Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kurejea kwa beki Juma Abdul ni habari njema kwa kikosi chake kinachojiandaa na mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers
Abdul alikosa mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam, akiweka ngumu kuingia kambini hadi alipwe madai yake
Abdul ana nafasi ya kuanza mchezo utakaopigwa Botswana August 23 baada ya Boxer kupata majeraha
Zahera amefichua kuwa anataka kumtumia Abdul kwenye mechi hiyo ya ugenini kumimina krosi zenye macho ambazo zitakuwa zikiwafikia mastraika wake watakaokuwa na kazi ya kufunga tu, baada ya kubaini kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita walizikosa krosi hizo. "Kikosi chetu kilikuwa kikimtegemea zaidi Boxer ambaye atakuwa nje kwa muda baada ya kuumia goti kwenye mchezo wa awali ulioisha kwa sare ya 1-1, lakini hata wale ambao niliwatumia kuziba nafasi yake hawakufiti ndio maana nimefurahi Abdul kurejea," Zahera amenukuliwa na Mwanaspoti
Zahera alisema kwa jinsi alivyowasoma wapinzani wake amegundua ni wabovu kwenye mipira ya krosi, hivyo ujio wa beki huyo anayefanya vizuri eneo hilo inaweza ikawa dawa dhidi ya wapinzani wao kuweza kupata matokeo katika uwanja wao wa ugenini
Kuhusu Yondani, Zahera alisema pia ana nafasi ya kucheza itategemea na mfumo atakaoutumia, huku akiwamwagia sifa mabeki Ally Mtoni βSonsoβ, Lamine Moro jinsi walivyocheza kwa kuelewana hawakuwa na makosa mengi kwenye mchezo huo.
Alisema kwa mfumo wa kuchezesha mabeki watatu Yondani anaweza kufiti kwa kukaa kati huku Sonso na Moro wakiwa pembeni yake, lakini alisisitiza mchezo unaofuata unahitaji mawinga wenye kasi sambamba na mabeki wa kupanda kupitia pembeni.
#sisihaoβ - Yangafulldoz