Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

suala la viwango duni si hoja.....cha msingi kuijaza silverware cabinet!

angalia Man U kule ulaya wanavyofukuzia mataji matatu huku wakicheza kwa kiwango duni!

au umesahau pia Kili Stars walivyochukua Challenge cup na kiwango duni kabisa?

niendelee???

Mpe mfano wa kocha anaefundisha kupasiana (Wenger) na kocha anaebeba makombe (Mourinho)
 
simba%2Byanga.jpg

Nilikuwa na pita hapo kwa mjomba michuzi nikaona hii picha ya mashujaa enzi hizo 1992 nazani hapa ni mahali pake.
Kutoka kushoto na Hamisi Gaga 'Gagarino' (marehemu), Saidi Mwamba 'kizota'(marehemu), David Mwakalebela,Method Mogela(marehemu),Abed Mziba, Ken Mkapa, na Salum Kabunda 'Ninja'. Na nyuma kwa mbali ni Steven Nemes.

Hii picha inanikumbusha mbali sana enzi hizo katika mitaa ya Sinza kijiweni daa kulikuwaga na vituko timuyako ikishidwa. Kulikuwa na mahali watu walikuwa wanasubiria kazi basi wengine ikawa kazi ni kubishana wiki nzima kati ya Simba na Yanga ilikuwa raha tupu kusikia wazee wa uswahilini wakibishana mwezi mzima mechi ikiisha daa. Ningeweza rudisha mda nyuma ningerudi enzi hizo
 
Back
Top Bottom