Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Hivi jamani Klabu yetu ina mpango kweli wa kuongeza beki 🤔 kipindi cha Usajili sababu Job na Kibwana Shomari mnawaonaje wale Kimataifa?

Hapa nazungumzia maumbo yao hasa tukikutana na timu zinazotumia mipira ya juu wataweza kweli?
 
Hivi jamani Klabu yetu ina mpango kweli wa kuongeza beki [emoji848] kipindi cha Usajili sababu Job na Kibwana Shomari mnawaonaje wale Kimataifa?

Hapa nazungumzia maumbo yao hasa tukikutana na timu zinazotumia mipira ya juu wataweza kweli?
Nina imani na Dickson Job kuliko Bakari Nondo. Yule jamaa ni kama kuna wakati anajisahau halafu Job anafuta makosa yake. Anahitaji msaada Mwamnyeto
 
Hivi jamani Klabu yetu ina mpango kweli wa kuongeza beki [emoji848] kipindi cha Usajili sababu Job na Kibwana Shomari mnawaonaje wale Kimataifa?

Hapa nazungumzia maumbo yao hasa tukikutana na timu zinazotumia mipira ya juu wataweza kweli?
Kuna Beki Mmoja Ni Mkongomani Anaitwa Lomalisa Mtambala Anachezea Timu Ya G.D Sagrada Esperanca Ya Angola, Nasikia Yanga Wanasubiri ITC Yake Ikamilike Na Kupewa Release Letter Kutoka Kwa Klabu Yake Then Watamtambulisha, Huyu Jamaa Anacheza Beki Wa Kushoto Na Kiungo Mkabaji Kwaio Nadhani Ujio Wake Utamfanya Kibwana Shomari Arudi Kugombania Namba Yake Kwa Djuma Shabani Af Lomalisa Rasmi Atakuwa Beki Wetu Wa Kushoto, Bangala Na Bakari Mwamnyeto Watabaki Kati Af Kulia Atakaa Djuma Shabani.
 
Afadhali na hii italeta nafuu kwenye michuano ya Kimataifa ili tuachane na mambo za kutolewa mapema.
 
Huyo jamaa nilisikia tetesi zake kuhusu Yanga kumtaka japo sina taarifa zake ni kwa namna gani ni aggressive defensively
 
Bora beki mtulivu kuliko yule mrefu na bado hana utulivu. Tunahitaji beki wa kweli waku wachangamsha Job na Nondo
Kweli Kabisa Mkuu Tunahitaji Mtu Wa Kuwapa Ushindani Wa Namba Pale Nyuma Kwa Hawa Jamaa Wawili Mfano Mimi Huwa Napenda Sana Kumuona Bangala Akicheza Kama Kiungo Pamoja Na Aucho... Sasa Sijui Kwenye List Ya Usajili Ambao Alisema Manara Kuwa Tutasajili Wachezaji Wasiopungua Wanne Na Wasiozidi Watano Wa Kimataifa Kama Kutakuwa Na Beki Wa Kati Wa Kuja Kuwapa Changamoto Hawa Watu Wawili.... Ngoja Tuone.
 
Kama ni kweli hizo sajili zitafanyika basi ni lazima kutakua na CB haiwezekani kutosajili beki wa kati
 
Hii ndo shida (ufupi) na Kimataifa kuna timu baadhi wao goli zao huwa ni za kupitia kona na set pieces tu.

Sasa hawa mabeki wafupi watatugharimu huko mbeleni.
Kabisa Yaani Mkuu...Nadhani Akina Nabi Na Kamati Yake Ya Usajili Wanaliona Hilo.
 
Huyo jamaa nilisikia tetesi zake kuhusu Yanga kumtaka japo sina taarifa zake ni kwa namna gani ni aggressive defensively
Nasikia Wanamsifia Kwamba Yupo Vizuri Sana Jamaa Hasa Kwenye Kupandisha Mashambulizi... Bangala Na Djuma Shabani Ndio Waliompigia Debe Kwa Nabi...Kama Ni Kweli Atakuwa Vizuri Kama Wanavyomsifia Basi Tutakuwa Tumelamba Dume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…