Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Huwa nachukia nikiona shabiki anaumia eti mchezaji ametaka kusepa afu mtu alaumu Viongozi. Kama amesepa asepe, good thing ni kwamba eneo lake lina watu kibao wa kucheza.

Huu ndio muda wa kuona ubora wa watu kama Aziz Ki.

Always ukitanguliza tamaa matokeo yake huwa majuto.
KAVUMBAGU, SINGANO (MESSI), NGASSA nk

Mwacheni aende akapambane, Yanga ni kubwa kuliko Mtu, na naushauri uongozi kuachana na habari za kumfuatilia wala nn, wapige kimya, tujiandae na International games.

Mchezaji mwenye akili angesubiri acheze game za kimataifa ili ajiuze zaidi mbele huko na sio kuhangaika na timu za Dar.

Binafsi nimelipokea kwa kawaida sana, nikiwa najua huko mbele angetusumbua sana maana tulimjaza sifa, mpaka ameona bila yeye timu haiendi.
 
BAADA YA KUIONA BARUA YA FEITOTO... NIMERIDHIKA KABISA KUONDOKA KWAKE... NA BILA SHAKA KWENYE MECHI YA KESHO HATOKUWEPO BENCHI LA YANGA. KILA LA KHERI... NAMUONEA HURUMA SANA... WALIO NYUMA YAKE HAWAMTAKII MEMA... NIA YAO NI KUIBOMOA YANGA...SI KWA MASLAHI YA FEISAL...

SAWA ATAPATA PESA ILA POSSIBLY NI SHORT TERM.
 
Wewe ndio unamtajia mema mwnzio aendelee kusugua vumbi aache kwenda kula pesa???????huo ni uchawi
 
Nakazia Mkuu.

Yanga ni kubwa kuliko mchezaji yeyote yule.
 
+Donald Ngoma
 
Kama hizi sio rumours kwa Feisal mi kwa upande wangu naona ni sawa tu sababu mwenyewe ndo ameshaamua na siku zote wanasema mpira ni ajira basi tumtakie kila la kheri.

#DaimaMbeleNyumaMwiko.
Mataahira ya Ngada FC yalivyobeba bango utafikri pale jangwani alikuwa nakaa bure! Kwa kweli ni haki yake, wala Yanga haipaswi kuwa na pressure naye! Wamwache aende kwa salama!
 
MAONI YANGU KUHUSU SAKATA BYUTI BYUTI

Kuhusu uhalali wa Feisal Salum kuvunja mkataba ni suala la kisheria zaidi. Sina utaalam wa sheria kwahiyo nikizungumza utakuwa uongo!

Nahitaji muda kuzungumza na wataalam wa sheria kidogo kabla sijaweka mawazo yangu. Kwasasa ninachoweza ni kunyamaza na kusikiliza wengine mpaka nipate utaalam wa kisheria.

Kitu pekee ninachoweza kuchangia ni mtazamo wangu kuhusu uamuzi wa Fey Toto. Amefanya vema au amekosea??

Kwanza kabisa nafikiri Fey Toto yupo katika kiwango bora cha maisha yake. Feial wa leo sio miaka mitano iliyopita. Fey amekua, ameimarika na sasa yupo katika 'peak' ya soka lake.

Huu ndio ulikuwa muda kwa yeye kupata pesa nyingi katika kipindi chote cha maisha yake ya soka. Kiwango cha sasa ndicho kilichopaswa kumpa pesa ndefu.

Kwa kuitazama kona ya maslahi, nafikiri Fey amefanya vema! Soka ni 'career' ya muda mfupi. Unapokuwa katika nafasi ya kuchuma pesa kazana kuchuma pesa nyingi uwezavyo.

Nasikia atalipwa mshahara mara nne zaidi ya aliokuwa akipokea Yanga. Hapo weka kando signing on fee na bonuses. Angefanya nini zaidi Fey??

Kama Fey amevunja mkataba kihalali basi Yanga walifanya kosa kubwa sana, kutokuchungulia kipi kinaweza kutokea mbele. Walipaswa kuboresha maslahi yake hata kama bado walikuwa na mkataba nae.

Watazame Chelsea walivofanya kwa bwana mdogo Trevoh Chalobal juzi tu! Angalia walichokifanya Man City kwa Phil Foden. Hata Yanga walifanya vema kwa Yanick Bangala na Mayele mwanzo wa msimu.

Kama Fey amevunja mkataba kihalali basi kuna uzembe mkubwa sana kwa upande wa Yanga. Feisal Salum si aina ya mchezaji wa kumpoteza kwa mpinzani wako wa karibu. Labda ushawishiwe kwa kitita kikubwa cha pesa.
 
Binafsi nimekuwa nikimuona kama mchezaji ambaye tunampa sifa kubwa zaidi, hali hii imepelekea tukose kuona vipaji vya watu kama Aziz Ki kwa kukosa ule uungwaji mkono wa mashabiki. Feisal sio kwamba yy ameibeba timu mabegani, kuchomoa kwenye game ngumu, ni sawa na afanyavyo Mayele, sema tu sisi Wabongo tukipenda kitu inakuwa hivyo.

Binafsi kwa Yanga only two au Three players wakiondoka nitakuwa na hofu sana kwa maana nafasi zao ni muhimu na ngumu kuziziba.
1. DIARRA
2. MAYELE
3. BANGALA

hao watu wakiondoka leo hii timu yetu itayumba sana.
OTHERWISE DOGO ASEPE, akashindanie MAPINDUZI CUP, mpira sio tu pesa, mpira ni zaidi ya exposure, unabaki AZAM kisa 200M? Then what next? Azam ni ngumu kwa scouts kukuona ukapata timu za maana nje.

Mashabiki tuache kuwavimbisha kichwa hawa maboya.

LETS GO AZIZ KI, tumemsajili ili aoneshe ufundi, na ana more skills than Feisal tena amemuacha mbali, ameanza kuclick kwenye mfumo na kuelewana na wenzake.

Ilikuwa suala la muda Fei kula mbao.
 
Maneno meeeeeeengi ,pesa kidogo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapo je?
 
Mlijinasibu mna pesa mob kengemaji nyie kumbe waongo,mnamlisha mtoto wa watu mihogo wakati kazoea urojomix na kuku wa kupaka[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jiesiemu yupo wapi aokoe jahazi?
Nchi hii tajiri ni mmoja tu hao wengine wote machawa ....
 
Ina mana gsm ni chawa wa mo
 
Mataahira ya Ngada FC yalivyobeba bango utafikri pale jangwani alikuwa nakaa bure! Kwa kweli ni haki yake, wala Yanga haipaswi kuwa na pressure naye! Wamwache aende kwa salama!
Kweli kabisa sababu ukiangalia nyuzi zao hao Ngada Fc zilivyojaa majukwaani kuhusu huyo Feisal mpaka unajiuliza hawa majamaa vipi sababu hii issue wameivalia vibwaya haswa.

Na mawazo yao wanajua kama bila Feisal basi Timu ya Wananchi haitakuwepo tena.

Wanasahau siku zote wachezaji ni watu wa kupita tu katika vilabu.
 
Nimekuelewa sana Mkuu. 👏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…