HAKUNA MCHEZAJI MKUBWA KULIKO YANGA - EYMAEL
“ Yondani alisema hawezi kucheza dhidi ya Azam, alidai anasumbuliwa na tumbo, baada ya hapo sijui nini kilitokea. Kwa siku sita siku simu yake ilikuwa imezimwa. Tulishindwa kuwasiliana naye kumpa taarifa za kwenda Singida. Baadaye alirejea klabuni na kusema anajisikia vizuri”
“Lazima watu wakubali kuwa tunatakiwa kwenda kwa mstari mmoja, sipangi jina, nachezesha timu. Hakuna aliye mkubwa kuliko timu. Sote tutapita hapa, Yanga itabaki hapa.”
Kocha wa Yanga, Luc Eymael akisisitiza hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya Yanga baada ya Yondani ‘kupotea’ klabuni kwa siku sita na kulazimika kumtumia Juma Makapu kama beki wa kati katika mechi dhidi ya Singida na Prisons.
@Yangadaima