hivi jiulize ingekuwaje kama kila mtu angepewa maarifa hayo kuwa we can synchronize with the higher creators...?
Hapa ngoja nikujibu kwa mtindo huu. Nyinyi tatizo lenu huwa hamko wazi na huwa mna mung'unya maneno kwa maslahi yenu binafsi.
Suala la maarifa au upatikanaji wa maarifa kwa mwanadamu kuna nyenzo,nyenzo ambazo kwazo binadamu anapata maarifa. Na hizo nyenzo ni akili,milango ya fahamu na ufunuo.
Elimu zimegawanyika sehemu mbili,kuna elimu za kilimwengu na elimu ya kumtambua Mola muumba wa mbingu na ardhi na vyote vilivyomo. Mola wetu amejiwekea utaratibu wa kumpa anae mtaka,mathalani sisi watu wa dini tuna amini ya kuwa hakuna mtume alie kuja ulimwenguni kufundisha kujenga majumba,wala elimu ya kilimo au elimu ya hali ya hewa bali mitume walipewa za kujitambua wewe ni nani,upo duniani kwa lengo gani,ni yapi maisha baada ya kufa ? Je kifo ni mwisho wa misha,ni lipi baya na lipi zuri,vipi nilinde akili yangu,vipi nilinde kizazi changu na mfano wake.
Umewagusia wanasayansi na ufahamu waliopewa,kupewa ufahamu huo sio jambo la ajabu kwani Mola wetu anampa amtakae katika waja wake na anamnyima amtakae,kwa mtu mwenye upeo mdogo kama wewe japo kuwa siwezi kukulaumu lazima utawaona wanasayansi ni bora kuliko wengine kisa wamefanya ugunduzi wa mambo kadha wa kadha,na ukafikia mbali kusema kwamba wao walipewa access ya code bila kutaja walipewa na nani ? Kufanya hivyo ni kuihujumu elimu na kuuficha ukweli kwa makusudi. Unasahau ya kuwa wana sayansi hao walipewa ufahamu huo lakini hawakumjua ni nani amewapa ufahamu aidha kwa makusudi au kwa ujinga wao na hii ndio hasara kubwa walio ipata wanasayansi na wana falsafa.
Maarifa yanaendana na juhudi leo hii weww usipofanya jitihada katika jambo fulani kamwe huwezi kulijua jambo hilo,huu ndio msingi wa maarifa au kupata elimu ulivyo.
Binadamu yeyote awaye ameumbwa akiwa na fitra/human nature,hali ambayo ni ya utayari kuupokea ukweli kuhusu Mola wake alie muumba,hali hii huwepo endapo mwanadamu huyo akiwa haja haribiwa kifikra au kimtazamo na watu wa imani za kishirikina,watu wenye kuabudu masanamu,watu wenye kuabudu jua na mfano wake.
Kuhusu hiyo higher level unayo ipigia upatu na kuizungumzia kwa kufanya ghishi na udanganyifu,suala hilo walikuja nalo mitume,kutokana na ukomo wa akili ya mwanadamu aliyo pewa na huku akiwa anajiuliza maswali kwa yale mambo yaliyofichikana ndio Mol akawa anachagua mitume miongoni mwa hao binadamu na kuwapa ufunuo na kuwajibu yale maswali ambayo akilo zetu haziwezi kuyang'amua mfano wa maswali kuhusu kifo,njaa,majanga ya asili,kufufuliwa na mfano wake,na kupitia hao mitume Mola wetu akajielezea jinsi alivyo kimaumbile. Kwa mfano mimi ukiniuliza umbile la Mola wangu nitakwambia yukoje na mimi nina muelezea Mola wangu kama alivyojielezea yeye mwenyewe. Mfano Mola wangu mimi ana mikono miwili na yote iko upande wa kuume. Lakini nitaona ajabu ukiniuliza swali,tena kwa mshangao,he Mola wako ana mikono ? Nitakujibu ndio ana mkono,na mimi nitakuuliza au kukwambia " Birika lina mkono,je mkono wako ni sawa na mkono wa birika ?". Sasa basi Mola wangu ni kweli ana mikono lakini mikono yake namna ilivyo ni kwa dhati yake yeye mwenyewe Mola na sisi hatujui ikoje,lakini tunathibitisha ya kuwa ana mikono na wala haifanani na mikono yetu.
Sasa unavyojifaragua kila siku na hizo "Higher level ......" sisi tunakuona kielimu bado mpo gizani tena kwa kujitakia nyinyi wenyewe sababu maswalo yenu au mambo yenu mnayo yazungumzia leo mitume na manabii waliyazungumzia miaka na mikaka iliyopita.
Sasa kwangu mimi wana sayansi na wana falsafa huwa nawaona wajinga hasa wanapo jaribu kizungumzia maumbile sababu wao walichagua ujinga na Mola wetu akawaelekeza huko huko kwenye ujinga wao.
Napumzika kidogo ..... Ila kaa ukijua mtume wetu anasema "Nime wa acha katika hali ambayo usiku wake ni sawa na mchana wake,hato potea humo isipokuwa yule atakae taka" au kama alivyosema. Siri wanazo binadamu wenyewe kwa mambo yao ila katika elimu hakuna siri zaidi ya udanganyifu tu wanao uleta wajinga fulani,ili waweke gap la kuogopewa wakati katika mizani ya kielimu na tabia njema ni watu wadogo sana tena wenye kupuuzwa.
Nina mengi sana ya kuandika kuhusu Mola wangu mlezi,Mola ambae ameumba ulimwengu na vyote vilivyomo,Mola ambae amemuumba binadamu katika umbile bora zaidi,Mola ambae ametufanya sisi binadamu kuwa watawala katika huu ulimwengu,ukiondoa Malaika hakuna kiumbe bora kuliko mwanadamu wala chenye kumzidi mwanadamu,ama kuhusu hao Aliens endeleeni kujifurahisha.