Yoshua - Amiri jeshi mkuu wa kwanza wa waisrael

Yoshua - Amiri jeshi mkuu wa kwanza wa waisrael

Kizuio

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
845
Reaction score
521
Yoshua ni kiongozi wa taifa la Israeli linalojulikana hasa kupitia kitabu cha sita kati ya vitabu vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na vya Agano la Kale katika Biblia ya Ukristo.

Kitabu hicho chenye sura 24 kinatupasha habari za uvamizi wa nchi takatifu ambao Waisraeli waliufanya chini ya Yoshua, ambaye ni mfano wa Yesu (hata jina lao kwa Kiyahudi ni moja, linalotafsiriwa “Mungu anaokoa”): ndiye aliyewaingiza watu katika nchi ya ahadi, si Musa.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Yoshua anaheshimiwa kama mtakatifu na Wayahudi, Wakristo na Waislamu, hasa tarehe 1 Septemba.

Mazingira yake

Kitabu cha Yoshua kinahusika zaidi na Waisraeli walipoteka nchi ya Kanaani na nchi hiyo ilivyogawiwa kati ya makabila yake. Tangu wakati wa Ibrahimu Mungu alikuwa ameahidi kwamba Kanaani ingekuwa mali ya Waisraeli (Mwa 13:14-17), lakini karne kadhaa zilipita mpaka Waisraeli walipokuwa taifa kubwa la kutosha kwa kuteka na kumiliki nchi hiyo.

Taifa la Israeli lilikua na kuongezeka hasa katika nchi ya Misri, na wakati ulipowadia, Musa aliwaongoza watu hao kutoka Misri kuelekea Kanaani (Kut 3:7-10; 12:40-41). Lakini watu walipofika karibu, ambapo wangeweza kuandaa mashambulio, waliwaogopa Wakanaani wakamwasi Mungu. Kwa ukaidi wao, watu walikataa kumtegemea Mungu na kuingia Kanaani, isipokuwa viongozi wawili, yaani Yoshua na Kalebu. Mungu akawaadhibu jangwani mpaka walipokufa watu wazima wote (waliokuwa na miaka 20 na kuzidi, isipokuwa Yoshua na Kalebu) na kizazi kipya kilipokuwa na nguvu ya kutosha (Hes 14:28-35).

Wakati huo, miaka 40 baada ya wazazi wao kuondoka Misri, watu wa kizazi kile kipya walikuwa tayari kuingia Kanaani. Kambi yao kubwa ilikuwa mashariki mwa Mto Yordani kukabili Yeriko (Hes 22:1). Musa alikuwa amekufa tangu muda mfupi (Kum 34:1-5), na Yoshua alipewa jukumu la kuwaongoza Waisraeli baada ya kifo cha Musa kwenye miaka 1210-1200 hivi KK (Kum 34:9; Yos 1:1-2).

Kiongozi mpya wa Israeli shupavu

Yoshua alizaliwa na kukulia Misri, lakini miaka ya taabu huko ilimsaidia kujenga tabia, uwezo na imani ya kumtegemea Mungu ambayo siku moja itamfanya awe mtu wa maana sana katika taifa lake.

Muda mfupi baada ya Waisraeli kuondoka Misri, Yoshua alionyesha uwezo wake wa kuongoza alipokusanya kwa haraka sana jeshi dogo na kuwafukuza wachokozi Waamaleki (Kut 17:8-16).

Waisraeli walipofika Mlima Sinai, Yoshua alikuwa msaidizi maalumu wa Musa. Yeye peke yake alifuatana naye alipokwea mlima, ambapo Musa alikutana na Mungu katika wingu, lakini Yoshua alibaki nje (Kut 24:13).

Vile vile Yoshua hakutoka katika hema ambamo Musa alikutana na Mungu (Kut 33:11; taz. Hes 11:28).

Siku moja, Waisraeli walipomwasi Mungu jangwani, Yoshua alionyesha imani yake yenye ujasiri ambapo yeye na Kalebu walisimama imara kinyume cha wenzao wote (Hes 14:9).

Imani yake ya kumtegemea Mungu ilimpa uvumilivu na kumlinda asije akachukuliwa na tamaa ya ubinafsi ya kutaka makuu. Hakuwa na kijicho dhidi ya Musa kuwa kiongozi wa Israeli, bali alijaribu kumtetea watu wengine walipojaribu kushambulia daraja yake ya pekee (Hes 11:26-30).

Mungu alimchagua Yoshua awe kiongozi wa taifa baada ya Musa, lakini alionyesha wazi kwamba Yoshua asingekuwa na mamlaka kubwa sawa sawa na Musa, kwa kuwa baada ya kufa kwake, uongozi wa kiraia na ule wa kiroho ukawa juu ya watu tofauti. Tangu wakati huo kawaida ilikuwa kwamba, kiongozi wa kiraia alipata maagizo ya Mungu kwa njia ya kuhani mkuu (Hes 27:18-23).

Hata hivyo, Yoshua alikuwa mtu aliyemwelewa Mungu. Uzoefu wake kama kiongozi wa kiroho, mtawala wa kiraia na mkuu wa jeshi ulimfaa sana kuwaongoza Waisraeli katika nchi yao mpya na katika wakati mpya uliowakabili (Kum 31:7, 14, 23; 34:9).

Mtindo wa Kitabu cha Yoshua Edit

Kitabu cha Yoshua kimepata jina lake kutokana na mtu ambaye habari zake zimesimuliwa zaidi humo, lakini hakimtaji mwandishi wake.

Inawezekana kwamba mwandishi alipata habari kutokana na kumbukumbu ambazo Yoshua mwenyewe aliziandika (Yos 24:25-26) na vitabu vingine vya historia vya wakati ule (Yos 10:13) na ripoti za kikabila na za kitaifa kuhusu mahali, koo na matukio mbalimbali (Yos 18:8-9).

Ingawa kitabu kinaeleza utekaji wa nchi ya Kanaani, hakitoi orodha ya kinaganaga kuhusu matukio yote ya historia. Vita vya kuteka Kanaani vilichukua muda mrefu (Yos 11:18) usiopungua miaka mitano (Yos 14:7, 10), lakini mwandishi alitaja baadhi ya vita virefu katika mistari michache tu, na mambo mengine yasiyokuwa na maana sana ya kivita aliyaandika kirefu.

Sababu ya tofauti hizo katika masimulizi ni kwamba, madhumuni maalumu ya mwandishi hayakuwa kuandika kinaganaga kuhusu vita na siasa, bali alitaka kuonyesha kazi ya Mungu na watu wake. Mwandishi alikuwa mhubiri kuliko mwandishi wa ripoti na orodha mbalimbali tu. Alikuwa nabii kuliko mwandishi wa historia.

Kwa Waisraeli kazi ya kwanza ya nabii haikuwa kutabiri mambo ya usoni, bali kuwajulisha watu mapenzi ya Mungu (Isa 1:18-20; Yer 1:7,9; Amo 3:7-8; taz. Kut 4:10-16; 7:1-2). Wao waliona historia yao kama ufunuo wa matendo ya Mungu, na kwa sababu hiyo kitabu hiki na vingine kadhaa vya Biblia tunavyoviona vya historia, Waisraeli waliviita vya unabii. Waandishi wengi wa historia katika Israeli walikuwa manabii (1 Nya 29:29; 2 Nya 9:29; 12:15).

Waisraeli waligawanya vitabu vyao vya unabii katika sehemu mbili zilizoitwa Vitabu vya Unabii wa Awali (Yoshua, Waamuzi, Samweli na Wafalme), na Vitabu vya Unabii wa Baadaye (Isaya, Yeremia, Ezekieli na vitabu 12 vya manabii wadogo). Katika vitabu vya Unabii wa Awali, Mungu alidhihirisha makusudi yake kwa njia ya historia ya Waisraeli, na kwa kweli mataifa yote yalikuwa chini ya utawala wake mkuu. Katika vitabu vya Unabii wa Baadaye, Mungu alidhihirisha makusudi yake zaidi kwa njia ya maneno ya wasemaji wake.

Kwa sababu ya namna hiyo ya pekee ya Waisraeli kutazama historia, mwandishi wa kitabu cha Yoshua hakujaribu kuorodhesha kila tukio lililotokea wakati ule, wala hakuandika katika utaratibu maalumu wa mfululizo wa matukio. Zaidi alichagua na kupanga mambo yake kadiri ya kusudi lake kuu la unabii. Alitaka kuwasaidia watu wamjue Mungu zaidi, akishughulika na matukio yale yaliyokuwa na maana kubwa katika uhusiano wa taifa na Mungu wake.

Habari za kitabu chenyewe kilivyo

Mara baada ya kushika uongozi, Yoshua alituma wapelelezi nchini; huko Yeriko, mji wa zamani kuliko yote ya dunia, walisaidiwa na Rahabu, kahaba aliyeamini kuwa ushindi utakuwa wa Mungu wa Israeli (Yos 2): kwa hiyo akaokolewa pamoja na ndugu zake, tena akajaliwa kuwa bibi wa babu wa mfalme Daudi, hata akatajwa na Injili kama bibi wa Yesu Kristo (Math 1:5-6), halafu akachukuliwa kama mfano wa imani (Eb 11:31) na wa matendo mema (Yak 2:25).

Kadiri ya kitabu hicho, Yoshua aliwavusha Waisraeli pakavu kati ya mto wa Yordani (Yos 3-4) na hivyo akawaingiza katika nchi takatifu. Hapo ikawabidi kwanza wafunge tena agano na Mungu kwa kutahiriwa wanaume wote na kwa kuadhimisha Pasaka ambapo kwa mara ya kwanza walikula mazao ya nchi hiyo waliyoahidiwa: ndio mwisho wa mana na wa kipindi cha jangwani (Yos 5:1-12). Hata sisi tutaacha kula mkate toka mbinguni tutakapoingia pale tulipoahidiwa.

Baada ya matendo hayo ya kidini Mungu alimtokea Yoshua kama amiri jeshi wa Israeli ili kumhakikishia kwamba mwenyewe ataongoza mambo, hivyo Yoshua amtegemee akijisikia chombo chake tu (Yos 5:13-15). Ni rahisi kwa kila binadamu aliyeshika uongozi kujisikia mwenyewe na hivyo kuacha kumtegemea Mungu. Kumbe Yoshua kwa kupokea ujumbe huo akaweza kushinda watu wenye maboma, nguvu na silaha kali kuliko Waisraeli.

Kwamba hiyo ni nguvu ya Mungu inaonekana wazi hasa katika simulizi la kuteka Yeriko (Yos 6:1-21): huko Waisraeli walifanya maandamano ya ibada mpaka kuta za mji zikaanguka. Vita vyetu vya kiroho na vya kitume vitegemee hasa sala.

Baada ya vita vingi Yoshua akayagawia makabila 12 ya Israeli nchi yote, ikiwa ni pamoja na sehemu zilizobaki chini ya wenyeji (Yos 12:1-13:14).

Huko Shekemu aliwadai wote wachague kumtumikia YHWH au miungu mingine, akisisitiza ugumu wa kumtumikia sawasawa Mungu aliye mtakatifu na mwenye wivu kwa watu wake. Lakini wao walikubali kwa moyo wote kumtumikia Mungu tu, wakasimamisha jiwe kubwa kama kumbukumbu (Yos 24:1-28).

Kabla hajafa Yoshua akawaita Waisraeli wote ili kuwaimarisha katika imani na umoja kwa kuwakumbusha maajabu waliyotendewa na Mungu na kwa kuwahimiza wamuonyeshe shukrani (Yos 23). Kukumbuka ni jambo muhimu ili tuishi kwa imani bila ya kudanganywa na maisha yanayosahaulisha kwa urahisi mambo ya Kimungu.
 
Biblia ni Tamuu mnoo usomee. Lakini ukisoma uchambuzi wa kitabu kimojakimoja historia yake kilivyoandikwa na kikapatikana It very Irritating and surprising..
Mfano.
Inasemekana (Kwa mujibu wa biblia nayotumia mimi ikiwa inaeleza historia ya kitabu kimoja kimoja) Musa alipovuka baharini na wana israel Maji yalikua yamekupwa wammisri walipopita maji yakawa yamejaa bado hawajapita.

Mapigo Kumi kwa Wamisri..
Ipo hivi Mvua ilinyesha huko juu ukateremsha matope ndani ya mto naili mto ukawa mwekundu, Wana waisrael walipoona vile wakasema kua maji ya mto yalikua damu lakini kiuharisia maji yalikua mekundu kama damuu na sio damu iljaa mtoni.
Ajili ya matope vyura vikajaa mjini kutoka ndani ya mto..
 
Mkuu hizi stori ni tamu sana kama ukiamua kuzifuatilia kwa kumsoma mtu anaetajwa katika kitabu husika

Mfano hapa nimegundua kuwa vita ya waisrael na wenyeji wa kanaan ilichukua miaka mitano na zaidi mpaka kuimiliki yote
 
Kitu kingine ni kwamba vita bila Mungu mtaishia kupigwa tu hata kama wapinzani wenu wana vifaa vya kivita vichache
 
Kingine ni kuwa waisrael baada ya kusota jangwani miaka 40 kwa kupinga amri ya Mungu ya kuingia kanaan bila woga na kuishia kufa watu waliokuwa na miaka 20 na kuendelea
Waliingia kanaan kupitia mji uliotawaliwa na fukwe wa yeriko ili kuweza kuiteka nchi nzima ya kanaan kwa vita
 
Mungu anae taka jamii moja kuteka nyingine na kupora adhi yao. Tunaweza kusema ni mungu wa wote kweli? Maana anao uwezo wa kuipanua ardhi watu wakaishi kwa amani. Tufikili tu kwa akili ya kawaida
 
Mungu anae taka jamii moja kuteka nyingine na kupora adhi yao. Tunaweza kusema ni mungu wa wote kweli? Maana anao uwezo wa kuipanua ardhi watu wakaishi kwa amani. Tufikili tu kwa akili ya kawaida
Jua kwanza kisa cha Mungu kuwachukia hawa waperisi na wakanaan ndio uchangie
Tafuta historia ya kanaan mwenyewe
Hutamsema vibaya Mungu
 
Jua kwanza kisa cha Mungu kuwachukia hawa waperisi na wakanaan ndio uchangie
Tafuta historia ya kanaan mwenyewe
Hutamsema vibaya Mungu
Mwanadamu ana sifa ya kuchukia na kulipa visasi. Mungu kumchukia binadamu nikumuonea
 
Kitu kingine ni kwamba vita bila Mungu mtaishia kupigwa tu hata kama wapinzani wenu wana vifaa vya kivita vichache
Mungu hahusiki na vita,sasa kama wayahudi waliteka eneo lenye ukubwa wa km 5o za mraba,na imekuwa ngumzo,vipi akina Alexandra the great waliofika mpaka India?,au kina Cyrus wa Persia ealioteka karibu Asia yote na sehemu za ulaya?.
Hapo ndo utajua kuwa watu wanawaoverate sana watu kama joshua.
Mwingine ni Solomon I,wanasema utawala wake haukuwa na mfano,ilikuwa na nguvu na ulienea sehemu kubwa,lakini ukisoma bible,Solomon I hakuwahi kupigana na kuteka hats kijiji kimoja.

Kwamba alikuwa na hekima haijapata kutokea,lakini ajabu aliishia kuabudu dini za kipagani,
Kwamba alijenga bonge
la hekalu,mafundi tu walikuwa 100,000,wakati plot yenyewe ilikuwa na ukubwa wa 20*20.
Kwamba hilo hekalu mpaka Leo kuna ukuta ambao wayahudi wanauabudu.,wakati ukweli ni kuwa ule ukuta ni mabaki ya ngome ya kijeshi ya utawala wa warumi
 
Sasa hizo Falme siijui Alexander wa ugiriki, uajemi babeli Roma we unajua nini kilisababisha zianguke na zisiwepo tena mpaka leo zimebaki historia tu
 
Jua kwanza kisa cha Mungu kuwachukia hawa waperisi na wakanaan ndio uchangie
Tafuta historia ya kanaan mwenyewe
Hutamsema vibaya Mungu
Sijui wapi ulisoma mungu anawachukia wa Persia,unless mungu unaemsema awe Netanyahu
Hao wapersia ndo waliwarudisha wayahudi toka utumwani babel,
Hata amri ya kujenga hekalu ilitoka kwa Cyrus,na ndo alimpa pesa Ezra na misaada mingine kujenga hekalu.
As caanan,habari ya wakanani kuchukiwa na sijui mungu ni propaganda tu,ili wayahudi wachukue ardhi,kama caanan ililaaniwa vipi tena ibadilike kuwa nchi takatifu?
 
Sasa hizo Falme siijui Alexander wa ugiriki, uajemi babeli Roma we unajua nini kilisababisha zianguke na zisiwepo tena mpaka leo zimebaki historia tu
Hakuna kitu permanent,hivi Sasaa kuna modern states,hats Israel ya Leo ni modern state sio ile ya enzi zile,
Israel ya zamani ilianguka na kupotea,
Zamani mwaka 1920,hakukua hata na Iraq,Kuwait,Dubai etc.

Nchi ambao zimekuweko enzi na enzi na kuendelea kuwepo continuously ni Syria,ottoman ambao ndo Turkey na Persia ambao ndo iran
Turkey ni kiini cha ottoman empire na Iran ni kiini cha Persia,
Syria peke yake IPO tangu Abraham anahamia caanan.
Hii Israel ya Leo ni tofauti na Israel ya enzi zile,kwani haina continiournity
 
Sijui wapi ulisoma mungu anawachukia wa Persia,unless mungu unaemsema awe Netanyahu
Hao wapersia ndo waliwarudisha wayahudi toka utumwani babel,
Hata amri ya kujenga hekalu ilitoka kwa Cyrus,na ndo alimpa pesa Ezra na misaada mingine kujenga hekalu.
As caanan,habari ya wakanani kuchukiwa na sijui mungu ni propaganda tu,ili wayahudi wachukue ardhi,kama caanan ililaaniwa vipi tena ibadilike kuwa nchi takatifu?
Mkuu naona tunazungumza lugha 2 tofauti singumzii Persia nazungumzia wenyeji ambao abraham aliwakuta wakati anatoka huko iraki kwenda kanaan kujichanganya na wenyeji
We inaleta story za wayahudi ambao ni kabila pekee la Yuda lililobaki Israel kwa sasa
 
Hakuna kitu permanent,hivi Sasaa kuna modern states,hats Israel ya Leo ni modern state sio ile ya enzi zile,
Israel ya zamani ilianguka na kupotea,
Zamani mwaka 1920,hakukua hata na Iraq,Kuwait,Dubai etc.

Nchi ambao zimekuweko enzi na enzi na kuendelea kuwepo continuously ni Syria,ottoman ambao ndo Turkey na Persia ambao ndo iran
Turkey ni kiini cha ottoman empire na Iran ni kiini cha Persia,
Syria peke yake IPO tangu Abraham anahamia caanan.
Hii Israel ya Leo ni tofauti na Israel ya enzi zile,kwani haina continiournity
Kabila la Yuda ndio lilibaki na ndio hawa wanaojiita wayahudi leo
 
Kabila la Yuda ndio lilibaki na ndio hawa wanaojiita wayahudi leo

Lakini hakuna kabila la yuda.
Na hats kiebrania wanachoongea sasa ni modern sio mile cha zamani,yaani kiebrania kilihuishwa upya miaka ya 1700.
Kwa hiyo hata kiebrania wanachoongea ni cha kuunda.
Inatakiwa ujue kuwa Israel ilipotea hawa waliokuja kuunda mpya waliforce ndo maana hawajui wajitambulishe kama waisrael ama wayahudi.
Kumbuka wakati wa tawala za Israel na yuda.
Israel walishikilia kuabudu mungu El.
Wayahudi wa yuda walikuwa na mungu wanaabudu akiitwa Yahwew.
Na wayahudi waliwaona waisrael kama wamepotea[/QUOTE]
 
Biblia ni Tamuu mnoo usomee. Lakini ukisoma uchambuzi wa kitabu kimojakimoja historia yake kilivyoandikwa na kikapatikana It very Irritating and surprising..
Mfano.
Inasemekana (Kwa mujibu wa biblia nayotumia mimi ikiwa inaeleza historia ya kitabu kimoja kimoja) Musa alipovuka baharini na wana israel Maji yalikua yamekupwa wammisri walipopita maji yakawa yamejaa bado hawajapita.

Mapigo Kumi kwa Wamisri..
Ipo hivi Mvua ilinyesha huko juu ukateremsha matope ndani ya mto naili mto ukawa mwekundu, Wana waisrael walipoona vile wakasema kua maji ya mto yalikua damu lakini kiuharisia maji yalikua mekundu kama damuu na sio damu iljaa mtoni.
Ajili ya matope vyura vikajaa mjini kutoka ndani ya mto..

Sasa wewe mwenzangu na mimi Yoshua anakuhusu nini? Hiyo Biblia yenyewe hapa kwetu haina hata miaka 150 leo hii wewe unataka kujiingiiza kwenye ambayo hata hauyafahamu undani wake?

Waache Waarabu na Wayahudi wenyewe watatue matatizo yao, wanajuana hao hata wanashare same dna pamoja lkn wewe hauna DNA na Yesu, Wayahudi au Waarabu!
 
Back
Top Bottom