Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Ameandika wilson Oruma.

"Yani Kanuni zikikupiga wewe tu ndo zinakuwa
hazijasajiliwa? Na kama Kanuni hazijasajiliwa simple logic ni kwamba Yanga msimu huu sio Bingwa.Hebu jaribu kusema hivi nione kama kweli ww ni kudume.

Eti ndugu yangu Lengai ole nasha Leo unajiona wewe ni Yanga zaidi kuliko Waziri Mchengerwa?Yani wewe ni Yanga zaidi kuliko mtu ambae hajawahi kusema yeye ni Simba hata kwa utani?Hii nchi Uhuru
umepitiliza.

Halafu Moja ya vitu navichukia zaidi kutoka kwako ni kugeuza matatizo yako dhidi ya TFF au mtu yeyote kuwa ni matatizo dhidi Yanga.
Hata wakati ule ni msemaji wa team yako ya Simba hii ndo ilikuwa tabia yako.Niligombana na wewe kwenye group ukageuza ukawa ni ugomvi wa group
dhidi Yangu.

Na kwasababu team zetu hizi Mashabiki wake wengi ni wale oya oya agenda yako hii huwa inafanikiwa.Nakukumbusha brother wewe umegombana na TFF iweke Yanga pembeni kwenye hili.

Ndugu zangu Yanga jitengeni na hii dhambi.Huyu ni mtu ambaye anataka kuwatumia nyie kwa manufaaa
yake binafsi.

Yeye peke yake ndo alitaka kumpiga Rais
wa TFF Wallace Karia.Na yeye ndo aliomba radhi kukiri makosa yake.Jitengeni nae.

Eti TFF kukufungia wewe ni kutaka kufifisha tamasha la Siku ya Wananchi.Who are you? Wewe ni nani kutaka kujipa vyeo ambavyo huna? Yanga ni li kitu kubwa na ndo maana waliweka rekodi ya Mapato na attendance wakati wewe upo Simba Sports.

Na ndugu zangu TFF huyu mtu ana kiburi Cha
Followers ongeza tena miaka 3 iwe 5 kabisa.Kuna Serious allegations nyingi amezitoa Leo ikiwa na kusema Katibu Kidao amepeleka ushahidi wa Uongo
Kamati ya Maadili.

TFF Please Ongeza 3 huyu iwe 5 kabisa..[emoji119]"
 
Shida ni moja kwa wote Mana na Karia. Kwa kuanza na Karia na Kamati ya Maadili + TFF ni kwamba, kama katika Video ilionekana wanazozana, Je, ni nani aliyeanza kumzoza mwenzake? Kama wanaonekana kutupiana maneno kwa nini kanunu ya Natural Justice isingetumika ili kuwasikiliza wote ili hata kama mlengwa ni Manara mjioneshe kuwatendea haki wote kuwa mliwaita na kuwahoji.

Kwa nini Kamati ya Maadili haijampa hati ya adhabu kama ilivyotaratibu kuonesha kuwa ameshapewa adhabu, kukaa nayo na mnasema mmemfungia si sawa maana mnasema jwa midomo ilihali sheria ipo wazi kuwa udhibitisho wa maandishi ndiyo unaokubalika. Kwa kweli madai ya Manara ni sahihi kutopewa hati ya adhabu TFF wamekosea.

Upande wa Manara, kama Manara anaona ameonewa kwa nini asiende kwenye vyombo zaidi ya TFF kutafuta haki kuliko kutafuta huruma ya Wananchi ambao hawatampa msaada wowote?
Ni kweli Manara hana wanasheria kumsaidia kuitafuta haki Kisheria kuliko kuja kuongea na wananchi?

Pia, Manara ameshajiona mkubwa sana, anatumia nafasi hiyo kufanya anaoyoona ni sawa lakini si sawa. Apunguze kujiona bila yeye hakuna Yanga wala Mpira, apunguze nyenyenyeeee
 
Manara Hujifanya Mtoto wa Kariakoo kakutana na Mtoto Tanga

Yaani anakujaza upepo unaingia kingi unamtukana hadharani anakuangalia tu.

Sekretariate inakupeleka kamati ya nidhamu.

Unaibuka kuwa hukumtukana
Anakupigia simu kuwa njoo home tuyamalize.

Unaenda nyumbani kwake kama bibi harusi ukiwa na mshega,unakaribishwa juice mtoto wake anakupiga picha na anakwambia yameisha.

Kesho yake unatoa tamko kuwa ulikosea kumtukana na unajutia kitendo hicho na umeomba msamaha kwa ujinga uliofanya.nimekosa mimi nimekosa mmi nimekosa sana.

Wiki inayofuata Unapigwa ban ya miaka miwili

Unaitisha press huku unalia kuwa umeonewa hukumtukana bali yeye ndio alisema tuna kinyesi kwenye chupi

Jamaa yuko nyumbani anakuchora kwenye luninga unavyolia anakucheka tu
[emoji3][emoji3]

Kuwa mtoto wa mjini raha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…