View attachment 1244440
MASHABIKI WASHAURIWA KUCHANGAMKIA TIKETI MAPEMA
Mashabiki wa klabu ya Yanga jijini Mwanza wametakiwa kuchangamkia kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza Jumapili ambayo ni siku ya mchezo dhidi ya Pyramids Fc
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema tiketi zinaanzwa kuuzwa leo kupitia vituo vilivyoainishwa na klabu hiyo jana
Viingilio vya mchezo huo ambao utapigwa saa 10 jioni ni Royal Tsh 50,000/-, VIP Tsh 20,000/- na Mzunguuko Tsh 7,000/- "Mashabiki wachangamke mapema kununua tiketi ili siku ya Jumapili wawe na zoezi moja tu, kwenda uwanjani kuishangilia timu yao," amesema "Hii itawaepusha na changamoto zinazoweza kujitokeza siku ya mchezo. Tutafunga zoezi la kuuza tiketi Jumapili mchana lakini inaweza kuwa mapema zaidi kama tiketi zitamalizika"
Vituo vinavyouza tiketi
1. Nyamagana
2. Kituo cha mabasi Nyegezi
3. Kituo cha mabasi Buzuruga
4. Kituo cha mabasi Igoma
5. Shule ya Msingi Buhongwa
6. Uwanja wa CCM Kirumba
7. Lenana Hotel Pasiasi
8. Posta Pamba Road
9. Kituo cha mabasi Mkolani
10. Kituo cha mafuta Buswelu