Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
- Thread starter
- #41
Long timeHalafu zikiishiwa chaji zinaanikwa juani ama kupigwa pigwa nyundo ili zipate chaji 😂😂
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Long timeHalafu zikiishiwa chaji zinaanikwa juani ama kupigwa pigwa nyundo ili zipate chaji 😂😂
Hivi alikua mchaga au ni mpare
Mkuu heshima yakoAiseee hatari sana enzi zile. Nakumbuka those days back, ninasoma Mbeya, nimekata tiketi ya kwenda Mwanza, basi la Subira la kanisa Katoliki Mbeya.
Lami enzi hizo inaishia Isanga, haifiki hata Kawetere. Barabara vumbi balaa, yaanibukiiangalia barabara unaiona iko very smooth, ukiingiza mguu ni vumbi tupu, hadi pajani ndipo uikute sakafu ya barabara.
Basi kuanzia Mbeya hadi Tabora tulipigiwa kanda moja tu, YONDO SISTER album Deviation.
Hakika ni miongoni mwa siku zangu bora kabisa za kukumbukwa. Ilikuwa September mwaka 1994.
Naaam muziki wake ulituburudisha haswa.View attachment 2702740
Yondo Kusala Denise (amezaliwa tar. 1 Januari 1958) ambaye anajulikana zaidi kwa jina la kisanii kama Yondo Sister, ni msanii wa Kikongo. Wengi humwita "Malkia wa Soukous", "Tina Turner" wa muziki wa dansi barani Afrika. Yondo Sister amepata kuwa mwimbaji mkuu katika bendi ya Soukous Stars kwa miaka kadhaa kabla ya kwenda kufanyakazi kama msanii wa kujitegemea. Uwezo wake wa kuimba iliibuliwa na Lutu Mabangu wakati huo Yondo akiwa kama mnenguaji wa Tabu Ley katika bendi yake ya Rocherettes. Yondo muziki uko katika damu, mzee wake alikuwa akipiga muziki kwa kujifurahisha tu, humo kukajengeka ujasiri wa kutoogopa hadhira. Na mara kadhaa alishiriki katika dansi, polepole na kuja kuwa mwanamuziki kamili na kutoa albamu ya kwanza mwaka 1991.
Yondo Sister amepata kutoa album 6 kwenye studio za Air B. Mas Production na Melodie, T.J.R. Music na zote zilikuwa moto mkali. Album hizo ni:-
FBI (2001)
Agenda (2002)
Dernière Minute(1995)
Deviation (1994)
Bazo (1991)
Planete (1990)
View attachment 2702741
Yondo Sister bado yuko hai nchini kwao Congo DRC akiendelea na shughuli za muziki.
Mungu amjalie umri mrefu wenye afya njema, furaha, amani ya moyo, ma mafanikio ya kila aina na ya kila rangi.
Mshana Jr , Pascal Mayalla, Elli
[emoji1787][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].......nilikuwa napiga hesabu amenizidi miongo miwili na ushee, lakini hata mimi miaka hiyo ya 90 nilikuwa naweweseka sana juu yake [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Asante sana Buji... Hawa ndio wanamuziki wa ujana wetu.. Huyu mwanadada alitusababishia sana ndoto nyevu na wimbo wake wa Mbuta mutu
Sent using Jamii Forums mobile app
AminaNaaam muziki wake ulituburudisha haswa.
Indeed Mungu amjalie Afya Njema
Marioooooooooooooooooooo[emoji1787][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].......nilikuwa napiga hesabu amenizidi miongo miwili na ushee, lakini hata mimi miaka hiyo ya 90 nilikuwa naweweseka sana juu yake [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
You are the legendLutu Mabangu ametajwa na Extra musica kwenye albamu ya Etat Major, ule wimbo wa "La pluie" ulotungwa na Roga roga[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91], nlijua tu Lutu Mabangu atakua mtu mzito.
Ule muuno wake ulikuwa siyo wa Dunia hiiView attachment 2702740
Yondo Kusala Denise (amezaliwa tar. 1 Januari 1958) ambaye anajulikana zaidi kwa jina la kisanii kama Yondo Sister, ni msanii wa Kikongo. Wengi humwita "Malkia wa Soukous", "Tina Turner" wa muziki wa dansi barani Afrika. Yondo Sister amepata kuwa mwimbaji mkuu katika bendi ya Soukous Stars kwa miaka kadhaa kabla ya kwenda kufanyakazi kama msanii wa kujitegemea. Uwezo wake wa kuimba iliibuliwa na Lutu Mabangu wakati huo Yondo akiwa kama mnenguaji wa Tabu Ley katika bendi yake ya Rocherettes. Yondo muziki uko katika damu, mzee wake alikuwa akipiga muziki kwa kujifurahisha tu, humo kukajengeka ujasiri wa kutoogopa hadhira. Na mara kadhaa alishiriki katika dansi, polepole na kuja kuwa mwanamuziki kamili na kutoa albamu ya kwanza mwaka 1991.
Yondo Sister amepata kutoa album 6 kwenye studio za Air B. Mas Production na Melodie, T.J.R. Music na zote zilikuwa moto mkali. Album hizo ni:-
FBI (2001)
Agenda (2002)
Dernière Minute(1995)
Deviation (1994)
Bazo (1991)
Planete (1990)
View attachment 2702741
Yondo Sister bado yuko hai nchini kwao Congo DRC akiendelea na shughuli za muziki.
Mungu amjalie umri mrefu wenye afya njema, furaha, amani ya moyo, ma mafanikio ya kila aina na ya kila rangi.
Mshana Jr , Pascal Mayalla, Elli
[emoji28][emoji28][emoji1787][emoji1787]Marioooooooooooooooooooo
Haha hahah[emoji28][emoji28][emoji1787][emoji1787]
Aisee ni moto zaidi ya moto wa gesiUkitaka kuja balaa LA huyu mama kasikilize Ngoma kama Mbuta Mutu Bazu Wapi Yo ndio utajua ana balaa
Hata kwenye soka. Congo DRC sio tajiri tu wa rasilimali, hadi vipajiWacongoman wako juu sana kwenye muziki. Enzi za miaka ya 1990's, muziki wa Kikongo ulikuwa ndiyo moto wa kuotea mbali.
Enzi hizo kuna akina Pepe Kale, Bozi Boziana, Yondo Sister, Aulus Mabere, Allain Koukou, Diblo Dibala, Dally Kimoko, Ngouma Lokito, Wenge BCBG, Extra Musica, Koffi Olomide, Lucien Bokilo, General Defao, Mbuta Likasu, na wengineo wengi!! Hakika vijana wa wakati huo tulifaidi sana zile video za chongo na ile mikanda yake.
By the way, Yondo Sister anaishi Ufaransa. Na siyo Congo. Kuna wakati aliwahi kuhojiwa na mtangazaji wa RFA (Zuberi Msabaha RIP). Jambo la kufurahisha, anaweza pia kuongea Kiswahili ingawa ni kile cha kuokoteza maneno. Alibahatika pia kuwa na mtoto mmoja tu wa kike, ambaye pia amerithi kipaji chake.