Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20191101_130449.jpg
Beki kisiki Lamine Moro amerejea kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United Septemba 28 nchini Zambia

Lamine atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga ambacho kitaikabili Pyramids Fc siku ya Jumapili Novemba 03 uwanja wa June 30 huko Misri

Wakati Lamine akirejea, Yanga itamkosa Kelvin Yondani ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa Mwanza

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema pamoja na kumkosa Yondani, hana wasiwasi na safu yake ya ulinzi baada ya Lamine kurejea

Katika mchezo uliopigwa jijini Mwanza, Yondani alishirikiana na Ali Ali safu ya ulinzi wa kati hivyo nafasi ya Yondani ni wazi itachukuliwa na Lamine

Wakati Yanga ikihitaji ushindi kwenye mchezo huo, safu ya ulinzi itakuwa na kazi ya ziada kuhakikisha hawaruhusu bao

Yanga wanahitaji angalau matokeo ya ushindi wa mabao 2-0 ili waweze kutinga hatua ya makundi
 
MECHI DHIDI YA PYRAMIDS KUPIGWA SAA TATU USIKU.

Mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho kati ya Pyramids Fc dhidi ya Yanga utapigwa keshokutwa Jumapili, Novemba 03 kwenye uwanja wa June 30, ukipangwa kupigwa saa tatu usiku kwa saa za Tanzania

Yanga wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-1 nyumbani hivyo wanafahamu ni mchezo ambao wanahitaji kushinda sio chini ya mabao mawili

Wachezaji wa Yanga wameapa kuwa watapigana kwa dakika zote tisini ili kuhakikisha wanapata matokeo yatakayowapeleka makundi

Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul, amesema kama Pyramids waliwafunga hapa Tanzania basi nao watahakikisha wanapata ushindi ugenini

Kama Yanga itafanikiwa kuwaondoa Pyramids Fc na kutinga makundi, watajihakikishia kitita cha Tsh Milioni 130 zilizotolewa ahadi na kampuni ya GSM (Mil 30) na kocha Mwinyi Zahera (Mil 100)
 
Wakuu nipo nimekaa tayari kwaajili yakucheki mechi lakini sioni dalili hivi inaanza saa ngapi?
 
MECHI DHIDI YA PYRAMIDS KUPIGWA SAA TATU USIKU.

Mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho kati ya Pyramids Fc dhidi ya Yanga utapigwa keshokutwa Jumapili, Novemba 03 kwenye uwanja wa June 30, ukipangwa kupigwa saa tatu usiku kwa saa za Tanzania

Yanga wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 2-1 nyumbani hivyo wanafahamu ni mchezo ambao wanahitaji kushinda sio chini ya mabao mawili

Wachezaji wa Yanga wameapa kuwa watapigana kwa dakika zote tisini ili kuhakikisha wanapata matokeo yatakayowapeleka makundi

Nahodha Msaidizi wa Yanga Juma Abdul, amesema kama Pyramids waliwafunga hapa Tanzania basi nao watahakikisha wanapata ushindi ugenini

Kama Yanga itafanikiwa kuwaondoa Pyramids Fc na kutinga makundi, watajihakikishia kitita cha Tsh Milioni 130 zilizotolewa ahadi na kampuni ya GSM (Mil 30) na kocha Mwinyi Zahera (Mil 100)
Mkuu chanel namba ngapi dstv inaonyeshwa
 
Back
Top Bottom