Ndugu yangu @wilsonorumatz_ amesema derby ya Simba na Yanga ndio mechi pekee duniani inayochezwa kila siku. Inachezwa uwanjani na nje ya uwanja. Inachezwa wakati wa msimu na nje ya msimu. Inachezwa mjini na vijijini. Inachezwa makanisani na misikitini. Inachezwa usiku na inachezwa mchana.
Nakubaliana nae kwa 100%. Simba na Yanga zinacheza kila siku kupitia tambo, majigambo, utani wa jadi, kejeli (sio matusi) na mambo mengine yanayofanyika nje ya uwanja. Simba wakifanya jambo Yanga watalibeba kwa utani na litazaa tambo, majigambo, kejeli etc. Vivyo hivyo Yanga wakifanya jambo.
Kwa mfano wiki hii Simba na Yanga zimecheza kupitia jezi za Yanga. Jezi zimeleta mjadala mkubwa mtaani baina ya mashabiki. Wakati Yanga wakijisifia na umaridadi wa jezi zao, Simba wanawatania kwa kukosa ubunifu. Wanadai ni utando wa buibui, GPS, na wengine wakidai wamemuona "Hamza" kwenye jezi hizo [emoji1787][emoji1787].
Huu ni utani wa kunogesha derby ya Karikoo. Mashabiki wa Simba wanatupa makombora mazito na mashabiki wa Yanga wanajitutumua kujibu japo wanaonekana kuzidiwa nguvu na akili. Sasa nao wanajipanga kusubiri kwa hamu uzi wa Simba. Ikitokea ukawa uzi wa hovyo tujiandae kupigwa vijembe, kejeli na utani wa kila aina.
Na hii ndio maana ya utani wa jadi. Ni fujo isiyoumiza. Shabiki wa Yanga hawezi kukasirika akitaniwa na Simba, vivyo hivyo Simba akitaniwa na Yanga. Ukiona mtu anakasirika sababu ya mpira, ujue huyo sio shabiki, ni "kibaka" tu mwenye stress za maisha. Achana nae. Vibaka wa aina hii wapo wengi. Hawelewi maana ya utani. Kila utani wao ni kukasirika na kutukana tu.
Wanasahau kwamba utani, kejeli na tambo za mpira zinasaidia kuongeza thamani ya derby ya Kariakoo. Kwa mfano msimu ujao Yanga watajitahidi sana kufanya ubunifu kwenye uzi wao ili yasitokee ya msimu huu. Simba nao watajitahidi wakienda pre-season wakae hoteli yenye hadhi ili wasitaniwe kuishi bwenini. Hivi vyote vinaongeza thamani ya derby ya Kariakoo na ligi yetu.
Bila hizi amsha amsha, derby yetu ingepoteza mvuto. Ingepoa, ingedoda. Kenya kulikua na derby ya FC Leopards vs Gormahia. Leo iko wapi? Imekufa kwa kukosa amsha masha. Kwahiyo "vishohia" punguzeni stress na makasiriko. Utani unaongeza value ya mpira.!