Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Anajiona hata akiringa atabembelezwa.....Na pia amekuwa na makosa kiasi Kelvin nadhani Sonso aaminiwe kucheza maana ameimprove sana na anajihad sana currently
Umeonaeee. Mie naona ikiwezekana uongozi ikifikia kipindi cha usajili watafutage mbadala tu na hapo ndio akili itamkaa sawa.
 
Hivi hizo mechi ndio na za round ya pili zitakuwa zimeanza au sijaelewa mana Mbeya City tulishakipiga nao kule kwao Mbeya?
 
Hivi hizo mechi ndio na za round ya pili zitakuwa zimeanza au sijaelewa mana Mbeya City tulishakipiga nao kule kwao Mbeya?
Yaani hii bodi ya ligi inajijua yenyewe. Yaani raundi ya kwanza na ya pili humo humo. Mana kuna game wanamalizia za raundi ya kwanza na kuna game za raundi ya pili zitaendelea pia kama hao Mbeya city
 
SHIKALO KUWAKOSA MTIBWA SUGAR

Mlinda lango wa Yanga Farouk Shikhalo huenda atakosa mchezo wa iigi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa kesho Jumapili Feb 02 2020 baada ya kuruhusiwa kurejea Kenya kwenda kumuuguza Mama yake.

Wakati Shikhalo akikabiliwa na dharura hiyo, mlinda lango namba tatu Ramadhani Kabwili ataendelea kukosekana kwa kuwa anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu.

Kabwili, Cleofas Sospeter na Mrisho Ngasa walifungiwa mechi tatu pamoja na kutakiwa kulipa faini ya Tsh laki tano kila mmoja kutokana na makosa waliyofanya kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City.

Hata hivyo Yanga imekata rufaa kupinga adhabu zao.

Metacha Mnata anatarajiwa kuendelea kulinda lango la Yanga kwenye mchezo huo wakati mlinda lango kutoka kikosi cha pili huenda akaongezwa.

Aidha baadhi ya nyota waliokuwa majeruhi wamerejea kikosini. Wachezaji hao ni Mohammed Issa 'Banka', Tariq Seif na Juma Mahadhi aliyeanza mazoezi mepesi baada ya kukaa nje kwa miezi 18.
 
Yaani hii bodi ya ligi inajijua yenyewe. Yaani raundi ya kwanza na ya pili humo humo. Mana kuna game wanamalizia za raundi ya kwanza na kuna game za raundi ya pili zitaendelea pia kama hao Mbeya city
Hata na hiyo ya Prisons pia tulishacheza nao siku ile ambayo Uwanja uliharibiwa na Wasafi game ikachezewa Iringa kama unakumbuka hivyo ni marudiano nao pia.

Yaani Soka la Tanzania ni kichefu chefu.
 
Nguli wa mfumo wa soka la Kisasa yaani Modern Football fundi Carraca Antonio Domingoz Pinto ambaye alikuwa Mtendaji Mkuu (General Manager) wa Klabu Benfica ya Ureno kwa muongo mmoja (miaka 10) atua rasmi Dar es salaam ili kuanza kazi ya kushauri kueleka Mabadiliko ya kimfumo ya uendeshaji wa Klabu.. Shukran kwa Brand Chapa Gsm kwa kulisimamia hili.

"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

@Yangasc
 
Hata na hiyo ya Prisons pia tulishacheza nao siku ile ambayo Uwanja uliharibiwa na Wasafi game ikachezewa Iringa kama unakumbuka hivyo ni marudiano nao pia.

Yaani Soka la Tanzania ni kichefu chefu.
Sahihi!
 
Daaa itakaa poa sana kama azma hii ikitimia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…