Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Kabisa Mtani hata na mie naungana nawe kwani kwa sasa tunafurahia ila siku akifanya mbwembwe zake ambazo zitatugharimu ni lazima tumshushe thamani na kumzodoa juu.
Nimekubali Shadeeya wewe kweli soka unalijua na tabia za mashabiki piaunazijua. Miaka hiyo Juma Pondamali alitolewa uwanjani kwa escort ya polisi akiwa kipa wa Yanga baada ya kumletea mbwembwe marehemu Victor Sefwa Mkanwa African Sports, tena dakika za mwisho na jamaa akafunga goli la kusawazisha
 
We mpira unajua ,na uhakika kocha hata Jana hakuipenda hy

Ila jamaa MTU , hata yule Mzambia Erik nae mkali sana ujue this time Mtani uko vzr

MTC | 101| [emoji769]
Yah! Nadhani atamwambia ili asijelewa sifa zetu mashabiki mwishowe akaharibu.

Huyo Mzambia majuzi kocha alimuingiza dakika za mwisho ambapo sidhani hata kama mpira aliugusa hivyo nilishindwa hata kuona uchezaji wake akiwa Yanga.

Ila huenda akampanga siku moja na yeye tuuone motto wake. 😂😂
 
Hakika Ses Mbwembwe ni nzuri ila zikizidi kiasi zinagharimu.
 
Hakika Ses Mbwembwe ni nzuri ila zikizidi kiasi zinagharimu.
Unajua miaka ya nyuma wachezaji wa bongo walikua wanajua hasa kuuchezea mpira. Wakati ule watu walikwenda uwanjani kuangalia manjonjo ya kina Hamis Thobias Gaga "Gagrino" au Celestine "Sikinde" Mbunga na kabda ya hapo kina Juma Pondamali "Mensah" na wengineo wengi

Hawa waliujua mpira na mpira uliwajua. Kulikua na misamiati ya mpira kama "kanzu", tobo, tiktaka, chenga ya mwili na kadhalika ambazo siku hizi huzisikii kutokana na mabadiliko, na watu wakiyapenda sana hayo. Lakini sasa soka limebadilika Shadeeya.
Watu wanataka ushindi. Isitoshe kwa wenzetu wa Ulaya mchezaji mwenye manjonjo mengi inakua rahisi sana kuumizwa na club ikapata hasara baada ya kua imemnunua kwa pesa nyingi kwa hiyo makocha wanawakataza. Hata ule ushangiliaji wa kuruka samasoti wazungu hawautaki maana ikitokea mchezaji akiruka vibaya kisha akaumia timu ndio inakua imepata hasara. Upuuzi huo utauona Afrika tu

Brazil ilifanikiwa kujipatia mashabiki wengi dunia nzima kutokana na soka la namna hii, lakini wao pamoja na udambwidambwi wanafunga magoli. Tena utakuta timu nzima ni mafundi wa kuuchezea mpira, sio kama huku kwetu utakuta ni mchezaji mmoja mmoja tu ndio wana control ya mpira iliyokamilika
 
HAKUNA MCHEZAJI MKUBWA KULIKO YANGA - EYMAEL

“ Yondani alisema hawezi kucheza dhidi ya Azam, alidai anasumbuliwa na tumbo, baada ya hapo sijui nini kilitokea. Kwa siku sita siku simu yake ilikuwa imezimwa. Tulishindwa kuwasiliana naye kumpa taarifa za kwenda Singida. Baadaye alirejea klabuni na kusema anajisikia vizuri”

“Lazima watu wakubali kuwa tunatakiwa kwenda kwa mstari mmoja, sipangi jina, nachezesha timu. Hakuna aliye mkubwa kuliko timu. Sote tutapita hapa, Yanga itabaki hapa.”

Kocha wa Yanga, Luc Eymael akisisitiza hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya Yanga baada ya Yondani ‘kupotea’ klabuni kwa siku sita na kulazimika kumtumia Juma Makapu kama beki wa kati katika mechi dhidi ya Singida na Prisons.

@Yangadaima
 
Acha kucheka wewe kamwambie Kabwili alete ushahidi wa tuhuma dhidi ya mabingwa wa nchi Mnyama mkali Simba sc.😉

Simba nguvu moja
Nimecheka sana Mtani kuna sehemu Wana Simba wenzio wanamwaga matusi utadhania imethibitika Kabwili kaongopa. Tuacheni muda ndio utazungumza na kutenganisha pumba na mchele.

#Ilaaibusana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…