Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Umemuambia hapo juu leta msimamo wa kundi ulivyomalizika tuone hiyo timu anayosema ni bora ilimaliza ya ngapi ana piga blabla tu
Anajua ila anajaribu kufuturu mchana kwenye chumba chenye giza
 
Unataka tathmini gani ,Tathmini ya ubora ilkuwa kwenye Group stage basi hakuna tathmini nyingine zaidi ya hiyo ,Msimamo wa kundi ulivyomalizika ndio ubora wa timu huo sio kufunga magoli.
Iyo group stage kama ingekuwa ni knockout stage usingetoboa labda kwa saoura peke yake , sababu nyumbani ulishinda sawa lakini away ulikuwa unafyatuliwa mpaka raha yani
 
Anajua ila anajaribu kufuturu mchana kwenye chumba chenye giza
Hizo taarabu tuu, zile zile timu za kwenye group ukikutanishwa nazo kwenye mtoano home & away humtoi hata m'moja.. Tukiacha ngonjera
 
Iyo group stage kama ingekuwa ni knockout stage usingetoboa labda kwa saoura peke yake , sababu nyumbani ulishinda sawa lakini away ulikuwa unafyatuliwa mpaka raha yani
Huyo As vital alishinda mechi gani ya Away au hata kutoa draw
 
Iyo group stage kama ingekuwa ni knockout stage usingetoboa labda kwa saoura peke yake , sababu nyumbani ulishinda sawa lakini away ulikuwa unafyatuliwa mpaka raha yani
Kwa hiyo CAF na FIFA wanafanya makosa kuweka timu katika makundi? Pia TFF inafanya makosa kuendesha mechi kwa mtindo wa ligi badala ya mtoano?
 
Hizo taarabu tuu, zile zile timu za kwenye group ukikutanishwa nazo kwenye mtoano home & away humtoi hata m'moja.. Tukiacha ngonjera
Huo mdomo wako sio mpira... game za mtoano niza tofauti sana na unavyokiria
Wale waarabu tuliwapiga 3-0 away.. home wakashinda 2-0, kwa mfano huu tungewatoa hawa sio kwamba wote wangetutoa.
Lakini mpira hauko hivyo fikiri tena... Ndio maana wengi tuliamiani kundi la simba hawezi kupita ila akapita
 
Hawezi kuleta kundi mkuu .. anaponda kisa tulifika malengo yetu
Kufika malengo yenu kusiwafanye kujiona bora zaidi ya waliokuzudi tatizo manara kashashikia akili mnamwamini hata akiwalisha makamasi
 
Sawa sikatai vipi na huyu mnayemwita mbovu..
 
Kufika malengo yenu kusiwafanye kujiona bora zaidi ya waliokuzudi tatizo manara kashashikia akili mnamwamini hata akiwalisha makamasi
Ubora wetu ndio huo kufika malengo... hayo ya Manara ni povu lako tu lenye jazba na ubora wetu.
Relax bado tunajenga timu yetu na nyie jengeni yenu sio kuvaa madela ya timu nyingine
 

Kampuni ya GSM ilishinda tenda ya kutengeneza na kusambaza vifaa mbalimbali vya timu ya Yanga zikiwemo jezi

Inaelezwa mchakato wa utengenezaji wa jezi mpya za Yanga unasimamiwa na GSM na zitatambulishwa August 04 siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi wakati Yanga itakapomenyana na AS Vita kwenye mchezo wa Kimataifa wa kirafiki ambao pia utatumika kutambulisha kikosi cha timu hiyo

Msimu huu unaokuja Yanga itakuwa na matoleo matatu tu ya jezi, yaani jezi ya nyumbani, ugenini na jezi nyingine ya dharura

Kwa mara ya kwanza mashabiki wa Yanga wataweza kununua jezi halisi zitakazotumiwa na timu yao msimu mzima

Msimu uliopita Yanga ilitoa zaidi ya matoleo tisa ya jezi ambapo ilifikia wakati jezi halisi hazikufahamika

Wakati huu wa maandalizi ya msimu, kwenye michezo ya kirafiki Yanga inatumia jezi nyeusi zenye michirizi ya njano

Aidha, kampuni ya GSM pia itasimamia mauzo ya jezi halisi za Yanga hivyo kuwa na uhakika wa jezi hizo kupatikana nchi nzima

GSM pia itaweka duka Makao Makuu ya klabu ya Yanga
 

Mlinda mlango wa timu ya Yanga Farouk Shikalo aliyesajiliwa kutoka timu Bandari Fc ya Kenya anataraji kuwasili nchini leo kwa ajili kujiunga na timu hiyo iliyopo kambini mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo zinaeleza Shikalo anataraji kuwasili hapa nchini kwa Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways,
 


Kocha Msaidizi Noel Mwandila ndiye Msimamizi Mkuu wa program za mazoezi ya Yanga mkoani Morogoro

Wakati huu ambao Zahera bado hajarejea kutoka mapumzikoni Ufaransa, Mwandila ndiye anayeratibu na kusimamia mazoezi yote

Peter Manyika yeye ana kazi ya kuwanoa walinda lango

Naye anasubiri ujio wa mlinda lango Farouk Shikalo ili akamilishe idadi ya walinda lango wanne ambao huenda akafanya nao kazi msimu mzima

Shikalo anaweza kutua mkoani Morogoro leo Jumapili

Metacha Mnata, Ramadhani Kabwili na Klaus Kindoki wako katika mikono salama ya kipa huyo wa zamani wa Yanga

Manyika ametua kuchukua nafasi ya Juma Pondamali ambaye alidumu katika nafasi hiyo kwa takribani misimu minne

Hafidh Saleh ni mratibu na msimamizi wa shughuli zote za timu hiyo nje ya dimba

Dk Edward Bavu yeye jukumu lake kubwa ni kuhakikisha afya za wachezaji ziko salama

Meneja Nadir Haroub 'Cannavaro' (hayupo pichani) yeye ndiye mtu wa karibu zaidi na wachezaji

Ni kiunganishi kati ya uongozi wa Yanga na wachezaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…