Masaki
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 3,463
- 754
Tulisahau tu kumwomba ile sheria yao inayoshughulikia wala rushwa wakubwa kama wanasiasa, watendaji wakuu wa serikali na taasisi za UMMA.
Msaada huo hawezi kutupa kamwe, yuko tayari kutuongeze USD zingine milioni 100 ili tuendelee kuwa wababaishaji hivi hivi na aje achume anachokitaka miaka 10 ijayo kuliko akuletee siri kubwa ya mafanikio yake.
Moja ya siri za mafanikia makubwa ya kiuchumi ya China ni utawala wa sheria kali na kutolindana. Kuna mahali niliwa kusoma humu JF kwamba katika kuliweka taifa lao sawa, serikali ililazimika kuwauwa mafisadi 70! Baada ya hapo, mambo yakaanza kwenda sawa na kwa kasi ya ajabu. Mwaka 2025 China linatarajiwa kuwa taifa tajiri kuliko yote duniani!
Kwa bahati mbaya sana, Tanzania itakuwa bado masikini wa kutupwa na tena si ajabu wakati huo Rais atakuwa mtoto wa mojawapo wa maraisi wastaafu! Yaani wale wale!