Diblo Dibala, Dally Kimoko, Ngouma Lokito, Wenge BCBG, Extra Musica, Koffi Olomide, Lucien Bokilo, General Defao, Mbuta Likasu, na wengineo wengi!! Hakika vijana wa wakati huo tulifaidi sana zile video za chongo na ile mikanda yake.

By the way, Yondo Sister anaishi Ufaransa. Na siyo Congo. Kuna wakati aliwahi kuhojiwa na mtangazaji wa RFA (Zuberi Msabaha RIP). Jambo la kufurahisha, anaweza pia kuongea Kiswahili ingawa ni kile cha kuokoteza maneno. Alibahatika pia kuwa na mtoto mmoja tu wa kike, ambaye pia amerithi kipaji chake.
 
Hata kwenye soka. Congo DRC sio tajiri tu wa rasilimali, hadi vipaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…