Muda ufike Yanga ifanye uchaguzi; ili wapatikane viongozi makini. Baada ya uchaguzi, hao viongozi watakao chaguliwa waje na mkakati wa kutafuta vyanzo vya kuiendesha timu na pia kusajili wachezaji wenye hadhi. Wazee wenzangu na wachezaji wenye viwango vya kawaida, waachwe kwenye usajili ili wakatafute maisha mahali pengine.
Hii hali ya kuwa na wachezaji wengi wa kawaida inaifanya Yanga kutotabirika kama watani wetu Simba na mwisho wa siku timu inaishia kupata ushindi kwa kubahatisha au kupoteza kabisa.