Shadeeya
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 49,759
- 118,798
Lamine atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga ambacho kitaikabili Pyramids Fc siku ya Jumapili Novemba 03 uwanja wa June 30 huko Misri
Wakati Lamine akirejea, Yanga itamkosa Kelvin Yondani ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa Mwanza
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema pamoja na kumkosa Yondani, hana wasiwasi na safu yake ya ulinzi baada ya Lamine kurejea
Katika mchezo uliopigwa jijini Mwanza, Yondani alishirikiana na Ali Ali safu ya ulinzi wa kati hivyo nafasi ya Yondani ni wazi itachukuliwa na Lamine
Wakati Yanga ikihitaji ushindi kwenye mchezo huo, safu ya ulinzi itakuwa na kazi ya ziada kuhakikisha hawaruhusu bao
Yanga wanahitaji angalau matokeo ya ushindi wa mabao 2-0 ili waweze kutinga hatua ya makundi