Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Timu ndogo mnaanzia mchangani 😂😂😂😂😂😂🐸🐸🐸🐸🐸🐸
 
Vp hizi timu za Otoho na Al Merrikh ubora wao ukoje?
Binafsi nawaogopa zaidi Al Merrikh kwasababu wanauzoefu na hii michuano ya CAF. Hawa Otoh waliwahi kufika hatua makundi mara moja tu msimu wa 2018/2019 ila mara zingine zote ni hatua ya awali au ya pili wanishia.

Pamoja na kutokufuzu kucheza hatua ya makundi, Otoh ni habari nyingine akiwa nyumbani kwake. Hajafungwa nyumbani kwake

Msimu wa 2018/2019 kashinda 2:0 vs Mc Alger
Kashinda 2: 0 vs de Agosto
Kasuluhu vs Platinum

Msimu wa 2019 kamfunga Mamelod 2:1
Kasuluhu vs Al Merrikh

Msimu wa 2021/2022 kamfunga UD Songo 1:0
Katoa sare na petro Luanda
Msimu wa 2022/2023 katoa sare vs Cape Town

Hawajawahi kufungwa kwao hao jamaa.
 
Hapo nadhan El merreikh wako VIZURI..ila tutawakalisha...
NAWAOMBEA SANA ,WAMALIZE VITA SUDAN
Huenda mechi zote zikachezwa uwanja mmoja au wakatafuta uwanja mwingine nje ya Sudan. Ila hawa jamaa wako vizuri mno, ni mfupa mgumu kwa Yanga. Tunapaswa kujipanga haswa, wana uzoefu na pia wana timu nzuri. Msimu uliopita walicheza hatua ya makundi
 
Hata sisi msimu uliopita tumekutana na timu zilikuwa hazijawahi kufungwa nyumbani lakini tukazifumua! Kwa Yanga hii yeyote anakaa!
 
Sikatai hilo linawezekana ila tupate kwanza straika mwenye uwezo wa kumzidi Mayele au awe sawa na Mayele
Yanga Wafanye Kweli Kwa Karamoko Wa Asec Mimosas Waachane Na Huyo Mahop Sinaga Imani Kabisa Na Washambuliaji Wenye Miili Mikubwa Ukute Mwili Mkubwa Mpira Wenyewe Hamna, Akatuletea Mambo Ya Lukaku Pale Mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…