Unaweza kusema tumefika kutokana na mtazamo wa haraka na matokeo tunayopata lakini kimbinu na kiufundi kulingana na falsafa yangu bado kabisa hatujafika pale ninapotaka . Tunatakiwa kuwa bora na kuweza kudumu katika ubora huo kwa msimu wote “
“ kila kitu kipo hapa cha kutufanya tuwe bora . Tuna uongozi bora , mashabiki wenye upendo na timu yao na kikosi chenye mseto mzuri kuweza kukifanya kuwa bora uwanjani . Hatuhitaji kuridhika kwa sasa ! Bado mapema na tena mtazamo wa kuridhika kwangu haupo labda msimu ukiisha . Muda wote tunapaswa kuwa na kiu ya kushinda na mchezo bora pia “
🗣️ Gamondi