Naomba unipe neno mbadala kutumia badala ya logic. Inawezekana kabisa hilo lina madhaifu.
Pili, sina haja ya kutafuta ushahidi sana sababu hata katika hali ya kawaida kabisa tunapokuwa kwenye shughuli zetu, ukiuliza watu wanaokuzunguka katika jamii kama wanamuogopa Mungu? Jibu utapata ni Ndiyo. Utiifu kwa kuogopa au nidhamu itokanayo na hofu/woga. Hata mahakamani wanakuapisha kutumia vitabu vya dini ili uanze na hofu ya imani yako kwanza.
Chini hapo nimeweka baadhi ya mistari toka kwenye Biblia inayohusiana na swali lako. Kwa upande wa uislam naomba wenye hiyo mistari toka kwenye Quran wajibu kwa sasa.
Exodus 20:20- Moses said to the people, Do not be afraid. God has come to test you, so that the fear of God will be with you to keep you from sinning.
Luke 1:50- His mercy extends to those who fear him, from generation to generation.
Acts 10, 34-35: Then Peter began to speak, I now realise how true it is that God does not show favoritism but accepts men from every nation who fear him and do what is right.
Hivi kwa akili ya kawaida kumuogopa Mola ni sawa na kupandikizwa hofu ? Hili swali jibu unalo mwenyewe.
Nakupa maelezo ya ule msemo wa waswahili ya kuwa "Ya kuwa asie kujua hakuthamini". Wewe leo hii huwezi kujua nafasi ya Mola muumba sababu humjui,kwahiyo kwako wewe Mola muumba unamuona hana thamani sababu humjui.
Sasa narudi katika uhalisia,uhalisia ambao wewe umekupitia mbali,suala la mja kumuogopa Mola ni matokeo ya yeye kumjua na kumthamini na kumtii. Kuchunga mipaka yake,mathalani Mola wetu amekataza watu kula riba, kwani riba ni katika njia chafu na upotevu,sababu asili ya mja kumsaidia mja mwenzake ni kumfanyia wepesi katika lile tatuzo lilo msibu,sasa wewe unapotaka kumsaidia mwenzio kwa kumuwekea riba,ile maana ya msaada inaondoka na wewe unamzidishia tatizo mwenye shida. Kwa hali hiyo Mola akaweka adhabu kali kwa wale walao riba na wahusikao katika riba. Sasa yule mja alie mjua Mola wake na kumtii na kujua ubaya wa kile anachokifanya na akawekwa wazi juu ya malipo ya adhabu ya kile anachokifanya,kisha aka acha kufanya ovu lile kwa kuogopa adhabu ya Mola wake huo ndio usahihi,bali anakuwa amewasaidia wengine katika kupata shida ya kile kibaya endapo angekifanya.
Sasa wewe unapojaribu kutafsiri kuogopa kama ugonjwa mbauya,umesahau natija ambazo zinapatikana endapo binadamu wata acha kufanya maovu,na kuwekwa wazi juu ya malipo ya ubaya ndio usahihi bali ni jambo la lazima,na kumuogopa Mola kwa kumtii na kutom muidhi yeye ndio uokovu,sababu hajakataza jambo lolote isipokuwa lina faida na sisi.
Kwahiyo ni kwamba sisi tumefundishwa kumjua Mola na hatuja fundishwa kumuogopa Mola,bali kumuogopa Mola ni matokeo ya kumjua,kumtii na kuogopa adhabu zake kwani ni haki yetu kuziogopa kwani ni kali na zenye kuumiza. Bila kusahau ya kuwa kuna kinyume cha adhabu ambacho ni malipo kwa yale mema tunayo yafanya kwa kumridhisha yeye, na ametuahidi kutulipa mema na starehe ya kudumu.
Na ni kweli ya kuwa Mola wetu ni mjuzi wa kuadhibu.