Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread


Mpe mfano wa kocha anaefundisha kupasiana (Wenger) na kocha anaebeba makombe (Mourinho)
 

Nilikuwa na pita hapo kwa mjomba michuzi nikaona hii picha ya mashujaa enzi hizo 1992 nazani hapa ni mahali pake.
Kutoka kushoto na Hamisi Gaga 'Gagarino' (marehemu), Saidi Mwamba 'kizota'(marehemu), David Mwakalebela,Method Mogela(marehemu),Abed Mziba, Ken Mkapa, na Salum Kabunda 'Ninja'. Na nyuma kwa mbali ni Steven Nemes.

Hii picha inanikumbusha mbali sana enzi hizo katika mitaa ya Sinza kijiweni daa kulikuwaga na vituko timuyako ikishidwa. Kulikuwa na mahali watu walikuwa wanasubiria kazi basi wengine ikawa kazi ni kubishana wiki nzima kati ya Simba na Yanga ilikuwa raha tupu kusikia wazee wa uswahilini wakibishana mwezi mzima mechi ikiisha daa. Ningeweza rudisha mda nyuma ningerudi enzi hizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…