Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Muda ufike Yanga ifanye uchaguzi; ili wapatikane viongozi makini. Baada ya uchaguzi, hao viongozi watakao chaguliwa waje na mkakati wa kutafuta vyanzo vya kuiendesha timu na pia kusajili wachezaji wenye hadhi. Wazee wenzangu na wachezaji wenye viwango vya kawaida, waachwe kwenye usajili ili wakatafute maisha mahali pengine.

Hii hali ya kuwa na wachezaji wengi wa kawaida inaifanya Yanga kutotabirika kama watani wetu Simba na mwisho wa siku timu inaishia kupata ushindi kwa kubahatisha au kupoteza kabisa.
 
Yanga ni wajinga sana, Tambwe kakosa penati.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tambwe kwa sasa amekuwa ni mchezaji wa kawaida sana kutokana na umri bila shaka. Nadhani huyu ni mmoja wa wale wachezaji wanaostahili kupewa mkono wa kwa heri mwishoni mwa msimu iwapo timu itapata viongozi na kufanya usajili.

Amekosa penati kizembe na bado dakika chache baadae akakosa tena goli la wazi. Leo hakuwa kabisa kwenye mchezo.
Kocha amefanya jambo la msingi kumtoa ndani ya dk chache tu za hiki kipindi cha pili.
 
Back
Top Bottom