Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza nafasi mbili za kazi, moja ikiwa ya Afisa wa Habari na nyingine ikiwa Afisa wa Uhamasishaji
 
Tunawaahidi kufunga kila timu itakayoingia anga zetu. Hivyo mtavaa sana majezi ya timu za nje
 
KUELEKEA MBIO ZA KUWANIA UBINGWA WA TPL MSIMU WA 2019 / 2020 TIMU YA WANANCHI INAFUNGUA DIMBA KWA KUJITUPA UWANJA WA BIBI KUKIPIGA NA RUVU SHOOTING HAPO 16:00HRS. KILA LA KHERI TIMU YA WANANCHI.

"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.
 

Wachezaji Paulo Godfrey 'Boxer' na Mohammed Issa 'Banka' wataukosa mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa leo kwenye uwanja wa Uhuru

Daktari wa kikosi cha Yanga Dk Edward Bavu, amethibitisha wachezaji hao kuwa majeruhi

Boxer alipata maumivu ya nyama za paja kwenye mchezo dhidi ya Township Rollers wakati Banka aliumia kabla ya mchezo wa Rollers lakini alilazimika kucheza mchezo huo

Dk Bavu amesema beki Ally Ally aliyepata majeraha kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania, amepona na amerejea kikosini
 
KUELEKEA MBIO ZA KUWANIA UBINGWA WA TPL MSIMU WA 2019 / 2020 TIMU YA WANANCHI INAFUNGUA DIMBA KWA KUJITUPA UWANJA WA BIBI KUKIPIGA NA RUVU SHOOTING HAPO 16:00HRS. KILA LA KHERI TIMU YA WANANCHI.
"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO.

Kila la heri timu ya wananchi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…