Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Sisi kama Yanga tutakaa na Kabwili kuzungumza nae kwa undani, Kabwili ni Mchezaji wa Yanga Sc hivyo tutampa ushirikiano wa kutosha katika hili baada ya kumsikiliza.
Ni kweli wachezaji hawaruhusiwi kuongea na vyombo vya habari lakini kwa kuwa imetokea na Kabwili ni mchezaji wetu hayo mambo ni ya ndani ya klabu, lakini kuhusu hizo tuhuma tutashirikiana nae kuona mambo kama haya yanakoma kama ni kweli yapo.

Niwaombe wadau wenye ushahidi pia wajitokeze sio katika hili tu, hata vitendo vingine kama hivi ili tukomeshe mambo kama haya kwenye mpira wetu.

Hassan Mbumbuli- Afisa habari wa Yanga Sc
 
Hakika Mtani. Japo si ajabu pia yakaisha juu juu tu.

🤔🤔🤔 Hivyo hilo jina ndio linasomeka troizieme eee?
Ni kweli yanaweza yakaisha juu juu ila binafsi siamini kama tuhuma ni za kweli.

Hahaha jina linasomeka hivi 'twaiziem' hicho ni kifaransa
Troisième Ceil = Third Eye
 
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Bernard Morrison amesema anapofanya mbwembwe uwanjani halengi kuwadhihaki timu pinzani bali ni mahsusi kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki ambao wamelipa viingilio kuingia uwanjani

Aidha Bernard ameongeza kuwa hatafanya matukio hayo wakati wote, isipokuwa pale ambapo timu iko kwenye mazingira ya uhakika wa kuondoka na ushindi

Morrison ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kocha Luc Eymael kueleza kutofurahishwa na matukio hayo ambayo aliyafananisha na dhihaka kwa timu pinzani "Mashabiki wanakuja uwanjani kuona timu yao inashinda, ndio maana wanalipa viingilio, lakini ninapoona timu inaongoza vizuri huwa naona ni bora kufanya kitu ambacho kitawapa burudani zaidi mashabiki wakienda nyumbani wapate cha kusimulia zaidi," amefafanua Morrison. "Nafikiri kocha yeyote hawezi kukubali hilo moja kwa moja, namheshimu kocha wangu (Eymael) kwa alichoniambia, lakini kwangu nafikiri kuna kitu cha ziada natakiwa kukifanya kama mchezaji, sidhani kama naweza kuacha lakini nitakuwa makini wakati gani nafanya hivyo"

@Yangadaima
 
Hapo nimekubali amejibu vizuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…